Je, ni salama kufanya uavyaji mimba kwa dawa kati ya wiki ya 10 hadi 13?
Utoaji mimba kwa kutumia vidonge katika hatua za awali za ujauzito huwa na uwezekano
mdogo wa kusababisha madhara. Hatari ya kupata matatizo, ikama vile tatizo la utoaji
mimba kuto kamilika, huongezeka kadri ujauzito unavyoendelea kukua. Kwa mfano,
ujauzito wa chini ya wiki tisa una kiwango cha matatizo cha chini ya 1%, ilhali
ujauzito wa kati ya wiki 10–13 una kiwango cha matatizo cha hadi 3%.
Nitaona nini wakati wa uavyaji mimba kwa dawa kati ya wiki ya 10 hadi 13?
Utoaji mimba kwa njia ya vidonge hupelekea kutokwa na damu. Damu hii inaweza kuwa
nzito zaidi kuliko hedhi yako ya kawaida na inaweza kuwa na mabonge ya damu. Katika
utoaji mimba kati ya wiki 10–13, unaweza kuona mabaki ya mimba yanayotambulika, au
yanaweza kuonekana tu kama tishu au mabonge ya damu. Hili ni jambo la kawaida na
halipaswi kukutia hofu. Ni ishara kwamba utoaji mimba unafanyika kama inavyotarajiwa.
Kama ilivyo kwa hedhi nzito, unaweza kutupa mabonge makubwa ya damu au tishu kwenye
choo kwa usalama. Ikiwa unaishi katika nchi ambayo utoaji mimba au vidonge vya kutoa
mimba ni haramu, hakikisha unatupa mabaki yoyote yanayotambulika kwa uangalifu na
kwa siri.
Waandishi:
Yote yaliyomo kwenye wavuti hii yameandikwa na timu ya HowToUseAbortionPill.org kwa kufuata viwango na itifaki kutoka Shirikisho la Kitaifa la Utoaji Mimba, Ipas, Shirika la Afya Ulimwenguni, DKT Kimataifa na carafem.
Marejeo:
- “Safe abortion: technical and policy guidance for health systems.” World Health Organization. https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/;jsessionid=B7AEEBE4F34809D869F73B1ABA7F6221?sequence=1
- “Clinical updates in reproductive health.” Ipas. https://www.ipas.org/resource/clinical-updates-in-reproductive-health/
- “Clinical policy guidelines for abortion care.” National Abortion Federation (NAF). https://5aa1b2xfmfh2e2mk03kk8rsx-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2018_CPGs.pdf