Jinsi ya Kutumia Vidonge vya Kutoa Mimba

Kuna aina mbili za dawa zinazotumika kutoa mimba: mifepristone na misoprostol. Utoaji mimba kwa kutumia vidonge hufanya kazi vizuri zaidi ikiwa dawa zote mbili zitatumika kwa pamoja. Hata hivyo, ikiwa mifepristone haipatikani, waweza kutumia misoprostol pekee na bado ukafanikiwa kutoa mimba kwa usalama.

Ili kutumia vidonge vya kutoa mimba kwa usalama, tumia kidonge 1 cha mifepristone (200 mg), subiri saa 24–48, kisha weka vidonge 4 vya misoprostol (200 mcg kila kimoja) chini ya ulimi. Ikiwa ni lazima, rudia dozi ya misoprostol. Ikiwa mifepristone haipatikani, tumia vidonge 12 vya misoprostol katika dozi 3. Hakikisha kuwa ujauzito wako ni chini ya wiki 13 na fuata maelekezo ya usalama.

Soma zaidi ikiwa ungependa kujifunza jinsi ya kutumia vidonge vya kutoa mimba, mifepristone na misoprostol.

Mifepristone na Misoprostol
Misoprostol Pekee
How to Use

Kabla ya kuanza, soma makala yetu: Kabla ya Kutumia Vidonge, pia kabla hujatumia vidonge hakikisha:

Nitatumiaje mifepristone na misoprostol kwa kutoa mimba?

Ili kutoa mimba kwa kutumia mifepristone na misoprostol, unatakiwa kumeza kidonge kimoja cha mifepristone chenye mg 200 na angalau vidonge vinne vya misoprostol zenye mcg 200 (jumla ya mcg 800).

Ni vyema kutumia jumla ya vidonge nane vya misoprostol. Huenda ukahitaji kuzitumia zote ili kuhakikisha utoaji mimba umekamilika, hasa ikiwa ujauzito wako ni wa kati ya wiki 9–13. Hata hivyo, ikiwa una vidonge vinne tu vya misoprostol, bado vinaweza kufanya kazi.

Dawa za kupunguza maumivu (kama vile ibuprofen) na dawa za kupunguza kichefuchefu zinaweza kusaidia wakati wa utoaji mimba. Ikiwa unahisi kichefuchefu kikali, tunapendekeza utumie dawa ya kuzuia kichefuchefu dakika 30 kabla ya kumeza mifepristone au misoprostol ili kuzuia kutapika.

Si lazima kuacha kula chakula pindi unapotoa mimba kwa kutumia vidonge. Unaweza kula na kunywa kama kawaida, isipokuwa pale ambapo vidonge vinapaswa kuwa chini ya ulimi wako.

Hivi ndivyo mifepristone na misoprostol zinavyotumika kwa pamoja ili kutoa mimba:

Hatua ya 1: Nitakaje kutumia mifepristone?

Meza kidonge kimoja cha mifepristone cha mg 200 kwa kutumia maji.

Ikiwa utatapika ndani ya saa moja baada ya kumeza mifepristone, huenda haitafanya kazi, na utatakiwa kutumia kidonge kingine.
Ikiwa utatapika baada ya saa moja, huna haja ya kuwa na wasiwasi.

Hatua ya 2: Ninapaswa kusubiri kwa muda gani baada ya kutumia mifepristone?

Subiri saa 24–48

Kwa kawaida mifepristone huwa haina maudhi, kwahiyo unaweza kuendelea na shughuli zako za kawaida. Mara chache, baadhi ya watu hutokwa na damu kabla ya kutumia misoprostol. Ikiwa hili litatokea, ni sawa, endelea kama kawaida.

Unaweza kuendelea na hatua inayofuata wakati wowote baada ya saa 24 hadi 48, kwahiyo unaweza kuchagua wakati unaofaa zaidi kwako kuanza. Mara tu unapoanza kutumia misoprostol, hakikisha uko mahali unapohisi ni salama na huru kwa angalau saa 12, lakini saa 24 ni bora zaidi. Ikiwezekana, tunapendekeza uanze kutumia misoprostol asubuhi. Hii itakuruhusu kufuatilia mwitikio wa mwili wako mchana kutwa, pia itahakikisha kuwa unapata muda wa kutosha kupumzika wakati wa usiku.

Hatua ya 3: Tumia dawa za maumivu

Anza kwa kutumia dawa ya kupunguza maumivu kama ibuprofen (mg 800) takriban dakika 30 kabla ya kutumia misoprostol kwa sababu maumivu ya tumbo yataanza mara tu baada ya kutumia vidonge. Ikiwa una dawa ya kupunguza kichefuchefu, tumia pamoja na dawa ya kupunguza maumivu.

Kisha, weka vidonge vinne vya misoprostol (mcg 200 kila kimoja) chini ya ulimi wako na vishikilie hapo kwa dakika 30. Unaweza kumeza mate yako, lakini usiongee au kula kwa muda wa dakika 30; kwa hiyo, ni bora kuvitumia mahali tulivu ambapo hutavurugwa. Baada ya dakika 30, kunywa maji na kumeza chembechembe za vidonge zilizobaki.

Ikiwa utatapika ndani ya dakika 30 baada ya kutumia misoprostol, rudia Hatua ya 3. Ikiwa utatapika baada ya muda huo, hakuna haja ya kurudia chochote kwa sababu dawa itakuwa imeshaingia mwilini.

Maumivu ya tumbo na kutokwa na damu vinaweza kuanza dakika 30 baada ya kutumia misoprostol, wakati mwingine inaweza kuchukua hadi saa 24 kuanza. Watu wengi huanza kutokwa na damu ndani ya saa nne hadi sita baada ya kutumia.

Unaweza kuendelea kutumia vidonge vitatu hadi vinne vya ibuprofen (mg 200 kila kimoja) kila baada ya saa sita hadi nane ili kudhibiti maumivu, ikiwa inahitajika. Usizidi mg 3200 ndani ya saa 24, na usitumie aspirin ya kawaida kwani inazidisha hatari ya kutokwa na damu. Acetaminophen au paracetamol (mg 1000) pia inaweza
kutumika ikiwa una mzio na NSAIDs, lakini inaweza isifanye kazi vizuri kama ibuprofen.

Hatua ya 4: Ni lini ninahitaji dozi ya pili ya misoprostol?

Ikiwa una ujauzito wa chini ya wiki tisa, huenda usihitaji dozi ya pili. Lakini ikiwa hujatokwa damu nyingi kama ya hedhi ndani ya saa 24, au ikiwa unahisi damu inayotoka ni kidogo sana, unaweza kutumia vidonge vinne zaidi vya misoprostol kwa njia ile ile kama mwanzo.

Ikiwa una ujauzito wa wiki 9–13, ni vyema kutumia vidonge vinne zaidi vya misoprostol kwa njia ile ile uliyotumia dozi ya kwanza, saa nne baada ya dozi ya kwanza. Hii hufanya vidonge kufanya kazi vizuri zaidi na kuongeza uwezekano wa kufanikisha utoaji mimba.

Ni nini kingine ninachopaswa kujua ninapotumia mifepristone na misoprostol? mifepristone na misoprostol:

Matatizo ni nadra, hata hivyo, ni muhimu kuyatambua. Jifunze zaidi kuhusu dalili na ishara za tahadhari baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba.

Iwapo umetumia vidonge vya kutoa mimba, mifepristone na misoprostol, huenda usihitaji kumtembelea mtoa huduma wa afya kwa ajili ya ufuatiliaji. Ikiwa una wasiwasi kuhusu mchakato wa utoaji mimba na ungependa msaada wa ziada, unaweza kuwasiliana na marafiki zetu kupitia safe2choose.org, womenhelp.org, au womenonweb.org.

Maagizo Kuhusu Utoaji Mimba Kwa Kutumia Misoprostol Pekee

Kabla ya kuanza, soma makala yetu: Kabla ya Kutumia Vidonge, pia kabla hujatumia vidonge hakikisha:

Ikiwa mifepristone haipatikani mahali ulipo, waweza kutumia misoprostol pekee kutoa mimba.

Ili kutoa mimba kwa kutumia misoprostol pekee, utahitaji kutumia vidonge 12 vya misoprostol vyenye mcg 200 kwa kila kimoja.

Kutumia vidonge 12 vya misoprostol kunaweza kusaidia kufanikisha utoaji wa mimba, hasa ikiwa ujauzito wako uko kati ya wiki 9–13. Ikiwa ujauzito wako uko chini ya wiki tisa na huna vidonge 12 vya misoprostol, unaweza kutumia vidonge nane, lakini kiwango cha ufanisi kitapungua.

Maumivu (ibuprofen) na dawa za kupunguza kichefuchefu pia zinaweza kusaidia wakati wa utoaji mimba. Ikiwa unasumbuliwa na kichefuchefu, tunapendekeza utumie dawa za kupunguza kichefuchefu dakika 30 kabla ya kutumia misoprostol ili kuepuka kutapika.

Si lazima kuacha kula wakati wa utoaji mimba kwa kutumia vidonge. Unaweza kula na kunywa kama kawaida, isipokuwa wakati vidonge viko chini ya ulimi wako.

Hivi ndivyo misoprostol pekee inavyotumika kutoa mimba:

Hatua ya 1: Nitakaje kuchukua dozi ya kwanza ya misoprostol?

Anza kwa kutumia dawa ya kupunguza maumivu kama ibuprofen (mg 800) takriban dakika 30 kabla ya kutumia misoprostol kwa sababu maumivu ya tumbo yataanza mara tu baada ya kutumia vidonge. Ikiwa una dawa ya kupunguza kichefuchefu, itumie pia.

Kisha, weka vidonge vinne vya misoprostol (mcg 200 kila kimoja) chini ya ulimi wako na vishikilie hapo kwa dakika 30. Unaweza kumeza mate yako, lakini usiongee au kula kwa muda wa dakika 30; kwa hiyo, ni bora kuvitumia mahali tulivu ambapo hutavurugwa. Baada ya dakika 30, kunywa maji na kumeza chembechembe za vidonge zilizobaki.

Ikiwa utatapika ndani ya dakika 30 baada ya kutumia misoprostol, rudia Hatua ya 1. Ikiwa utatapika baada ya muda huo, hakuna haja ya kurudia chochote kwa sababu dawa itakuwa imeshaingia mwilini.

Maumivu ya tumbo na kutokwa na damu vinaweza kuanza dakika 30 baada ya kutumia misoprostol, wakati mwingine inaweza kuchukua hadi saa 24 kuanza. Watu wengi huanza kutokwa na damu ndani ya saa nne hadi sita baada ya kutumia misoprostol.

Unaweza kuendelea kutumia vidonge vitatu hadi vinne vya ibuprofen (mg 200 kila kimoja) kila baada ya saa sita hadi nane ili kudhibiti maumivu, ikiwa inahitajika. Usizidi mg 3200 ndani ya saa 24, na usitumie aspirin ya kawaida kwani inazidisha hatari ya kutokwa na damu. Acetaminophen au paracetamol (mg 1000) pia inaweza kutumika ikiwa una mzio na NSAIDs, lakini inaweza isifanye kazi vizuri kama ibuprofen.

Hatua ya 2: Ninapaswa kusubiri kwa muda gani kati ya dozi za misoprostol?

Subiri kwa saa tatu

Hatua ya 3: Nitakaje kuchukua dozi ya pili ya misoprostol?

Weka vidonge vingine vinne vya misoprostol (mcg 200 kila kimoja) chini ya ulimi wako na viache kwa dakika 30.”

Hatua ya 4:

Subiri kwa saa tatu nyingine.

Hatua ya 5: Nitakaje kuchukua dozi ya tatu ya misoprostol?

Weka vidonge vingine vinne vya misoprostol (mcg 200 kila kimoja) chini ya ulimi na viache kwa dakika 30.

Nitegemee nini baada ya kuchukua dozi zote za misoprostol?

Unapaswa kuanza kutokwa na damu na maumivu ya tumbo wakati unapotumia vidonge. Hakikisha umetumia vidonge vyote 12, hata kama utaanza kutokwa na damu kabla ya kumaliza vidonge vyote.

Ni nini kingine ninachopaswa kujua ninapotumia misoprostol?

Matatizo ni nadra, hata hivyo, ni muhimu kuyatambua. Jifunze zaidi kuhusu dalili na ishara za tahadhari baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba.

Iwapo umetumia vidonge vya kutoa mimba, mifepristone na misoprostol, huenda usihitaji kumtembelea mtoa huduma wa afya kwa ajili ya ufuatiliaji. Ikiwa una wasiwasi kuhusu mchakato wa utoaji mimba na ungependa msaada wa ziada, unaweza kuwasiliana na marafiki zetu kupitia safe2choose.org, womenhelp.org, au womenonweb.org.

Waandishi:

Yote yaliyomo kwenye wavuti hii yameandikwa na timu ya HowToUseAbortionPill.org kwa kufuata viwango na itifaki kutoka Shirikisho la Kitaifa la Utoaji Mimba, Ipas, Shirika la Afya Ulimwenguni, DKT Kimataifa na carafem.

Marejeo: