Mimba kikokotoleo (calculator)
Ujauzito wako ni wa muda gani? Utafiti unaonyesha kuwa mara nyingi utoaji mimba kwa kutumia vidonge unapendekezwa kwa mimba zenye umri chini ya wiki 13. Tumia kikokotoleo (calculator) hiki kujua ujauzito una muda gani?
Ikiwa kipindi chako cha mwisho kilianza tarehe au baadaye:
24 Februari 2023
Bado unaweza kuzingatia utumiaji wa kidonge cha kutoa mimba
Vya Kuzingatia
Wakati unaposumbuliwa na IUD (KITANZI)
Wakati ambapo unaishi na VVU
Kama unajali faragha yako
Wakati unaponyonyesha
Wakati unaposumbuliwa na upungufu wa damu
Ushauri Wa Jumla
Kutengeneza mpango wa usalama
Kulingana na shirika la Marekani la uzazi na jinakolojia, uavyaji wa mimba iliyo miezi mitatu au chini kwa kutumia tembe ni mojawapo ya taratibu za tiba salama . Hata hivyo, unapaswa kutayarisha ipasavyo kwa matibabu ya dharura kama itakavyohitajika. Zingatia maswali yetu hapa chini ili kusaidia kutengeneza mpango wako wa usalama iwapo kama utakavyohitaji.
Unahitaji kuwa na uwezo wa kufika kwenye kituo nkwa saa 1 au chini. (Kama una upungufu wa damu, unapaswa kuwa na uwezo wa kufika huko kwenye kituo kwa dakika 30.)
Je, kuna mtu atakayekuwa nawe na anayeweza kukufikisha kwa gari? Je, utachukua teksi? Utatumia Usafiri wa umma? Itagharimu pesa ngapi na je, inapatikana masaa ishirini na manne(24hours)? Kumbuka, sio salama kuendesha gari mwenyewe kwenda hospitalini wakati wa dharura ya matibabu.
Uavyaji wa mimba kutumia tembe una vikwazo vya kisheria nchini mwako? Ni nini utakachowaeleza wahudumu wa afya na madakatari ili waweze kuelewa msaada unaohitaji, huku ukilinda usalama na siri yako? Tuna baadhi ya mapendekezo iwapo unahitaji msaada wa taarifa na habari za kutoa inapohitajika.
Utakachowaambia wahudumu wa afya Katika baadhi ya nchi, kuavya mimba ukitumia tembe ni kinyume cha sheria. Hii ina maana kwambwa utakapohitaji msaada wa matibabu ya dharura, uwe mwangalifu unachosema. Kuavya mimba kw akutumia madawa kuna ishara sawa na mimba inayotoka kwa njia ya kawaida( pia hujulikana kama avyaji kwa hiari). Tumetayarisha baadhi ya majibu ambayo unaweza ukatumia:
- Sina uhakika kinachoendelea , nimeanza kufuja damu kwa ghafla
- Nina fuja damu lakini sidhani kwamba ni hedhi ya kawaida
- Nimeanza kufuja damu kwa ghafla na ninahofu kwamba kuna shida
Marejeo:
- “Induced Abortion.” American College of Obstetrics and Gynecologists. https://www.acog.org/Patients/FAQs/Induced-Abortion
- “Care for Women Choosing Medication Abortion.” The Nurse Practitioner. https://journals.lww.com/tnpj/Citation/2004/10000/Care_for_Women_Choosing_Medication_Abortion.9.aspx
- “Safe abortion: technical and policy guidance for health systems.”The World Health Organization. https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/?sequence=1