Baada ya Kutumia tembe za Kutoa Mimba

Kuna njia mbili za utoaji mimba wa kimatibabu-mifepristone na misoprostol ama misoprostol pekee.Njia zote ni bora kabisa: Kile utakachohisi na kupitia baada ya kutumia tembe hizi kinaweza kutofautiana.

Utajisikiaje baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba?
Kuwa mwangalivu?
After Use Pills

Utajisikiaje baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba?

Baada ya kutumia Mifepristone

Unaweza kutokwa damu kidogo baada ya kumeza mifepristone. Hata hivyo, ni jambo la kawaida iwapo hautatokwa damu.

Baada ya kutumia Misoprostol

Maumivu ya tumbo na kutokwa damu ndio matokeo makubwa. Dalili hizi ni nzuri kwa sababu zinaonyesha kuwa dawa inafanya kazi. Lakini, ni kwa kiasi gani utapata maumivu ya tumbo na kutokwa na damu?

Kwa wanawake wengine, maumivu ya tumbo ni makali sana – zaidi kuliko maumivu wakati wa hedhi (kama unapata maumivu ya tumbo wakati wa hedhi).

Kwa wanawake wengine, damu hutoka nyingi kuliko inayotoka wakati wa hedhi. Pia ni kawaida kufuja damu saa chache ya mwanzo baada ya kunywa misoprostol. Wingi wa damu utalingana na umri wa mimba.

Kwa wanawake wengine, maumivu ni kidogo na damu inayotoka sawa na ile ya wakati wa hedhi.

Usishtuke ukitokwa na damu zaidi kuliko hedhi ya kawaida.

Ukipata maumivu makali ya tumbo, dawa ya Ibuprofen ni dawa nzuri kupunguza maumivu. Unaweza kununua Ibuprofen ya milligram 200 bila ya karatasi ya dawa kutoka kwa daktari kwenye nchi nyingi. Tumia vidonge 3-4 kila baada ya saa 6-8. Hii itakusaidia kupunguza maumivu ya tumbo.

Unaweza Kula na kukunywa jinsi unavyotaka

Jaribu kupumzika na kutulia mpaka utakapohisi nafuu

Unapaswa kuhisi nafuu chini ya saa ishirini na manne( 24)

Angalizo:

Wiki 3-4 baada ya kutoa mimba, vipimo vitaendelea kuonyesha kua bado una ujauzito kwasababu ya homoni zilizobaki ndani ya mwili wako. Wakati mwingine, vipimo vinaweza kuonyesha una mimba hadi baada ya wiki 6. Kama bado utaendelea kuhisi dalili za ujauzito (ulaini wa matiti, kichefuchefu, uchovu n.k) baada ya kutumia vidonge, fanya kipimo cha ultrasound ili kubaini ikiwa utoaji mimba ulifaulu.

Dalili baada ya kutumia tembe ya kutoa mimba na Madhara za tembe ya kutoa mimba

Wakati mimba inavyotoka, dalili hapo juu ni kawaida. Kuwa makini. Chini ni baadhi ya ishara kwamba unaweza kuwa katika hatari ya kupata matatizo makumbwa.

Kutokwa damu nyingi.

Iwapo utalowesha vitamba viwili vya hedhi kila saa moja kwa saa 2 mfululizo baada ya kudhania kwamba ushaavya mimba, hii ni ishara ya kufuja damu kwa wingi.Unatakiwa kupata msaada wa kitabibu kama unatoka damu nyingi kiasi hiki. Kuloanisha pedi inamaanisha pedi kubwa yote imeloana damu mbele na nyuma, pembeni na pembeni na juu mpaka chini.

Maumivu Makali:

Kama unapata maumivu makali sana ambayo hayapungui hata baada ya kunywa dawa ya Ibuprofen, pata msaada wa kitabibu. Maumivu makali sana huenda ikamaanisha umepata matatizo makubwa ya mimba. Maumivu yasiyopungua ambayo hayapungui hata baada ya kunywa dawa ya Ibuprofen inaweza kuwa dalili ya hatari. Tunashauri mtu yeyote mwenye mimba anayepata maumivu atafute msaada wa kitabibu.

Unajihisi mgonjwa sana.

Unaweza kupata homa, kichefuchefu na kutapika siku ambayo umekunywa misoprostol. Hii ni jambo la kawaida. Unatakiwa kujisikia nafuu zaidi kila siku baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba. Haupaswi kujihisi mgonjwa. Kama utajisikia kuumwa zaidi siku yoyote baada ya kumeza misoprostol unahitaji kutafuta msaada wa kitabibu.

Waandishi:

  • Yote yaliyomo kwenye wavuti hii yameandikwa na timu ya HowToUseAbortionPill.org kwa kufuata viwango na itifaki kutoka Shirikisho la Kitaifa la Utoaji Mimba, Ipas, Shirika la Afya Ulimwenguni, DKT Kimataifa na carafem.
  • Shirikisho la Kitaifa la Kutoa Mimba (NAF) ni chama cha kitaalam cha watoaji mimba huko Amerika ya Kaskazini, na kiongozi katika harakati za uchaguzi. Yaliyomo kwenye HowToUseAbortionPill.org inahusiana na Miongozo ya Sera ya Kliniki ya mwaka 2020 iliyotolewa na NAF.
  • Ipas ndio shirika pekee la kimataifa linalolenga tu kupanua ufikiaji wa utoaji salama wa mimba na uzazi wa mpango. Yaliyomo kwenye HowToUseAbortionPill.org inahusiana na Sasisho za Kliniki Katika Afya ya Uzazi 2019 iliyotolewa na Ipas
  • Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ni wakala maalum wa Umoja wa Mataifa unaohusika na afya ya umma ya kimataifa. Yaliyomo kwenye HowToUseAbortionPill.org inahusiana na Utoaji mimba salama wa mwaka 2012: mwongozo wa kiufundi na sera kwa mifumo ya afya iliyotolewa na WHO.
  • DKT International ni shirika lisilo la faida lililosajiliwa mnamo mwaka 1989 ili kuzingatia nguvu ya uuzaji katika jamii katika baadhi ya nchi kubwa zilizo na mahitaji makubwa ya uzazi wa mpango, kinga ya VVU / UKIMWI na utoaji mimba salama.
  • carafem ni mtandao wa kliniki unaotoa utalaam wa kufaa wa utoaji mimba salama na uzazi wa mpango ili watu waweze kudhibiti idadi na nafasi ya watoto wao.

Marejeo:

HowToUseAbortionPill.org inashirikiana na shirika lisilo la faida lililosajiliwa huko Amerika-501c (3)
HowToUseAbortionPill.org hutoa yaliyomo yaliyokusudiwa kwa sababu ya habari tu na haihusiani na shirika la matibabu.

Powered by Women First Digital