Nani Anaweza Kutumia Tembe za Kuavya Mimba?

Awali nilifanyiwa ufungaji wa uzazi wa kike (ukataji mirija ya uzazi). Haikufanya kazi na nikawa mja mzito. Uja uzito ulikuwa katika mrija (uja uzito usio katika tumbo la uzazi). Sasa mimi ni mja mzito tena. Je ni salama kwangu kutumia tembe za kuavya mimba?

La, si salama kutumia tembe za kuavya mimba ikiwa unajua kuwa uko katika hatari ya kuwa na uja uzito usio katika tumbo la uzazi. Kwa sababu ulikatwa mirija ya uzazi, unajua kuna kovu katika mrija (futuza). Hiyo ndio maana labda uja uzito wako wa mwisho ulitokea nje ya tumbo la uzazi. Futuza ndipo yai la mwanamke linarutubishwa na mbegu za kiume. Uja uzito unaanza kukua na husafiri katika mrija hadi tumbo la uzazi. Ikiwa mrija wako una kovu, uja uzito wa awali unaweza ukanaswa katika mrija. Uja uzito unapokua, unaweza kusababisha mrija kupasuka. Ikiwa mrija utapasuka, hii inaweza kusababisha umwagikaji wa damu ndani yako, na ni tishio kwa maisha yako. Uko katika hatari ya kupata uja uzito mwingine nje ya tumbo la uzazi. Haustahili kutumia tembe za kuavya mimba hadi mhudumu wa afya ahakikishe kuwa uja uzito uko katika tumbo la uzazi na si katika mirija yako.


References

This website may require anonymous cookies and various third party services to function properly. You can read our Terms & Conditions and Privacy Policies. By continuing to use this site you are giving us your consent to do this.