
Namna Inavyofanya kazi
Dawa zinazotumika kutoa mimba zinafanya kazi kwa kulegeza na kufungua taratibu shingo ya mfuko wa kizazi (mlango wa kizazi), na kusababisha mfuko wa kizazi kukaza ambayo inasukuma mimba nje ya kizazi.
Kwa kutumia Misoprostol, kwa kawaida katika saa 1 au 2 baada ya vidonge vya kwanza kuingia mwilini mwako, utaanza kuumwa tumbo na damu kutoka. Kwa kawaida mimba itatoka ndani ya masaa 24 baada ya kunywa vidonge vya mwisho vya misoprostol, mara nyingi mimba inatoka kabla ya muda huo.
Kama una shaka
Kama unafuatilia vizuri, unaweza kujua mabaki ya mimba yanavyotoka. Unaweza kuona vitu kama vile zabibu ndogo nyeusi kidogo na utando mwembamba, au kifuko kidogo kilichozungukwa na utando mlaini mweupe. Kutegemeana na umri wa mimba, tishu hizi zinaweza kuwa ndogo kuliko ukucha wako hadi kufikia ukubwa wa kidole gumba. Kama unaweza kutambua mabaki haya, ni dalili kuwa utoaji mimba umefanikiwa. Mara nyingi mabaki ya mimba yanaweza kuwa ndani ya mabonge ya damu. Unaweza usione mabaki haya isipokuwa ukiwa makini sana.
Marejeo:
- “Induced Abortion.” American College of Obstetrics and Gynecologists.
https://www.acog.org/Patients/FAQs/Induced-Abortion - “Care for Women Choosing Medication Abortion.” The Nurse Practitioner.
https://journals.lww.com/tnpj/Citation/2004/10000/Care_for_Women_Choosing_Medication_Abortion.9.aspx - “Safe abortion: technical and policy guidance for health systems.”The World Health Organization.
https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/?sequence=1