Aina ya Tembe za Kuavya Mimba na Matumizi Yake

Tembe za kuavya mimba hufanya kazi vipi?

Kuna aina mbili ya tembe za kuavya mimba, na kila moja ina mbinu tofauti ya utenda kazi. Mifepristone huzuia homoni zinazohitajika kwa ukuaji wa uja uzito, ilhali virutubishi vinavyotumika katika misoprostol hufanya kazi kwa kulegeza na kufungua mlango wa tumbo la uzazi (mwanya katika tumbo la uzazi) na kusababisha tumbo la uzazi kujikaza, na hivyo kusukuma uja uzito nje.

Misoprostol hufanya nini?

Misoprostol husababisha tumbo la uzazi kujikaza na hivyo kutoa uja uzito.

Mifepristone hufanya nini?

Mifepristone huzuia homoni zinazohitajika kwa ukuaji wa mimba

Naweza kutumia misoprostol nyumbani?

Ndio, unaweza kutumia misoprostol salama ukiwa nyumbani. Unapotumia tembe za misoprostol, jaribu kuhakikisha kuwa uko katika sehemu (kama kwako nyumbani) ambapo una ufaragha na unaweza kulala chini kwa saa chache baada ya kumeza tembe. Kuwa na mtu karibu nawe anayeweza kukuangalia na kukuletea chai moto au kitu cha kula inaweza kusaidia sana.

Naweza kunywa maji baada ya kumeza misoprostol?

Usinywe au kula kitu chochote kwa dakika 30 unaporuhusu misoprostol kuyeyuka. Baada ya dakika 30 kupita, unaweza kunywa maji ili kumeza mabaki ya tembe, na kwa jumla kiasi cha maji unachostahili ili kuhisi mwili una maji ya kutosha.

Naweza kunywa maji baada ya kumeza mifepristone?

Ndio, unaweza kunywa maji kukusaidia kumeza mifepristone.

Nastahili kutumia misoprostol kupitia kuweka chini ya ulimi au kupitia uke?

Kuna njia mbili za kutumia misoprostol: kuweka tembe katika uke wako au chini ya ulimi wako. Jinsi ya kutumia inapendekeza kuwa utumie tu misoprostol chini ya ulimi wako kwa sababu ni faragha zaidi (tembe huyeyuka haraka na haziachi alama zinazoonekana katika mwili wako) na huwa na hatari ndogo la ambukizo.

Kuna tofauti gani kati ya kumeza misoprostol pekee na kumeza mifepristone na misoprostol kwa pamoja?

Mchanganyiko wote wa jumla ya mifepristone na misoprostol na misoprostol- ndio tu maamuzi yenye ufanisi. Hata hivyo, ikiwa inapatikana na unaweza kumudu gharama, mchanganyiko wa mifepristone na misoprostol unastahili kuwa uamuzi wako unaopendelewa.

Misoprostol huwa na ufanisi upi na pia misoprostol + mifepristone huwa na ufanisi upi?

Wanawake 98 kati ya 100 huwa na uaviaji mimba kamili ikiwa mifepristone na misoprostol zimetumika kwa pamoja. Takriban wanawake 95 kati ya 100 watakuwa na uaviaji mimba kamili ikiwa tu misoprostol inatumika.

Mbona nahitaji kumeza misoprostol zaidi ikiwa nitameza mifepristone kwanza?

Mifepristone na misoprostol hutumika pamoja kwa sababu tembe hizi hukamilishana. Dawa inayotumika katika misoprostol hufanya kazi kwa kulegeza na kufungua mlango wa uzazi (kufungua tumbo la uzazi) na kusababisha tumbo la uzazi kujikaza, hivyo kusukuma nje uja uzito.

Mtu yeyote anaweza kujua kuwa niliavya mimba kwa kutumia tembe ya kuavya mimba?

Ikiwa utatumia tembe za misoprostol chini ya ulimi wako, hakuna mtu anaweza kujua kuwa ulitumia tembe za kuavya mimba kwa sababu utameza kila kitu baada ya dakika 30. Ikiwa mtu atauliza, unaweza kusema ulipoteza mimba kwa njia ya kawaida. Ikiwa utatumia misoprostol kupitia uke, koti ya tembe huenda isiyeyuke kabisa kwa siku moja au mbili. Ikiwa unahitaji kutafuta usaidizi wa kiafya wa dharura kati ya saa 48 kwa sababu ulitumia misoprostol kupitia uke, mhudumu wa afya anaweza kuona koti nyeupe za tembe katika uke wako. Hii ndio maana jinsi ya kutumia hupendekeza kutumia misoprostol chini ya ulimi wako na si ndani ya uke wako.

Kuna aina mbili ya tembe za kuavya mimba, na kila moja ina mbinu tofauti ya utenda kazi. Mifepristone huzuia homoni zinazohitajika kwa ukuaji wa uja uzito, ilhali virutubishi vinavyotumika katika misoprostol hufanya kazi kwa kulegeza na kufungua mlango wa tumbo la uzazi (mwanya katika tumbo la uzazi) na kusababisha tumbo la uzazi kujikaza, na hivyo kusukuma uja uzito nje.

Misoprostol husababisha tumbo la uzazi kujikaza na hivyo kutoa uja uzito.

Mifepristone huzuia homoni zinazohitajika kwa ukuaji wa mimba

Ndio, unaweza kutumia misoprostol salama ukiwa nyumbani. Unapotumia tembe za misoprostol, jaribu kuhakikisha kuwa uko katika sehemu (kama kwako nyumbani) ambapo una ufaragha na unaweza kulala chini kwa saa chache baada ya kumeza tembe. Kuwa na mtu karibu nawe anayeweza kukuangalia na kukuletea chai moto au kitu cha kula inaweza kusaidia sana.

Usinywe au kula kitu chochote kwa dakika 30 unaporuhusu misoprostol kuyeyuka. Baada ya dakika 30 kupita, unaweza kunywa maji ili kumeza mabaki ya tembe, na kwa jumla kiasi cha maji unachostahili ili kuhisi mwili una maji ya kutosha.

Ndio, unaweza kunywa maji kukusaidia kumeza mifepristone.

Kuna njia mbili za kutumia misoprostol: kuweka tembe katika uke wako au chini ya ulimi wako. Jinsi ya kutumia inapendekeza kuwa utumie tu misoprostol chini ya ulimi wako kwa sababu ni faragha zaidi (tembe huyeyuka haraka na haziachi alama zinazoonekana katika mwili wako) na huwa na hatari ndogo la ambukizo.

Mchanganyiko wote wa jumla ya mifepristone na misoprostol na misoprostol- ndio tu maamuzi yenye ufanisi. Hata hivyo, ikiwa inapatikana na unaweza kumudu gharama, mchanganyiko wa mifepristone na misoprostol unastahili kuwa uamuzi wako unaopendelewa.

Wanawake 98 kati ya 100 huwa na uaviaji mimba kamili ikiwa mifepristone na misoprostol zimetumika kwa pamoja. Takriban wanawake 95 kati ya 100 watakuwa na uaviaji mimba kamili ikiwa tu misoprostol inatumika.

Mifepristone na misoprostol hutumika pamoja kwa sababu tembe hizi hukamilishana. Dawa inayotumika katika misoprostol hufanya kazi kwa kulegeza na kufungua mlango wa uzazi (kufungua tumbo la uzazi) na kusababisha tumbo la uzazi kujikaza, hivyo kusukuma nje uja uzito.

Ikiwa utatumia tembe za misoprostol chini ya ulimi wako, hakuna mtu anaweza kujua kuwa ulitumia tembe za kuavya mimba kwa sababu utameza kila kitu baada ya dakika 30. Ikiwa mtu atauliza, unaweza kusema ulipoteza mimba kwa njia ya kawaida. Ikiwa utatumia misoprostol kupitia uke, koti ya tembe huenda isiyeyuke kabisa kwa siku moja au mbili. Ikiwa unahitaji kutafuta usaidizi wa kiafya wa dharura kati ya saa 48 kwa sababu ulitumia misoprostol kupitia uke, mhudumu wa afya anaweza kuona koti nyeupe za tembe katika uke wako. Hii ndio maana jinsi ya kutumia hupendekeza kutumia misoprostol chini ya ulimi wako na si ndani ya uke wako.

Marejeo

Tovuti hii inaweza kuhitaji kuki zisizojulikana na huduma anuwai za mtu mwingine ili iweze kufanya kazi kunavyotakikana. Unaweza kusoma Sheria na Masharti yetu na Sera za Faragha . Ukitaka kuendelea kutumia tovuti hii, ni sharti utupe idhini ili uweze kufanya hivyo.