Uaviaji Mimba kwa Utabibu kwa Uja Uzito Kati ya Wiki 10 na 13

Mimba zilizo kati ya wiki 10 na 13 bado zinaweza kutamatishwa salama na kwa ufanisi kwa kutumia tembe za kuavya mimba kwa utabibu, lakini kuna baadhi ya vigezo vya pekee vinavyohitaji kuzingatiwa.

Pregnancies between 10-13 weeks

Usalama wa Uaviaji Mimba kwa Utabibu Kila Wiki

Uaviaji mimba unaotokea awali katika uja uzito huwa na hatari ndogo ya kuwa na utata. Hatari ya utata huongezeka kadri mimba inavyoendelea kukua. Chati iliyopo chini inaonyesha jinsi hatari ya utata inavyoongezeka na muda wa uja uzito. Ingawa hatari haitokei katika mimba zinazofuata, uaviaji mimba katika wiki 13 bado unaangaziwa kuwa salama.

Utaona Nini Wakati Wa Uaviaji Mimba Baada ya Wiki 10?

Uaviaji mimba kwa utabibu unawasababisha wanawake kuvuja damu. Hii kuvuja damu inaweza kuwa zaidi kuliko hedhi yako ya kawaida na inaweza kujumuisha damu iliyokolea. Inawezekana kwa wanawake walio na uja uzito wa wiki 10-13 kuona kitu kinachoweza kutambulika, au kinachoonekana kama vijinyama. Hii ni kawaida na haistahili kukutia hofu. Ni ishara kuwa uaviaji mimba unaendelea ilivyotarajiwa. Kwa hedhi nzito, unaweza kutupa damu nyingi iliyokolea au vijinyama chooni salama. Ikiwa unaishi katika nchi ambapo uaviaji mimba ni kinyume cha sheria, hakikisha kuwa unatupa kitu chochote kinachotambulika kwa makini na kisiri.

Waandishi:

Marejeo: