Kuhusu Dawa Za Kutoa Mimba

Responsive image

Nchi nyingi zina sheria zake zinazohusiana na upatikanaji na matumizi ya vidonge vya kutoa mimba. Kwenye nchi ambazo utoaji mimba unaruhusiwa, madaktari wengi hupendekeza kutumia dawa za utoaji mimba mifepristone na misoprostol ndani ya wiki 11 za mwanzo za mimba, lakini misoprostol ina ufanisi mkubwa pia kama unajaribu kutoa mimba ndani ya wiki 11 za mwanzo. Dalili zake ni sawa sawa na zile za mimba kuharibika, na dawa za utoaji mimba ni salama kwa wanawake kutumia faragha.

Dawa zinazotumika kutoa mimba zinafanya kazi kwa kulegeza na kufungua taratibu shingo ya mfuko wa kizazi (mlango wa kizazi), na kusababisha mfuko wa kizazi kukaza ambayo inasukuma mimba nje ya kizazi.

Kwa kutumia Misoprostol, kwa kawaida katika saa 1 au 2 baada ya vidonge vya kwanza kuingia mwilini mwako, utaanza kuumwa tumbo na damu kutoka. Kwa kawaida mimba itatoka ndani ya masaa 24 baada ya kunywa vidonge vya mwisho vya misoprostol, mara nyingi mimba inatoka kabla ya muda huo.

Responsive image
Responsive image

Kama unafuatilia vizuri, unaweza kujua mabaki ya mimba yanavyotoka. Unaweza kuona vitu kama vile zabibu ndogo nyeusi kidogo na utando mwembamba, au kifuko kidogo kilichozungukwa na utando mlaini mweupe. Kutegemeana na umri wa mimba, tishu hizi zinaweza kuwa ndogo kuliko ukucha wako hadi kufikia ukubwa wa kidole gumba. Kama unaweza kutambua mabaki haya, ni dalili kuwa utoaji mimba umefanikiwa. Mara nyingi mabaki ya mimba yanaweza kuwa ndani ya mabonge ya damu. Unaweza usione mabaki haya isipokuwa ukiwa makini sana.


References:

This website may require anonymous cookies and various third party services to function properly. You can read our Terms & Conditions and Privacy Policies. By continuing to use this site you are giving us your consent to do this.