Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Tembe za Kuavya Mimba

Nani Anaweza Kutumia Tembe za Kuavya Mimba?

    La, tumia idadi sawa ya tembe tunazopendekeza kwa kila mtu. Tafiti zinaonyesha kuwa ufanisi wa dawa haupungui kwa wanawake wanene au wanaozidi uzani. Hauhitaji kumeza kipimo tofauti au kumeza tembe Zaidi.

    Hauhitaji kubadili kipimo au idadi ya tembe ikiwa umegundua kuwa una mimba ya mapacha. Utaratibu unaofanana ndio hutumika kwa wanawake wenye mimba za mapacha.

    La, kila mimba ni tukio la kipekee. Ikiwa uliwahi kutumia tembe ya kuavya mimba awali, hauhitaji kipimo zaidi ikiwa utaitumia tena kwa mimba tofauti isiyohitajika.

    Ikiwa una kidude cha kuzuia mimba katika tumbo la uzazi (kama vile koili au IUD ya progesterone ), ni lazima ukitoe kabla ya matibabu ya kuavya mimba

    Ikiwa unanyonyesha mtoto, tembe za misoprostol zinaweza kusababisha mtoto kuhara. Ili kuzuia hii, nyonyesha mtoto, meza tembe za misoprostol, kisha subiri saa 4 kabla ya kumnyonyesha tena.

    Ikiwa unaishi na HIV, hakikisha kuwa uko hali dhabiti, unatumia dawa za kupunguza makali ya virusi, na kuwa afya yako ni nzuri.

    Kama una anemia (viwango vidogo vya madini katika damu yako), tambua mhudumu wa afya asiye zaidi ya dakika 30 mbali nawe ambaye anaweza kukusaidia ukiitaji msaada. Ikiwa umezidiwa na anemia, tafuta ushauri wa daktari kabla ya kutumia tembe ya kuavya mimba.

    La, kutumia tembe za kuavya mimba mapema unapokuwa mja mzito ni salama hata kama ulijifungua kwa njia ya upasuaji.

    Hakuna uhusiano ambao umepatikana kati ya mifepristone na kasoro za kuzaliwa. Hata hivyo misoprostol huwa inasababisha kiwango kidogo cha ongezeko za kasoro za kuzaliwa. Kama utameza misoprostol na bado ungali mja mzito baada ya kumeza tembe, unaweza kupoteza mimba kwa njia ya kawaida. Ikiwa hautapoteza mimba hiyo na uwe nayo hadi wakati utimie, hatari ya kasoro za kuzaliwa huongezeka kwa 1% (mtoto mmoja kwa kila 100).

    La, si salama kutumia tembe za kuavya mimba ikiwa unajua kuwa uko katika hatari ya kuwa na uja uzito usio katika tumbo la uzazi. Kwa sababu ulikatwa mirija ya uzazi, unajua kuna kovu katika mrija (futuza). Hiyo ndio maana labda uja uzito wako wa mwisho ulitokea nje ya tumbo la uzazi. Futuza ndipo yai la mwanamke linarutubishwa na mbegu za kiume. Uja uzito unaanza kukua na husafiri katika mrija hadi tumbo la uzazi. Ikiwa mrija wako una kovu, uja uzito wa awali unaweza ukanaswa katika mrija. Uja uzito unapokua, unaweza kusababisha mrija kupasuka. Ikiwa mrija utapasuka, hii inaweza kusababisha umwagikaji wa damu ndani yako, na ni tishio kwa maisha yako. Uko katika hatari ya kupata uja uzito mwingine nje ya tumbo la uzazi. Haustahili kutumia tembe za kuavya mimba hadi mhudumu wa afya ahakikishe kuwa uja uzito uko katika tumbo la uzazi na si katika mirija yako.

    Kwanza, unastahili kujua kuwa wanawake wengi hawawezi kujua wako katika hali hii hadi wafanyiwe kipimo cha idadi ya marudio ya mawimbi ya sauti. Uja uzito nje ya tumbo la uzazi hauwezi kudumu hivyo hata katika nchi ambapo uaviaji mimba ni kinyume cha sheria wanawake wanaweza kuwa na utaratibu wa kisheria kwa kutamatisha huu uja uzito.

Aina ya Tembe za Kuavya Mimba na Matumizi Yake

    Kuna aina mbili ya tembe za kuavya mimba, na kila moja ina mbinu tofauti ya utenda kazi. Mifepristone huzuia homoni zinazohitajika kwa ukuaji wa uja uzito, ilhali virutubishi vinavyotumika katika misoprostol hufanya kazi kwa kulegeza na kufungua mlango wa tumbo la uzazi (mwanya katika tumbo la uzazi) na kusababisha tumbo la uzazi kujikaza, na hivyo kusukuma uja uzito nje.

    Misoprostol husababisha tumbo la uzazi kujikaza na hivyo kutoa uja uzito.

    Mifepristone huzuia homoni zinazohitajika kwa ukuaji wa mimba

    Ndio, unaweza kutumia misoprostol salama ukiwa nyumbani. Unapotumia tembe za misoprostol, jaribu kuhakikisha kuwa uko katika sehemu (kama kwako nyumbani) ambapo una ufaragha na unaweza kulala chini kwa saa chache baada ya kumeza tembe. Kuwa na mtu karibu nawe anayeweza kukuangalia na kukuletea chai moto au kitu cha kula inaweza kusaidia sana.

    Usinywe au kula kitu chochote kwa dakika 30 unaporuhusu misoprostol kuyeyuka. Baada ya dakika 30 kupita, unaweza kunywa maji ili kumeza mabaki ya tembe, na kwa jumla kiasi cha maji unachostahili ili kuhisi mwili una maji ya kutosha.

    Ndio, unaweza kunywa maji kukusaidia kumeza mifepristone.

    Kuna njia mbili za kutumia misoprostol: kuweka tembe katika uke wako au chini ya ulimi wako. Jinsi ya kutumia inapendekeza kuwa utumie tu misoprostol chini ya ulimi wako kwa sababu ni faragha zaidi (tembe huyeyuka haraka na haziachi alama zinazoonekana katika mwili wako) na huwa na hatari ndogo la ambukizo.

    Mchanganyiko wote wa jumla ya mifepristone na misoprostol na misoprostol- ndio tu maamuzi yenye ufanisi. Hata hivyo, ikiwa inapatikana na unaweza kumudu gharama, mchanganyiko wa mifepristone na misoprostol unastahili kuwa uamuzi wako unaopendelewa.

    Wanawake 98 kati ya 100 huwa na uaviaji mimba kamili ikiwa mifepristone na misoprostol zimetumika kwa pamoja. Takriban wanawake 95 kati ya 100 watakuwa na uaviaji mimba kamili ikiwa tu misoprostol inatumika.

    Mifepristone na misoprostol hutumika pamoja kwa sababu tembe hizi hukamilishana. Dawa inayotumika katika misoprostol hufanya kazi kwa kulegeza na kufungua mlango wa uzazi (kufungua tumbo la uzazi) na kusababisha tumbo la uzazi kujikaza, hivyo kusukuma nje uja uzito.

    Ikiwa utatumia tembe za misoprostol chini ya ulimi wako, hakuna mtu anaweza kujua kuwa ulitumia tembe za kuavya mimba kwa sababu utameza kila kitu baada ya dakika 30. Ikiwa mtu atauliza, unaweza kusema ulipoteza mimba kwa njia ya kawaida. Ikiwa utatumia misoprostol kupitia uke, koti ya tembe huenda isiyeyuke kabisa kwa siku moja au mbili. Ikiwa unahitaji kutafuta usaidizi wa kiafya wa dharura kati ya saa 48 kwa sababu ulitumia misoprostol kupitia uke, mhudumu wa afya anaweza kuona koti nyeupe za tembe katika uke wako. Hii ndio maana jinsi ya kutumia hupendekeza kutumia misoprostol chini ya ulimi wako na si ndani ya uke wako.

Matumizi ya tembe za kuavya mimba kinyume na maelekezo

    Unastahili kuepuka kutumia tembe za kuavya mimba ikiwa una uja uzito wa zaidi ya wiki 13; ikiwa unaathiriwa na mifepristone au misoprostol; una matatizo ya kina ya kiafya kama vile shida za kuganda kwa damu; au ikiwa unaamini au unajua kuwa uja uzito unakua nje ya tumbo la uzazi (uja uzito katika mrija wa uzazi)

Madhara na Matatizo ya Tembe za Kuavya Mimba

    Kwa baadhi ya wanawake, msokoto huwa mkali- zaidi ya msokoto wa hedhi (ikiwa una msokoto wa hedhi) na umwagikaji damu huwa zaidi ya ule wa hedhi. Unaweza kupitisha donge la damu hadi kiasi cha limau katika saa za kwanza baada ya kumeza misoprostol. Kwa wanawake wengine, msokoto huwa hafifu na umwagikaji wa damu huwa kawaida kama hedhi.

    Tafuta msaada wa kiafya ikiwa hauna umwagikaji wa damu au una umwagikaji mdogo wa damu unaofuatwa na maumivu makali (hasa katika bega la kulia) ambayo hayapunguzwi na ibuprofen . Hii inaweza kuwa dalili ya uja uzito ulio nje ya tumbo la uzazi, na inaweza kuwa tishio la maisha. Unaweza pia kuwafikia marafiki zetu katika www.safe2choose.org ili kuongea na mshauri wa uaviaji mimba aliye na mafunzo ikiwa unahisi kuwa uaviaji mimba haukufanikiwa.

    Tafuta msaada wa kiafya ikiwa unalowa baada ya kutumia visodo viwili baada ya saa 2 mfululizo baada ya kufikiri uja uzito ushatoka. Kulowa kunamaanisha kuwa kisodo kimejaa damu mbele – hadi – nyuma, upande- hadi – upande na kupita- hadi – kupita.

    Meza tembe 3-4 (200 mg) baada ya kila saa 6-8 ili kusaidia kuondoa maumivu yako. Kumbuka kuwa unaweza kumeza ibuprofen kabla ya kutumia misoprostol, pia

    Baada ya misoprostol kuyeyuka, unaweza kula unavyotaka. Vyakula vilivyokauka (kama vile vilivyookwa au kuchomwa) vinaweza kusaidia kichefuchefu, ilhali mboga, mayai na nyama nyekundu inaweza kurejesha madini yaliyopotea wakati wa kuavya mimba.

    Baada ya misoprostol kuyeyuka, unaweza kunywa kinywaji unachokipenda (isipokuwa pombe).

    Pombe inastahili kuepukwa wakati wa matibabu ili kuzuia kuathiri ufanisi wa matibabu. Pombe inaweza kusababisha ongezeko la umwagikaji wa damu kutoka kwa tumbo la uzazi katika hali zingine na kupunguza ufanisi wa dawa zingine zinazomezwa kupunguza maumivu au ambukizo (kwa wanawake wanaokabili matatizo). Kwa jumla, inapendekezwa kuepuka pombe hadi uthibitishe kuwa uaviaji mimba umekamilika na unahisi ukiwa na afya nzuri.

    Wanawake wengi watapitisha uja uzito baada ya saa 4-5 na kuhisi vyema chini ya saa 24. Ni kawaida kuendelea kuona umwagikaji mdogo wa damu na madoadoa hadi hedhi yako inayofuata takriban wiki 3-4.

    Ni kawaida kuhisi kuwa mgonjwa kwa tumbo lako, kuhara, kibaridi, au hata kuhisi una joto katika kipindi hiki. Wanawake wengi wanaripoti kuwa wanajua kuwa wamepitisha mimba kwa sababu umwagikaji wa damu unapungua, na wanaanza kuhisi vyema zaidi.

    Baadhi ya wanawake wanaweza wakahitaji utaratibu wa upasuaji ikiwa bado wana uja uzito baada ya kumeza tembe. Kumbuka! Matibabu ya uaviaji mimba yasiyokamilika yanapatikana kwa urahisi popote duniani. Una haki kupata huduma hii, hata kama uaviaji mimba umebanwa kisheria katika nchi yako.

Utoaji mimba kwa matibabu na kuzaa baadaye

    Unaweza kupata na uja uzito haraka hata baada ya siku 8 baada ya matibabu ya uaviaji mimba. Ikiwa utafanya ngono, unastahili kuzingatia kutumia mbinu za kupanga uzazi ili kuzuia mimba zisizotarajiwa.

    La, tembe za kuavya mimba hazisababishi kasoro za kuzaliwa katika mimba za siku za usoni.

    La, kuwa na uaviaji mimba kwa tembe haiwezi kuifanya vigumu kupata uja uzito katika siku za usoni.

Maswali Mengine Yanayoulizwa Mimba

    Mbinu za uaviaji mimba hazistahili kuchanganyishwa na mbinu za kuzuia mimba (mbinu za kupanga uzazi, ikijumuishwa na upangaji uzazi wa dharura). Mbinu za kupanga uzazi hufanya kazi kwa kuzuia kuachiliwa kwa ovari (kuachiliwa kwa yai) au kwa kuzuia yai na mbegu za kiume kukutana. Mbinu za kupanga uzazi, ikijumuisha upangaji uzazi wa dharura, haziwezi kutumika kutamatisha au kuhitilafiana na mimba iliyotungwa. Unaweza kutembelea www.findmymethod.org ili kujifunza mengi kuhusu mbinu za kupanga uzazi.

    Tembe za upangaji uzazi wa dharura (ECPs) ni salama na njia faafu za kuzuia mimba baada ya kujamiiana bila kinga. Hufanya kazi kwa kuzuia kuachiliwa kwa ovari (kuachiliwa kwa yai) au kwa kuzuia yai na mbegu za kiume kukutana. ECPs haziwezi kutamatisha ama kuhitilafiana na mimba iliyotungwa. ECPs ni tofauti na taratibu za kiafya zilizowekwa (ambazo hujumuisha mifepristone na misoprostol). Matibabu haya yana manufaa ya pekee kwa afya ya uzazi wa wanawake kote duniani.

    Kuna njia mbili zitumikazo sana katika mbinu za uaviaji mimba
    1) Matibabu ya uaviaji mimba: matibabu ya kuavya mimba hutumia madawa ya kibaolojia ili kutamatisha uja uzito. Wakati mwingine dhana “ uaviaji mimba pasi upasuaji” au uaviaji mimba kwa tembe” pia huwa zinatumika.

    2) Uaviaji mimba kwa upasuaji: Katika taratibu za uaviaji mimba kwa upasuaji, mtaalamu aliyehitimu atamwaga uja uzito kutoka kwa tumbo la uzazi kupitia mlango wa uzazi ili kutamatisha uja uzito. Taratibu hizi hujumuisha ufyonzaji ombwe usiootomatiki (MVA) na upanuzi na uondoaji (D&E).

HowToUseAbortionPill.org inashirikiana na shirika lisilo la faida lililosajiliwa huko Amerika-501c (3)
HowToUseAbortionPill.org hutoa yaliyomo yaliyokusudiwa kwa sababu ya habari tu na haihusiani na shirika la matibabu.