Madhara na Matatizo ya Tembe za Kuavya Mimba

Ni umwagikaji upi wa damu au msokoto ni kawaida baada ya kumeza misoprostol?

Kwa baadhi ya wanawake, msokoto huwa mkali- zaidi ya msokoto wa hedhi (ikiwa una msokoto wa hedhi) na umwagikaji damu huwa zaidi ya ule wa hedhi. Unaweza kupitisha donge la damu hadi kiasi cha limau katika saa za kwanza baada ya kumeza misoprostol. Kwa wanawake wengine, msokoto huwa hafifu na umwagikaji wa damu huwa kawaida kama hedhi.

Je kama sitakuwa na umwagikaji wa damu baada ya kumeza misoprostol?

Tafuta msaada wa kiafya ikiwa hauna umwagikaji wa damu au una umwagikaji mdogo wa damu unaofuatwa na maumivu makali (hasa katika bega la kulia) ambayo hayapunguzwi na ibuprofen . Hii inaweza kuwa dalili ya uja uzito ulio nje ya tumbo la uzazi, na inaweza kuwa tishio la maisha. Unaweza pia kuwafikia marafiki zetu katika www.safe2choose.org ili kuongea na mshauri wa uaviaji mimba aliye na mafunzo ikiwa unahisi kuwa uaviaji mimba haukufanikiwa.

Je kama natokwa na damu nyingi baada ya kumeza dawa ya kuavya mimba?

Tafuta msaada wa kiafya ikiwa unalowa baada ya kutumia visodo viwili baada ya saa 2 mfululizo baada ya kufikiri uja uzito ushatoka. Kulowa kunamaanisha kuwa kisodo kimejaa damu mbele – hadi – nyuma, upande- hadi – upande na kupita- hadi – kupita.

Naweza kufanya nini kukabili maumivu yoyote baada ya kumeza tembe ya kuavya mimba?

Meza tembe 3-4 (200 mg) baada ya kila saa 6-8 ili kusaidia kuondoa maumivu yako. Kumbuka kuwa unaweza kumeza ibuprofen kabla ya kutumia misoprostol, pia

Naweza kula kama kawaida baada ya kumeza tembe ya kuavya mimba?

Baada ya misoprostol kuyeyuka, unaweza kula unavyotaka. Vyakula vilivyokauka (kama vile vilivyookwa au kuchomwa) vinaweza kusaidia kichefuchefu, ilhali mboga, mayai na nyama nyekundu inaweza kurejesha madini yaliyopotea wakati wa kuavya mimba.

Naweza kunywa vinywaji baada ya kumeza tembe ya kuavya mimba?

Baada ya misoprostol kuyeyuka, unaweza kunywa kinywaji unachokipenda (isipokuwa pombe).

Naweza kunywa pombe ninapomeza tembe na baada ya kumeza dawa ya kuavya mimba?

Pombe inastahili kuepukwa wakati wa matibabu ili kuzuia kuathiri ufanisi wa matibabu. Pombe inaweza kusababisha ongezeko la umwagikaji wa damu kutoka kwa tumbo la uzazi katika hali zingine na kupunguza ufanisi wa dawa zingine zinazomezwa kupunguza maumivu au ambukizo (kwa wanawake wanaokabili matatizo). Kwa jumla, inapendekezwa kuepuka pombe hadi uthibitishe kuwa uaviaji mimba umekamilika na unahisi ukiwa na afya nzuri.

Inachukua muda upi kwa madhara ya tembe za kuavya mimba kuisha?

Wanawake wengi watapitisha uja uzito baada ya saa 4-5 na kuhisi vyema chini ya saa 24. Ni kawaida kuendelea kuona umwagikaji mdogo wa damu na madoadoa hadi hedhi yako inayofuata takriban wiki 3-4.

Ni kawaida kuhisi kuwa mgonjwa au kichefuchefu baada ya kumeza misoprostol?

Ni kawaida kuhisi kuwa mgonjwa kwa tumbo lako, kuhara, kibaridi, au hata kuhisi una joto katika kipindi hiki. Wanawake wengi wanaripoti kuwa wanajua kuwa wamepitisha mimba kwa sababu umwagikaji wa damu unapungua, na wanaanza kuhisi vyema zaidi.

Nitafanya nini kama bado niko mja mzito baada ya kumeza tembe ya kuavya mimba?

Baadhi ya wanawake wanaweza wakahitaji utaratibu wa upasuaji ikiwa bado wana uja uzito baada ya kumeza tembe. Kumbuka! Matibabu ya uaviaji mimba yasiyokamilika yanapatikana kwa urahisi popote duniani. Una haki kupata huduma hii, hata kama uaviaji mimba umebanwa kisheria katika nchi yako.

Kwa baadhi ya wanawake, msokoto huwa mkali- zaidi ya msokoto wa hedhi (ikiwa una msokoto wa hedhi) na umwagikaji damu huwa zaidi ya ule wa hedhi. Unaweza kupitisha donge la damu hadi kiasi cha limau katika saa za kwanza baada ya kumeza misoprostol. Kwa wanawake wengine, msokoto huwa hafifu na umwagikaji wa damu huwa kawaida kama hedhi.

Tafuta msaada wa kiafya ikiwa hauna umwagikaji wa damu au una umwagikaji mdogo wa damu unaofuatwa na maumivu makali (hasa katika bega la kulia) ambayo hayapunguzwi na ibuprofen . Hii inaweza kuwa dalili ya uja uzito ulio nje ya tumbo la uzazi, na inaweza kuwa tishio la maisha. Unaweza pia kuwafikia marafiki zetu katika www.safe2choose.org ili kuongea na mshauri wa uaviaji mimba aliye na mafunzo ikiwa unahisi kuwa uaviaji mimba haukufanikiwa.

Tafuta msaada wa kiafya ikiwa unalowa baada ya kutumia visodo viwili baada ya saa 2 mfululizo baada ya kufikiri uja uzito ushatoka. Kulowa kunamaanisha kuwa kisodo kimejaa damu mbele – hadi – nyuma, upande- hadi – upande na kupita- hadi – kupita.

Meza tembe 3-4 (200 mg) baada ya kila saa 6-8 ili kusaidia kuondoa maumivu yako. Kumbuka kuwa unaweza kumeza ibuprofen kabla ya kutumia misoprostol, pia

Baada ya misoprostol kuyeyuka, unaweza kula unavyotaka. Vyakula vilivyokauka (kama vile vilivyookwa au kuchomwa) vinaweza kusaidia kichefuchefu, ilhali mboga, mayai na nyama nyekundu inaweza kurejesha madini yaliyopotea wakati wa kuavya mimba.

Baada ya misoprostol kuyeyuka, unaweza kunywa kinywaji unachokipenda (isipokuwa pombe).

Pombe inastahili kuepukwa wakati wa matibabu ili kuzuia kuathiri ufanisi wa matibabu. Pombe inaweza kusababisha ongezeko la umwagikaji wa damu kutoka kwa tumbo la uzazi katika hali zingine na kupunguza ufanisi wa dawa zingine zinazomezwa kupunguza maumivu au ambukizo (kwa wanawake wanaokabili matatizo). Kwa jumla, inapendekezwa kuepuka pombe hadi uthibitishe kuwa uaviaji mimba umekamilika na unahisi ukiwa na afya nzuri.

Wanawake wengi watapitisha uja uzito baada ya saa 4-5 na kuhisi vyema chini ya saa 24. Ni kawaida kuendelea kuona umwagikaji mdogo wa damu na madoadoa hadi hedhi yako inayofuata takriban wiki 3-4.

Ni kawaida kuhisi kuwa mgonjwa kwa tumbo lako, kuhara, kibaridi, au hata kuhisi una joto katika kipindi hiki. Wanawake wengi wanaripoti kuwa wanajua kuwa wamepitisha mimba kwa sababu umwagikaji wa damu unapungua, na wanaanza kuhisi vyema zaidi.

Baadhi ya wanawake wanaweza wakahitaji utaratibu wa upasuaji ikiwa bado wana uja uzito baada ya kumeza tembe. Kumbuka! Matibabu ya uaviaji mimba yasiyokamilika yanapatikana kwa urahisi popote duniani. Una haki kupata huduma hii, hata kama uaviaji mimba umebanwa kisheria katika nchi yako.

Marejeo

Tovuti hii inaweza kuhitaji kuki zisizojulikana na huduma anuwai za mtu mwingine ili iweze kufanya kazi kunavyotakikana. Unaweza kusoma Sheria na Masharti yetu na Sera za Faragha . Ukitaka kuendelea kutumia tovuti hii, ni sharti utupe idhini ili uweze kufanya hivyo.