Kozi za utoaji mimba mtandaoni kwa wafamasia

 • 1.1 Utoaji Mimba – Mtazamo wa Kimataifa
 • 1.2 Utoaji mimba salama – Ufafanuzi na Njia
 • 1.3 Njia na Mbinu Zilizoidhinishwa kwa Utoaji Mimba Salama
 • 1.4 Wajibu wa Wafamasia katika Utoaji Mimba wa Kitabibu ulio Salama
 • 2.1 Utoaji Mimba wa Kitabibu ulio Salama – Mambo ya Msingi
 • 2.2 Mwendeleo wa usalama katika Utoaji Mimba wa Kitabibu
 • 3.1 Umuhimu wa Kuchunguza
 • 3.2 Malengo ya Kuwachunguza Wateja
 • 4.1 Mambo ya Kuzingatia
 • 4.2 Jinsi ya Kutumia Vidonge vya Utoaji Mimba: Mifepristone + Misoprostol
 • 4.3 Jinsi ya Kutumia Vidonge vya Utoaji Mimba: Misoprostol Pekee
 • 5.1 Kuzikabili Athari Zinazotarajiwa
 • 5.2 Kuzikabili Athari za Mara kwa Mara
 • 6.1 Muda wa Utoaji Mimba
 • 6.2 Ishara za Hatari na Jinsi ya Kizikabili
 • 6.3 Wateja Wanaorudi – Visa vya Mara kwa Mara na Jinsi ya Kuvikabili
Somo la 1: Maelezo ya Jumla Kuhusu Utoaji Mimba

In this lesson, we will review abortion within a global context, define the various types of safe abortion, and explore the expanding role of pharmacists within safe abortion work. Upon completing this lesson successfully, you will be able to cite global rates of abortion and differentiate between safe and unsafe methods of abortion.

Utoaji mimba unafafanuliwa kama kuondoa matokeo ya mimba kutoka kwenye mfuko wa uzazi kabla ya ukuaji wa kijusi. Kutoa mimba kunaweza kutokia kwenyewe kwa sababu ya matatizo wakati wa mimba, au kunaweza kusababishwa. Dhana kutoa mimba mara nyingi hurejelea kutoa mimba ya mwanadamu kimakusudi, bali mimba kutoka yenyewe huitwa kuharibika mimba.

1.1) Utoaji Mimba – Mtazamo wa Kimataifa

Taasisi ya Guttmacher inakadiria kwamba kati ya mwaka 2010-2014, takribani mimba milioni 56 zilitolewa kwa kukusudia duniani kote. Hii ni sawa na kutamatisha asilimia 25% ya mimba zote kwa huo muda.1

Yamkini, utoaji mimba wa hiari ni utaratibu wa kawaida ulimwenguni kote. Wanawake wengi hutoa mimba kwa sababu wanashika mimba bila kutarajia. Japo wengi wa hawa wanawake wanakosa njia za uzazi wa mpango, ni muhimu kukumbuka kwamba njia zote za uzazi wa mpango zinaweza kukosa kufaulu wakati fulani, na kwamba wanawake wanaweza kuendea utoaji mimba hata wakati wanaendelea kutumia njia za mpango wa uzazi.

Wakati wahudumu waliofuzu wanapopeana huduma ya kutoa mimba kwa kutumia vyombo na dawa zinazofaa, kwa njia na dozi sahihi, na katika mazingira safi na katika hatua za mapema za mimba, kutoa mimba ni mojawapo wa mbinu za kitabibu salama zaidi. Kwa hakika, kutoa mimba huwa na hatari kidogo kukilinganishwa na mimba inayochukua muhula wake mzima. 2

Hata hivyo, utoaji mimba ambao haujazingatia viwango vilivyotajwa hapo juu unaweza kusababisha matatizo yanayoweza kusababisha kifo. Utoaji mimba usio salama ni chanzo kikuu cha idadi ya juu ya vifo vya wakina mama katika nchi zinazoendelea. Utafiti wa hivi karibuni unakadiria kuwa kati ya asilimia 8-18% ya vifo vya wakina mama duniani kote vinatokana na utoaji mimba usio salama. Idadi ya vifo vinavyotokana na Utoaji mimba mwaka 2014 ilikuwa kati ya 22,500 na 44,000. 3 4 5

1Sedgh G et al., Abortion incidence between 1990 and 2014- global, regional, and subregion-al levels and trends, The Lancet, 2016.

2Raymond, Elizabeth G.; Grimes, David A. The Comparative Safety of Legal Induced Abortion and Childbirth in the United States. Obstetrics & Gynecology. 119(2, Part 1) 215-219, February 2012.

3Singh S, Darroch JE and Ashford LS, Adding It Up- The Costs and Benefits of Investing in Sexual and Reproductive Health 2014, New York- Guttmacher Institute, 2014.

1.2) Utoaji Mimba Salama – ufafanuzi na njia

Utoaji mimba salama ni mchakato wa kitabibu unaofanywa na mtu mwenye mafunzo ambao hupunguzia mwanamke hatari ya maradhi na kifo. Hivyo, ni muhimu kwamba hatua za utoaji mimba zinazingatia mahitaji mahsusi ya usalama.

Kinyume na utoaji mimba salama, Shirika la Afya Duniani linafafanua utoaji mimba usio salama kama utaratibu wa kutoa mimba isiyokusudiwa unaoendeshwa ama na mtu asiyekuwa na ujuzi mzuri na/au katika mazingira yasiyoafiki viwango vya kimsing vya kiafya.

Matokeo ya kiafya ya utoaji mimba usio salama hutegemea vituo ambapo utoaji umefanyika; ujuzi wa anayetoa huduma ya utoaji; njia iliyotumiwa Kutoa mimba; afya ya mama; na ukubwa wa mimba. Njia za Utoaji mimba zisizo salama zinahuzisha lolote katika mambo yafuatayo -

 • kuingiza chombo au kitu kwenye mfuko wa uzazi, kama vile mizizi, vifaa vya chuma, au dawa za kienyeji za mitishamba;
 • upanuzi na upasuaji wa mfuko wa uzazi uliofanywa na mhudumu asiye na ujuzi;
 • kumeza vitu vinayodhuru afya;
 • au matumizi ya nguvu za nje.

Yote haya yanaweza kusabababisha matatizo ya kiafya, na katika hali nyingi huwa hatari katika maisha.6Safe Abortion - Technical and Policy Guidance for Health Systems, Second edition page 18 (World Health Organization 2012).

1.3) Njia na Mbinu Zilizoidhinishwa kwa Utoaji Mimba Salama

Shirika la Afya Duniani, kulingana na uchunguzi wa ushahidi, limependekeza mbinu zifuatazo kama salama kwa kutolea mimba -

 • Pampu ya Kuvuta (Vacuum Aspiration) (ya mkono au ya umeme) - Hii ni njia ya upasuaji ambapo matokeo ya mimba yanatolewa kwa kuvuta kwa kutumia mrija wa plastiki uliongizwa kwenye mfuko wa uzazi. Utupu uliotengezwa ama kwa kutumia pampu ya mkono au ya umeme unatumika kufanikisha uvutaji huu. Kwa kuwa chombo kilichotumika si cha chuma, na kiwango cha utupu kilichotumika ni kidogo, njia hii ni salama na hupunguza hatari ya madhara katika viungo inapotumika kwa njia sahihi. Njia hii kwa kawaida hutumika kutoa mimba za hadi wiki 12-14.
 • Utoaji Mimba wa Kitabibu (MA) - Katika njia hii, mseto wa dawa mbili au matumizi ya mara kwa mara ya dozi za dawa moja hupeanwa kutoa mimba. Hii ni mbinu isiyo ya upasuaji, isiyo ya upenyezi ya kutoa mimba. Dawa mbili zinazotumika mara kwa mara ni Misoprostol ama yenyewe au pamoja na Mifepristone. Kutokana na uchunguzi wa utafiti wa kitabibu, Shirika la Afya Duniani pamoja na mashirika mengine ya kimataifa wamegundua mpangilio mzuri zaidi na utaratibu wa kutumia hizi dawa kwa utoaji mimba salama. Dozi ya dawa zinazotumika zitatofautiana kulingana na muda wa mimba ili kutoa matokeo mazuri zaidi na kupunguza madhara kwa mama. Mbinu hii inaweza kutumika muda wote wa mimba, kwa kubadilisha dozi na wakati wa dawa zitumikazo ili kufaulu kutoa mimba.
 • Upanuaji na Kuondoa (Dilation and Evacuation) - Kwa mimba iliyozidi wiki 14, Shirika la Afya Duniani linapendekeza mbinu inayoitwa Upanuaji na Kuondoa, ambapo dawa au vipanuzi vya chuma hutumika kufungua mlango wa kizazi na kijusi kutolewa kutumia mkasi. Hii ni mbinu ya upasuaji ya hali ya juu na ngumu na inapaswa kufanywa na wahudumu wa afya waliofunzwa na mahiri katika mazingira mazuri.

Ni muhimu kukumbuka kwamba Upanuaji na Upasuaji (inayoitwa kwa kawaida kama “D&C” au “curettage”) haichukuliwi kuwa mbinu salama kutokana na uchunguzi wa ushahidi, na kwa hivyo Shirika la Afya Duniani halipendekezi mbinu hii kama mbinu salama ya kutoa mimba.

1.4) Wajibu wa Wafamasia katika Utoaji Mimba wa Kitabibu ulio Salama

Wafamasia na wafanyakazi katika maduka ya kuuza dawa ni kundi muhimu la washirika wa wahudumu wa afya ambao wanaweza kichukua nafasi muhimu katika kuongeza upatikanaji wa utoaji mimba wa kitabibu ulio salama. Utafiti wa sasa kutoka nchi kadhaa unaonyesha kuwa wanawake huendea ushauri wa wafamasia wanapotaka kutoa mimba zisizotakikana, bila kujali msimamo wa kisheria nchini mwao. Hii ni fursa nzuri kwa Wafamasia na wafanyakazi katika maduka ya kuuza dawa kuwa mstari wa mbele katika kuongeza upatikanaji wa huduma za Utoaji mimba ulio salama, hususani Utoaji mimba wa kitabibu ulio salama katika miezi 3 ya kwanza ya mimba.

Shirika la Afya Duniani linawatambua wazi Wafamasia na wafanyakazi katika maduka ya kuuza dawa kama kundi maalumu la wahudumu wa afya ambao wana wajibu katika kupanua upatikanaji wa huduma za utoaji mimba ulio salama. Shirika la Afya Duniani limependekeza, katika mazingira ya utafiti mpevu, shughuli zifuatazo kama salama na za mafanikio kwa wafamasia wakati wa utoaji mimba wa kitabibu katika miezi 3 ya kwanza ya mimba -

 • Kutathmini ustahilifu wa utoaji mimba wa kitabibu
 • Kupeana dawa na kusimamia mchakato na athari za mara kwa mara kwa kujitegemea
 • Kutathmini ukamilifu wa utaratibu na haja ya kutembelea kliniki baadaye

Hili ni eneo la kuvutia na utafiti unaoendelea kuongezeka. Kozi hii ya mafunzo ni juhudi za kuimarisha uwezo wa wafamasia kuwasaidia wanawake ili wafaidi kutokana na utoaji mimba wa kitabibu ulio salama na wa mafanikio kwa kutoa taarifa na huduma sahihi kwa utoaji mimba wa kitabibu ndani ya wiki 10 za kwanza.

7Health worker roles in providing safe abortion care and post-abortion contraception, World Health Organization 2015

Somo la 2: Utoaji Mimba wa Kitabibu ulio Salama

In this lesson, we will explore Mifepristone and Misoprostol, the two recommended drugs to be used for safe medical abortion. Upon completing this lesson successfully, you will be able to explain both drugs classification, administration, and pharmacological effects.

2.1 Mbinu za Utoaji Mimba wa Kitabibu

Utoaji mimba wa kitabibu umekuwa maendeleo pekee muhimu katika huduma za utoaji mimba tangu kuvumbuliwa kwa pampu ya kuvuta (vacuum aspiration), na umebadilisha kabisa utoaji wa huduma za utoaji mimba. Mbinu hii huwapunguzia wateja gharama na huwapa fursa wanawake kuchukua nafasi kubwa katika huduma yao wenyewe.

Dalili za utoaji mimba kutumia vidonge zinafanana sana na zile za mimba kutoka yenyewe. Mfanano huu humpa mwanamke faida nyingi. Mbinu ya utoaji mimba wa kitabibu inachukuliwa zaidi kama utaratibu asilia unaoweza kufanywa mahali salama na penye faragha, mbinu ambayo haihitaji matumizi ya vifaa vya upasuaji na inaweza kuigiza damu ya hedhi (japo uchungu na kiasi cha damu vitatofautiana na vitategemea ukubwa wa mimba).

Ulimwenguni kote, dawa mbili zinazopendekezwa kutumika kwa ajili ya utoaji mimba wa kitabibu ni pamoja na Mifepristone na Misoprostol.

Mifepristone - Mifepristone, inayojilakana pia kama RU- 486, ni homoni yenye mvuto wa nguvu wa vipokezi vya progesteroni ndani ya mfuko wa uzazi. Inapomezwa, inapigana na progesteroni huku ikiungana na vipokezi na kuzuia athari za progesteroni. Hili linasababisha -

 • Kung’oka kwa kifuko cha kizazi kutoka kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi;
 • Kulainika na kupanuka kwa mlango wa kizazi; na
 • Ongezeko katika uwezo wa ukuta wa mfuko wa uzazi kunywea, na kuwa msingi wa Misoprostol

Mifepristone lazima imezwe, na matokeo yake huonekana baada ya saa 12-24. Kutegemea mchakato dawa hii imepitia wakati wa utengenezaji, inaweza kudumu kwa miezi24 - 488

8"https://extranet.who.int/prequal/content/prequalified-lists/medicines"

Savitz, D. A., Terry, J. W., Dole, N., Thorp, J. M., Siega-Riz, A. M., & Herring, A. H. (2002). Com-parison of pregancy dating by last menstrual period, ultrasound scanning, and their combi-nation. American journal of obstetrics and gynecology, 187(6), 1660-1666.

Wegienka, G., & Baird, D. D. (2005). A comparison of recalled date of last menstrual periodwith prospectively recorded dates. Journal of Women’s Health, 14(3), 248-252.

Misoprostol - Misoprostol ni dawa ya homoni sanisia (Aina E1) ambayo awali ilisajiliwa kwa kuzuia vidonda vya tumbo vinavyotokana na dawa zisizo kuwa na steroidi za kuzuia maumivu. Hata hivyo, tangu uvumbuzi wake wa awali, matumizi kadhaa ya Misoprostol yamegunduliwa katika Afya ya Uzazi na Jinakolojia. Misoprostol sasa hivi inatumika katika nchi nyingi kuanzisha leba, kuzuia na kutibu utokaji damu baada ya kujifungua na kutibu utoaji mimba ambao haukukamilika au utoaji mimba wa uliosababishwa. Kutokana na matumizi yake ya mengi, Misoprostol inajumuishwa katika Orodha ya Shirika la Afya Duniani ya Dawa Muhimu kwa Watu Wazima. Aidha inatambuliwa katika Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu bidhaa za kuokoa maisha kwa wanawake na watoto, hasa kwa matumizi yake ya utoaji mimba salama.

Misoprostol inaweza kutumiwa kwa njia mbalimbali, kama vile kuibana kwenye mashavu au kuiweka chini ya ulimi au kupitia kwenye sehemu ya siri. Hata hivyo, kumbuka kwamba kunywa au kumeza Misoprostol hakupendekezwi kwa sababu kwa njia hiyo uwezo wake wa kufanya kazi ndani ya mfuko wa uzazi utakuwa mbaya.

Japo kuna njia nyingi za kutumia Misoprostol, ni vyema kuchagua njia moja na kuitumia njia hiyo moja kwa dozi zote wakati unafanya utoaji mimba wa kitabibu.

Punde tu inapoingia kwenye damu, Misoprostol inabadilishwa kuwa asidi ya Misoprostol. Hii huanziasha kunywea kwa nguvu ndani ya mfuko wa uzazi, na husababisha mlango wa kizazi kulainika na kupanuka. Michakato yote miwili inasaidia kutoa mimba.

Misoprostol ni mchanganyiko imara kwa kiasi fulani katika joto (hasa ikilinganishwa na Oxytocin) lakini huharibika haraka katika unyevu mwingi na joto la juu. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba vidonge vya Misoprostol viwekwe kwenye vifuko vyenye safu mbili za alumini na kuwekwa mahala baridi na pakavu.

Mwanamke ataanza kuhisi maumivu tumboni na kutoka damu ndani ya saa 1 hadi 2 baada ya seti ya kwanza ya vidonge vya Misoprostol kuingia mwilini. Kwa wanawake wengi, kawaida mimba itatoka mwilini ndani ya saa 24 baada ya kumeza vidonge vya mwisho vya Misoprostol, japo utoaji mimba unaweza kuchukua muda zaidi ya huo kukamilika.

Kumbuka - Utoaji mimba wa kitabibu wakati fulani huitwa utoaji mimba kwa dawa, utoaji mimba wa kifamakolojia, au vidonge vya kutoa mimba. Ni muhimu kukumbuka kwamba, MA ni tofauti na uzazi wa mpango wa dharura ambao huzuia mimba kutunga.

2.2 Mwendeleo wa Usalama katika Utoaji Mimba wa Kitabibu

Katika siku za nyuma, ufafanuzi wa utoaji mimba salama ulizingatia vipengele vitatu—maarifa ya mhudumu, ujuzi wa kitabibu au kiupasuaji wa mhudumu, na usalama wa mazingira ambamo utoaji mimba unatokea. Hata hivyo, ushahidi unaoendelea kuongezeka kuhusu utoaji mimba wa kitabibu umegeuza huu mtazamo wa kiusalama. Utoaji mimba wa kitabibu ulio salama sasa unategemea maarifa sahihi kuhusu mchakato wa mimba, kazi ya dawa zilizotumiwa, na dozi na matumizi yao sahihi. Hii inamanisha kuwa vipengele vingine vya usalama, kama vile mazingira na ujuzi wa kitabibu au wa kiupasuaji wa mhudumu, yana nafasi ndogo ya kuathiri usalama na matokeo ya mchakato wa Utoaji mimba wa kitabibu. Kwa hivyo, wafamasia au wafanyakazi katika maduka ya dawa wanapokuwa na maarifa kuhusu mambo matatu yaliyotajwa hapo awali, wanaweza kuwasaidia wanawake kwa ufanisi ili kufanikisha Utoaji mimba salama.

Japo zote Mifepristone na Misoprostol (zikitumiwa ipasavyo) ni dawa salama sana, si sawa na kusema kwamba hazina hatari yoyote. Dozi zisizo sahihi za dawa za Utoaji mimba wa kitabibu zinaweza kusababisha hali ya hatari mwishowe, hasa upande wa Misoprostol. Kwa kuwa hisi ya mfuko wa uzazi iliyo na mimba kwa Misoprostol huongezeka sana kulingana na ukubwa wa mimba, ni muhimu kukumbuka kuwa kadri mimba ilivyo ndogo (ndani ya wiki 12 za kwanza), ndivyo dozi kubwa ya Misoprostol inavyohitajika kufanikisha Utoaji mimba. Mimba inavyokua, dozi ya Misoprostol inapaswa kupunguzwa kulingana ukubwa wa mimba.

Kupeana dozi ndogo ya Misoprostol kiliko inayohitajika kwa mimba ndogo kunaweza kusababisha utoaji usio kamili, na kusababisha matukio mabaya kama vile kutoka damu na maambukizi ya maradhi. Kupeana dozi kubwa ya Misoprostol kiliko inayohitajika kunaweza kusababisha kusisimka zaidi kwa mfuko wa uzazi na huenda kukasababisha kupasuka kwa mfuko wa uzazi ambako ni hatari kwa maisha.

Unapotafuta utoaji mimba wa kitabibu ulio salama, ni muhimu kukiwazia kila kimoja cha vipengele vifuatavyo - uchunguzi kubaini kama mteja anastahili, kutolewa kwa dawa mwafaka, utoaji wa huduma ya kusaidia, na utoaji wa taarifa kamili na sahihi kwa wateja.

Hivyo vipengele vinne vya utoaji mimba wa kitabibu vitachunguzwa katika sehemu iliyosalia ya kozi hii. Kila kipengele ni muhimu katika kuchangia kuleta matokeo salama na ya ubora wa hali ya juu kwa wanawake.

Somo la 3: Kuwachunguza Wateja

Katika somo hili, tutajadiliana kuhusu umuhimuwa kuwachunguza wateja kwa ajili ya utoaji mimba wa kitabibu. Tutatambua shabaha kuu za uchunguzi,na jinsi ya kufanikisha shabaha hizi kwa namna rahisi na yenye mafanikio. Baada ya kukamilisha somo hili, utaweza kuelezea umuhimuna malengo ya kupima wateja kwa ajili ya utoaji mimba wa kitabibu katika mazingira ya famasia.

3.1) Umuhimu wa Kuchunguza

Uchunguzi wa wateja unamaanisha maingiliano mafupi ya kina kati ya wafanyakazi wa maduka ya dawa na mteja kuhakikisha kuwa mteja anastahili kiafya kupokea dawa hizi, na kwamba anaweza kuendelea na utoaji mimba wa kitabibu kwa usaidizi kidogo au bila usaidizi na usimamizi wa kimatibabu.

Shabaha ya upimaji - Shabaha kuu ya upimaji ni kuhakikisha kwamba dawa na taarifa muafaka zimeweza kutolewa kwa wanawake kuhakikisha kuwa mchakato wa utoaji mimba wa kitabibu ni salama, kupunguza hatari za matatizo yanayoweza kuepukika, na kuimarisha uwezekano wa utoaji mimba wenye mafanikio.

Kwa hali nyingi, kuna maingialiano kati ya mfamasia na mteja wakati dawa za utoaji mimba wa kitabibu zinahitajika. Wafanyakazi katika maduka ya dawa wanapaswa kutumia maingiliano haya kupata taarifa kuhusu afya ya mwanamke na mimba kuhakikisha kuwa mteja anastahili utoaji mimba wa kitabibu.

Mfanyakazi wa duka la dawa anapaswa kueleza haja ya kutathmini kama mteja anastahili kwa njia fupi na wazi. Maswali machache yenye mpangilio mzuri yatazalisha majibu kuonyesha ustahili. Mifano ya maswali yanayopendekezwa yamejumuishwa katika sehemu ifuatayo chini ya malengo na yanaweza kubadilishwa na wafamasia wenyewe kulingana na mazingira, mila na desturi za wenyeji.

Wakati Fulani, inawezekana kuwa mtu anayenunua dawa za Utoaji mimba wa kitabibu kutoka kwenye duka la dawa siye anayekusudia kuzitumia. Kwa tukio kama hilo, ni muhimu kuwa mfamasia aelezee umuhimu wa kumchunguza mteja. Mfamasia anaweza kumwandalia mteja orodha ya maswali ya kujitathmini mwenyewe ikiwa anastahili na kumpa dozi muafaka ya dawa.

3.2) Malengo ya kuwachunguza wateja

Shabaha ya kuu ya kuwachunguza wateja ni kuimarisha usalama na ubora wa utoaji mimba wa kitabibu.

Lengo la kuchunguza 1 - Kutathmini kwa usahihi ukubwa wa mimba kutambua kiasi cha dozi ya dawa za utoaji mimba wa kitabibu, hasa kwa Misoprostol

Mipangilio ya dozi kwa Utoaji mimba wa kitabibu lazima iafikiane na ukubwa wa mimba ili kupata utoaji salama na wenye mafanikio. Dozi muafaka ya Misoprostol itapunguza uwezekano wa mchakato usiofaulu kutokana na dozi ndogo, au kusisimka zaidi kwa mfuko wa uzazi kwa sababu ya dozi iliyopita kiasi.

Muulize mwanamke siku yake ya kwanza ya kupata hedhi yake ya mwisho halafu upige hesabu idadi ya wiki kutumia kalenda kutoka hedhi yake ya mwisho hadi siku ambayo pana uwezekano wa kuzitumia dawa. Utafiti katika miktadha mingi umeonyesha kwamba kutumia hedhi ya mwisho hadi tarehe ya sasa ya mimba huwa sahihi na hukubalika. Mara nyingi wanawake wanaweza kukumbuka hedhi yao ya mwisho kwa usahihi.

Hakikisha kwamba mimba haijapita wiki 10 kutokana na hesabu yako. Ikiwa kulingana na hesabu yako mimba inakadiriwa kuwa ya wiki 10 au chini ya wiki 10, unaweza kupeana dawa bila wasiwasi kama inavyoelekezwa katika somo la 4.

Ikiwa kulingana na hesabu yako kuna uwezekano kwamba mimba inazidi wiki 10, basi usipeane dawa kulingana na masharti katika somo la 4. Utapaswa kurekebisha dozi ya Misoprostol kutegemea ukubwa wa mimba au kumwelekeza mama apate huduma yenye usaidizi wa kimatibabu.

Lengo la kuchunguza 2 - Tambua ishara zuizi za matumizi ya dawa za utoaji mimba wa kitabibu.

Sawa na ilivyo na matibabu na dawa zote, Mifepristone na Misoprostol zina vizuizi kama vile mzio kwa Mifepristone, Misoprostol, au dawa nyingine za kihomoni (prostaglandins), au ikiwa mwanamke ana matatizo ya kiafya ambayo yanamzuia kutumia dawa hizi.

Ishara zuizi za matumizi ya Mifepristone ni pamoja na -

 • Matumizi ya dawa za corticosteroid ya muda mrefu kwa sasa
 • Kushindwa sugu kwa adrenali
 • Porphyrias ya kurithi
 • Matatizo ya kuvuja damu
 • Matumizi ya sasa ya dawa za kuzuia damu kuganda
 • Kutopatana na au mzio unaojulikana wa Mifepristone

Ishara zuizi za matumizi ya Misoprostol ni pamoja na -

 • Kutopatana na au mzio unaojulikana wa Misoprostol au dawa nyingine za kihomoni (prostaglandins)

Wakati ambapo mwanamke ana ishara zuizi za matumizi ya Mifepristone, mpangilio wa dawa ya Misoprostol pekee unaweza kutumika kwa usalama, madamu tu pasiwe na ishara zuizi za matumizi ya Misoprostol.

Ili kutambua ishara zuizi kwa dawa za utoaji mimba wa kitabibu, fanya yafuatayo -

 • Muulize tu mwanamke ikiwa ana mzio wowote unaojulikana wa dawa za kihomoni au Mifepristone. Pia unaweza kuuliza kuhusu mzio wowote wa dawa wakati kwa sasa ili kubaini ni huduma gani nyingine ya kimatibabu unaweza kutoa au usitoe.
 • Muulize mwanamke kama anatumia dawa zozote za kuifanya damu nyepesi au ikiwa anavuja damu kwa muda mrefu baada ya jeraha. Ikiwa atajibu ndio, mhoji zaidi kutathmini kama kuna tatizo lolote la uvujaji damu.
 • Ingawa uwepo wa matatizo ya kuvuja damu ya kurithiwa ni ishara zuizi ya utoaji mimba wa kitabibabu, matumizi ya pamoja ya dozi ndogo ya Asprini au Clopidrogel (dawa ya kupigana na vigandisha-damu) kwa kawaida si ishara zuizi hasa ya dawa za utoaji mimba wa kitabibu. Ingawa hamna utafiti wa karibu uliochunguza hatari ya kuvuja damu kwa ama matibabu katika wanawake wanaoendelea kufanyiwa utoaji mimba, kwa jumla, matibabu ya dozi ndogo ya asprini haiongezi sana tatizo la kuvuja damu au kifo wakati wa utoaji. Hata hivyo, ikiwa mteja anatumia vyote dozi ndogo ya asprini na Clopidrogel, anapaswa kutathiminiwa na daktari kabla ya kupewa dawa za utoaji mimba wa kitabibu.
 • Uwepo wa porphyrias hutofautiana katika watu tofauti, na ni hali ngumu kuchunguza bila kuwepo na kituo cha afya chenye vipimo vya hali ya juu na kutembelea kituo mara kadhaa. Hata katika vituo vya afya, hali hii inaweza tu kugunduliwa kwa kukumbukia nyuma baada ya kupata dawa. Kwa hivyo, lifahamu hili na mfahamishe mteja kwamba hali hii inaweza kuamshwa kidogo na matumizi ya dawa za utoaji mimba wa kitabibu.

Kuongezea kwa masharti ya hapo juu, ni muhimu kukumbuka kwamba kuna masuala mengine ya kiafya ambayo yanaweza kulazimu kuwepo na haja ya usimamizi au msaada wa kiafya wakati wa utoaji mimba wa kitabibu. Wafamasia wanafaa kulifahamu hili na kuwapendekezea wateja kutafuta huduma ya afya inayofaa.

Lengo la kuchunguza 3 - Hakikisha kuwa mwanamke hana kifaa cha kuzuia mimba ndani ya mfuko wa uzazi.

Wakati fulani, hata wakati wanawake wanatumia kifaa cha IUD, wanaweza kupata mimba. Katika visa kama hivyo, kifaa cha IUD lazima kiondolewe kabla ya kupewa dawa za utoaji mimba wa kitabibu. Kunywea kunakosababishwa na Misoprostol kunaweza kusababisha majeraha ya mfuko wa uzazi (kama vile kutoboka) ikiwa kifaa cha IUD kimo ndani ya mfuko wa uzazi.

Muulize mama ikiwa anatumia kifaa cha IUD kwa sasa au amewahi kuwekewa kifaa cha IUD ambacho hakikutolewa. Wanawake wengi watakumbuka na wanaweza kuuhisi uzi. Waelekeze wanawake kwamba hiki kifaa sharti kiondolewe (ama na mhudumu wa afya katika kituo cha afya au na wanawake wenyewe) kabla ya kupokea dozi ya kwanza ya dawa za utoaji mimba wa kitabibu.

Peana taarifa kuhusu hatari za kutumia dawa za utoaji mimba wa kitabibu kukiwa na kifaa cha IUD ndani ya mfuko wa uzazi.

Lengo la kuchunguza 4 - Eleza kwamba utoaji mimba wa kitabibu hautafanikiwa ikiwa mimba ipo nje ya mfuko wa uzazi na kwamba mwanamke anafaa kupata huduma ya dharura ya afya kwa matibabu ya mimba iliyo nje ya mfuko wa uzazi

Tatizo jingine la kiafya linaloweza kuleta hatari kubwa kwa mafanikio ya utoaji mimba wa kitabibu ni mimba iliyo nje ya mfuko wa uzazi . Kwa sababu mimba iliyo nje ya mfuko wa uzazi ni tofauti na mimba ya kawaida ya mfuko wa uzazi, dawa za utoaji mimba wa kitabibu (zote mbili Mifepristone na Misoprostol) hazitafaulu kutoa mimba iliyo nje ya mfuko wa uzazi —ambayo ni halali katika nchi zote na huhudumiwa katika matunzo ya wakina mama..

Ni vigumu kama si kwamba haiwezekani kugundua mimba iliyo nje ya mfuko wa uzazi bila kufanya uchunguzi wa ndani ya tumbo au kutumia picha za ultrasonogramu. Ikiwa mimba yoyote iliyo nje ya mfuko wa uzazi (hasa mimba iliyo kwenye mrija wa uzazi) imepasuka, inaweza kusabababisha uvujaji damu ndani ya mwili unaohatarisha maisha. Kwa hivyo, ingawa hali hii ya kiafya haiwezi kutathminiwa wakati wa ziara kwa duka la dawa, mfamasia lazima afahamu kuhusu uwezekano huu na kupeana taarifa muafaka ili mteja atambue na kutafuta matibabu ya hali hii.

Somo la 4: Ugawaji wa Dawa za Utoaji Mimba wa Kitabibu

Katika somo hili, tutajadili na kujifunza kuhusu masuala muhimu ya kuzingatia katika utoaji wa dawa za utoaji mimba wa kitabibu. Kufikia mwisho wa somo hili utaweza kutambua dawa za kutumia katia utoaji mimba wa kitabibu kwa usahihi, dozi za hizo dawa, wakati na njia ya kuzipeana kwa utoaji wa mimba iliyo ndani ya wiki 10 za mwanzo.

4.1) Mambo ya Kuzingatia -

Baada ya hatua ya kumchunguza mteja, unapaswa kuwa umebaini ukubwa wa mimba na kugundua kuwa mteja anastahili kutumia dawa za utoaji mimba wa kitabibu.

Based on the local situation and the availability of drugs, there are two options for a medical abortion
Njia ya 1 - Mchanganyiko ambao unatumia Mifepristone ikifuatiwa na Misoprostol
Njia ya 2 - Kutumia dozi za mfulululizo za Misoprostol pekee

Ambapo njia zote mbili zinapatikana, taarifa kuhusu ufanisi wazo lazima zitolewe kwa mteja pamoja na gharama yazo ili wachague njia wanayoipendelea.

Mifepristone na Misoprostol Misoprostol pekee
Zinafaulu sana zinapotumiwa kwa mimba ya wiki 10 za kwanza (95% – 99%), kwa ufaulu unaolingana na matumizi ya Pampu ya Kuvuta (Vacuum Aspiration) Inafaa kwa ufaulu wa 75% – 90%
Hatari ya mimba kuendelea kama tukio baya la hii njia iko chini sana (<1 %) Hatari ya mimba kuendelea hata baada ya kutumia dawa uliyoandikiwa ni kubwa kidogo takribani 5 -7%
Ni ghali zaidi kwa kuwa kuna kuna aina mbili za dawa zinazotumika Gharama yake inawezekana kuwa nafuu kidogo

4.2) Jinsi ya Kutumia Vidonge vya Utoaji Mimba - Mifepristone + Misoprostol -

Unapopeana dawa zote mbili Mifepristone na Misoprostol, hakikisha kuwa umempa mteja kiwango kamili cha dawa zote. Usipeane sehemu moja tu ya dawa, kwa kuwa hii haitafanya kazi.

Mpe mteja kidonge kimoja cha 200mg cha Mifepristone na vidonge vinne vya 200mcg vya Misoprostol pamoja na maagizo yafuatayo kuhusu jinsi ya kuvitumia -

Hatua ya 1 - Meza kidonge kimoja cha Mifepristone (200 mg) kutumia maji. Wanawake wengine (hadi asilimia 40%) wanaweza kuhisi kutapika baada ya kumeza Mifepristone. Ikiwa mteja atatapika ndani ya saa moja ya kumeza kidonge cha Mifepristone, huenda kisiwe kimefanya kazi na anapaswa kurudia dozi. Ikiwa mteja atatapika baada ya saa moja kupita tangu ameze kidonge cha Mifepristone, dawa ya kutosha kutoa mimba itakuwa imeingia mwilini na haina haja kurudia dozi.

Hatua ya 2 - Subiri kwa saa 24-48. Unapaswa kumwarifu mteja asubiri kwa saa 24 kabla ya kutumia Misoprostol, lakini asisubiri kwa zaidi ya saa 48. Wakati wateja wanaposubiri, wanaweza kuendelea kufanya shughuli wazifanyazo kila siku maishani, kama vile kuitunza familia au kwenda kazini au kwenda shuleni. Wanawake chini ya asilimia 10% wanatokwa na damu au kupata maumivu ya tumbo baada ya kumeza dawa ya Mifepristone.

Hatua ya 3 - Baada ya saa 24 na kabla ya saa 48 kuisha, kunywa maji kidogo kulowesha kinywa chako. Viweke vile vidonge 4 vya Misoprostol (200 mcg kila kimoja) baina ya shavu na ufizi wa meno ya chini au chini ya ulimi wako.

Hatua ya 4 - Vibane vidonge mashavuni pako au chini ya ulimi kwa dakika 30. Hii inaweza kukikausha kinywa au kukifanya kinywa kionje kama chokaa wakati vidonge vinapoyeyuka. Meza mate yote kinywani mwako kwa njia ya kawaida na usiteme chochote kipindi hiki cha dakika 30.

Hatua ya 5 - Baada ya dakika 30, safisha kinywa chako kwa maji na kumeza mabaki yote ya vidonge.

4.3) Jinsi ya Kutumia Vidonge vya Utoaji Mimba - Misoprostol Pekee

Unapopeana Misoprostol pekee – hakikisha kuwa mteja amepata dawa kamili. Kwa kuwa ni vigumu kubaini ni wanawake gani watahitaji dozi za ziada na ni dozi ngapi, kupeana dozi pungufu huenda kukasababisha ufaulu wa chini wa utoaji mimba na kusababisha matukio mengine mabaya.

Mpe mteja vidonge 12 vya 200mcg vya Misoprostol pamoja na maagizo yafuatayo kuhusu jinsi ya kuvitumia. Unapompa mteja vidonge, usivitoe ndani ya vifuko vyake na umwarifu kwamba avitoe kwenye vifuko hivi kabla ya kuweka vidonge kinywani.

Hatua ya 1 - Kunywa maji kulowesha kinywa. Weka vidonge 4 chini ya ulimi wako na kuviacha viyeyuke. Vibane chini ya ulimi wako kwa dakika 30. Vinaweza kukikausha au kukifanya kinywa kionje kama chokaa wakati vinapoyeyuka. Usile au kunywa kitu chochote kwa dakika 30. Meza mate yote kwa njia ya kawaida na usiteme chochote kipindi hiki cha dakika 30.

Baada ya dakika 30, safisha kinywa chako kwa maji na kumeza mabaki yote ya vidonge.

Subiri kwa saa 3-4 kabla ya kundelea.

Hatua ya 2 - Rudia hatua ya 1 kwa vidonge 4 vingine baada ya saa 3 -4 hata kama utakuwa umeanza kuhisi maumivu ya tumbo.

Subiri kwa saa 3-4 baada ya kukamilisha Hatua ya 2.

Hatua ya 3 - Rudia hatua ya 1 na seti ya mwisho ya vidonge 4 baada ya saa 3 - 4 zaidi (yaani saa 6- 8 tangu uchukue dozi ya kwanza ya Misoprostol). Hakikisha kwamba unakamilisha hatua ya 3 hata kama utahisi maumivu makali ya tumboni na kuvuja damu na kuona mabaki ya mimba yakitoka.

Somo la 5: Huduma ya Usaidizi Wakati wa Utoaji Mimba wa Kitabibu

Katika somo hili, tutajadili kuhusu aina nyingine za huduma zitolewazo kwa wanawake wanaotoa mimba kitabibu. Mafunzo katika somo hili yatakuwezesha kuwasaidia wateja kukabili athari zinazotarajiwa na zile mbaya zitokanazo na utoaji mimba wa kitabibu, na kuwafanya wateja waridhike zaidi na utoaji mimba wa kitabibu.

zaidi ya kupeana dawa sa Utoaji mimba wa kitabibu, kuna mambo mengine ambayo unaweza kufanya kama mfamasia ambayo yatamfanya mteja ajihisi vizuri wakati wa Utoaji mimba wa kitabibu. Mambo haya ni sehemu ya huduma na yanahakikisha kuwa huduma unayoitoa ni ya ubora wa juu na kumridhisha mteja.

Dalili za kawaida zinazoshuhudiwa wakati wa Utoaji mimba wa kitabibu ni pamoja na maumivu ya tumboni na kuvuja damu. Dalili hizi zote mbili ni muhimu na zinatarajiwa kutoka kwenye mchakato wa Utoaji mimba wa kitabibu. Ni muhimu kwamba wanawake wote waarifiwe kuhusu dalili hizi na wapewe huduma ya usaidizi inayofaa mapema ili kuwasaidia kukabiliana na dalili hizi.

Juu ya dalili hizi, sawa tu na matibabu mengine yoyote, baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na athari mbaya na zinaweza kuathiri hali nzima ya mteja wakati wa Utoaji mimba wa kitabibu. Ni muhumu wanawake wafahamu dalili zinazotarajiwa ambazo ni muhimu ili Utoaji mimba ukamilike na athari zinazotokana na kutumia dawa.

Ingawa athari za muda mrefu au athari kubwa ni nadra wakati wa Utoaji mimba wa kitabibu, athari ndogo ndogo ni za kawaida. Kwa kawaida athari hizi hutoweka ndani ya saa 4-6 baada ya kutumia Misoprostol. Hakuna athari za muda mrefu zinazotokana na Utoaji mimba wa kitabibu.

Huduma ya usaidizi inalenga kukabili ipasavyo dalili na athari za dawa za Utoaji mimba wa kitabibu na kuwasaidia wateja kuwa Utoaji mimba salama na kupendeza.

5.1) Kuzikabili Athari Zinazotarajiwa

Kabla ya kuanza utoaji mimba, hakikisha kwamba mwnamke amejua kwamba -

 • Hapaswi kushtuka ikiwa atavuja damu sana na kuhisi maumivu ya tumbo kuliko yale ya hedhi ya kawaida.
 • Anaweza kula na kunywa apendavyo baada ya kumaliza kutumia dawa.
 • Anapaswa kujaribu na kukaa mahali pazuri hadi atakapojihisi vizuri.
 • Anapaswa kutambua wazi athari ni nini na ishara za hatari ni nini.
 • Unaweza kumpatia dawa na ushauri kuhusu jinsi ya kukabili athari lakini pia anapaswa kuwa na mpango mzuri wa kupata huduma ya matibabu ya dharura kulingana na hali ya nchi.
 • Wanawake wengi wanahisi vizuri chini ya saa 24.

Ni muhimu kumwarifu mwanamke kwamba nyingi za athari zinatokana na Misoprostol (kuliko Mifepristone) na kwa hivyo anapaswa kujitayarisha kuwa sehemu salama, nzuri na ya faragha kabla ya kutumia Misoprostol.

Dalili zinazotarajiwa ni pamoja na -

Maumivu ya tumboni
Wanawake wengi wanapata maumivu ya tumboni ndani ya dakika 30 baada ya kutumia Misoprostol. Maumivu ya tumboni ni ishara kwamba mfuko wa uzazi umeanza kunywea na uko katika hatua ya kuyaondoa mabaki ya mimba inayotoka. Hii ni ishara kuwa dawa imefanya kazi. Maumivu ya tumboni yanakuwa na uchungu. Kiwango cha uchungu kinabadilika pakubwa na kinategemea ukubwa wa mimba, uthabiti wa minyweo ya mfuko wa uzazi, kiwango cha wasiwasi wa mteja, na kiwango cha mtu cha kustahimili uchungu.

Uvujaji wa damu
Wanawake wengi watavuja damu ikifuatana kwa karibu na maumivu ya tumbo. Ingawa wanawake chini ya asilimia 10% wataanza kutoka damu baada ya kutumia Mifepristone, wanawake wengi wataanza kutokwa na damu baada ya dozi ya kwanza ya Misoprostol. Baada ya kuanza, kutoka damu kunaweza kudumu kwa saa kadhaa na huongezeka zaidi wakati wa kutoa nje mabaki ya mimba. Wanawake wanaweza kushuhudia vipande vikubwa vya damu iliyoganda au tishu wakati wa hatua ya utoaji na hawapaswi kushtuka kwa kuona hili wakati wa hatua ya kuondoa mabaki ya mimba.

Kiasi cha damu na mtindi wa uvujaji unatofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwengine na hutegemea ukubwa wa mimba. Kwa wanawake wengi, uvujaji damu utapungua saa 1-2 baada ya kutoa nje mabaki ya mimba, na kutaendelea kwa wiki moja hadi mbili huku kukiendelea kufifia. Baadhi ya wanawake hutoka damu au kuona madoa ya damu kwa hadi wiki 4 baada ya kutumia vidonge vya utoaji mimba wa kitabibu.

Hizi dalili mbili zote ni muhimu kwa sababu huonyesha kuwa dawa zinafanya kazi. Kupunguza ukali wa maumivu ya tumboni na kumtuliza mwanamke, ni sharti apewe dawa za maumivu.

Unapomshauri mwanamke kuhusu jinsi ya kuyakabili maumivu wakati wa Utoaji mimba wa kitabibu, angazia yafuatayo -

 • Pendekeza njia zisizo za dawa za kupunguza maumivu na wasiwasi, kama vile kuwa mahali pazuri, kusikiza muziki, kuepuka kazi nzito, na kutumia chupa ya maji moto kukanda tumbo (sawa na zile zitumiwazo wakati wa hedhi)
 • Peana dawa za maumivu kwa wanawake wote wanaotoa mimba kitabibu. Kwa kawaida dawa hizi zinapaswa kupeanwa pamoja na Mifepristone na/au Misoprostol. Dawa za maumivu zisizo na steroidi (NSAIDS) kama vile Ibuprofen, Diclofenac n.k. Zinafaa zaidi kwa kupunguza uchungu mkali kwa wanawake wengi wanaoendelea na utoaji mimba wa kitabibu. Dozi zinazopendekezwa za NSAIDS za kawaida ni

  • Ibuprofen – 400 – 800 mg kila baada ya saa 6-8 (dozi ya juu zaidi ni 3200mg ndani ya saa 24)
  • Diclofenac sodium – 50 mg kila baada ya saa 12 (dozi ya juu zaidi ni 150mg ndani ya saa 24)

Ili kuhakikisha kuwa dawa za kumezwa zinafanya kazi vizuri zaidi, zinaweza kumezwa dakika 30–45 kabla ya kuchukua dozi ya Misoprostol. Wanawake wanapaswa waarifiwe kutumia dawa za maumivu mapema kwa sababu zinachukua muda kufanya kazi. Wasisubiri hadi uchungu unapozidi ndipo watumie dawa hizi. Ni muhimu kukumbuka kwamba paracetamol (ya kumeza au kupitia njia ya haja kubwa) haipunguzi maumivu wakati wa utoaji mimba wa kitabibu.

5.2) Kuzikabili Athari za Kawaida

Juu ya athari zilizotangulia kuzungumziwa, Misoprostol vilevile ina athari ambzo si nzuri. Visa na ubaya wa athari hizi hetegemea njia ambayo Misoprostol imetumiawa. Njia za kutumia kwa kubana kwenye mashavu au kuweka chini ya ulimi kwa kawaida zinahusishwa na utokeaji wa athari. Kwa hivyo ni muhimu kuwaarifu na kuwasaidia wanawake kukabili athari hizi zisizo nzuri kwa ajili ya utoaji mzuri.

Kuhisi Kichefuchefu na Kutapika
Kichefuchefu, kizunguzungu, na kutapika huweza kutokea kwa baadhi ya wanawake na huisha saa 2 hadi 6 baada ya kutumia Misoprostol. Wakati mwingine kichefuchefu kutokana na mimba huweza kuchanganyikana au kuwa kibaya zaidi baada ya matumizi ya Misoprostol. Hili linaweza kuwachafua sana wanawake na huweza kuwatapisha au kuwaletea kiu. Kwa kawaida hili kuisha wakati mimba imetoka.

Ushauri kama vile kula chakula kidogo na kikavu huweza kusaidia kukabili athari ya kichefuchefu. Unaweza kumpa mteja dawa za ziada kama vile Domperidone, Ondansetron na Metaclopromide (kwa kuwa matumizi yake hayahitilafiani na dawa za utoaji) ili kukabiliana na athari za dawa.

Kizunguzungu
Hadi asilimia 20% ya wanawake wanaotumia Misoprostol wanaweza kuhisi kizunguzungu kisichoelezeka. Kuhakikisha kwamba wanawake hawapati njaa na wamelala chini husaidia kukabili athari hii.

Maumivu ya tumbo na Kuharisha
Athari nyingine tatizi ya matumizi ya Misoprostol ni kwamba baadhi ya wanawake (hadi asilimia 40%) wanaharisha kidogo hadi wastani. Katika baadhi ya visa, kutumia Misoprostol kwa chakula husaidia kupunguza dalili hii. Ingawa athari hii hujizuia yenyewe na huisha ndani ya siku moja baada ya dozi ya mwisho ya Misoprostol, dawa za ziada kama vile Loperamide zaweza kupeanwa kuwasaidia kuikabili athari hii.

Joto na Baridi
Kutokea kwa joto hutegemea dozi ya Misoprostol na njia ya matumizi (matukio mengi yakipatikana kwa dozi ya juu zilizotumiwa kwa kuwekwa chini ya ulimi). Hata hivyo, kunaonekana kuwepo na tofauti za urithi kati ya makabila. Wanawake wengi wanaotumia njia ya kuweka chini ya ulimi hupata ongezeko la joto la muda mfupi linaloambatana na baridi. Joto huwa la juu saa 1-2 baada ya kutumia Misoprostol na kawaida huisha ndani ya saa 8 baada ya dozi ya mwisho. Dawa ya Ibuprofen ikitumika kukabili uchungu husaidia kuikabili athari hii vilevile. Ikiwa hiyo haitoshi na joto bado linasumbua, paracetamol yaweza kutimika juu ya Ibuprofen. Hata hivyo tahadhari inafaa kuchukuliwa kupunguza jumla ya matumizi ya NSAID ndani ya kipindi cha saa 24.

Somo la 6: Kutoa Taarifa Sahihi na Kamili

Katika hili somo la mwisho, tutazungumzia taarifa nyingine muhimu ambazo unafaa kujua ili kuwasaidaia wanawake wanaopitia utoaji mimba wa kitabibu kwa matokeo salama. Baada ya kukamilisha mafunzo haya kwa mafanikio, utaweza kutoa taarifa iliyo wazi na sahihi kwa baadhi ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu utoaji mimba wa kitabibu, kuwasaidia wanawake kutambua ishara hatari, na kukabili maswali ya wateja wanaorudi katika duka lako la dawa wakiwa na maswali baada ya utoaji mimba wa kitabibu.

6.1) Muda wa Utoaji Mimba

Aghalabu mimba hutoka ndani ya saa 24 baada ya kutumia vidonge vya mwisho vya Misoprostol. Hata hivyo, mchakato mzima wa utoaji mimba unaweza kuendelea katika siku zinazofuata huku wanawake wengi wakimaliza mchakato wa utoaji mimba kwa siku 7. Baadhi ya wanawake wanaweza kuendelea na mchakato kwa muda mfupi baada ya siku 7. Kwa sababu mwanzo na kipindi cha kutoka damu na maumivu ya tumbo huwa tofauti kwa kila mwanamke, ni vigumu kutabiri hali itakavyokuwa. Almuradi mwanamke anatoa nje mabaki ya mimba, hapati ishara za hatari, na anapata upungufu au kumalizika kwa dalili za mimba, hakuna jambo la jingine la kufanya.

Kuvuja damu nyingi kwa jumla hutokea wakati mimba yenyewe inatoka. Mara nyingi hali hii huambatana na kuvuja damu nyingi kuliko damu itokayo wakati wa hedhi kubwa na maumivu ya tumbo. Kutoka kwa damu na maumivu ya tumbo hupungua baada ya mabaki ya mimba kutoka. Damu kiasi sawa na kile cha hedhi itaendelea kwa hadi wiki mbili baada ya kutoa mimba. Hata hivyo kiasi cha damu inayotoka lazima kiendelee kupungua kadri muda unavyosonga.

Ufuatiliaji baada ya utoaji mimba wa kitabibu

Wanawake ambao hutumia Mifepristone na Misoprostol kwa jumla hawahitaji kurudi tena kumwona mhudumu wa afya maadam hawahisi tena dalili za mimba baada ya kutoa mimba, wanajisikia wazima wa afya, na hawatoki damu nyingi.

Hata hivyo, wanapotumia utoaji mimba wa kitabibu wa Misoprostol pekee, hadi asilimia 10% ya wanawake wanaweza kuendelea kuhisi mimba na kuwa na mimba—hali ambapo Misoprostol haikufanikiwa kuitoa mimba. Wanawaka kwa hivyo wanapaswa kupatiwa ushauri kuhusu umuhimu wa kumtembelea mhudum wa afya wanayenwamini kwa muda wa hadi siku 7 ili kuhakikisha kuwa mchakato umekamilika na kwamba hawahitaji huduma zaidi.

Kutegemea mazingira ya anakotoka, hii inaweza kuwa changamoto kwa sababu ya unyanyapaa mkubwa au hali ya kisheria. Wafamasia wanaweza ama kutoa taarifa kuhusu madaktari, manesi au wakunga ambao wanajulikana kutoa huduma salama, au wawashauri wateja kupata matibabu katika vituo afya vya umma kwa kueleza kwamba mimba ilitoka yenyewe.

6.2) Ishara za Hatari na Jinsi ya Kizikabili

Kama ilivyotajwa awali, Utoaji mimba wa kitabibu ndani ya miezi mitatu ya kwanza ni utaratibu salama sana na kwa hivyo matatizo makubwa huwa nadra. Hata hivyo, ni muhimu kwamba wanawake wanapatiwa taarifa sahihi kuhusu ishara za hatari ya matatizo makubwa ili kwamba waweze kuzitambua na kuchua hatua ya mapema kuepuka madhara mabaya. Ishara za matatizo wanazoweza kushuhudia ni -

 • Kuvuja damu nyingi - kulowesha zaidi ya vitambaa viwili vya hedhi kwa kila saa kwa saa mbili mfululizo, hasa kukiambatana na kisuli cha muda mrefu, kizunguzungu, na kuzidi kuwa mchovu
 • Kutotoka damu au kutoka damu kidogo sana (sawa na hedhi ndogo) baada ya kutumia Misoprostol (uwezekano wa mimba iliyo nje ya uterus)
 • Joto la 38°C (100.4°F) au zaidi au kupata joto jingi baada ya siku ambayo dozi ya mwisho ya Misoprostol imetumiwa
 • Harufu mbaya kutoka sehemu za siri na/au kutoa maji
 • Maumivu makali ya tumbo siku moja baada ya kutumia Misoprostol
 • Kujihisi mgonjwa sana ukiwa na joto jingi au bila joto, kichefuchefu kikali kisichoisha, kutapika au kuharisha kwa zaidi ya saa 24

Mwanamke anayehisi yoyote kati ya ishara hizi za hatari huenda amepata madhara mabaya na anapaswa kupata matibabu mara moja katika kituo cha afya. Katika visa vingi suluhisho dogo kutoka kwa mhudumu wa afya linatosha kukabili matatizo yaliyotajwa hapo juu. Mara chache sana, wanawake wanaweza kuhitaji kulazwa, suluhu kwa njia ya upasuaji, kuongezewa damu au matibabu ya hali ya juu.

Kufikia mwishoni mwa maingiliano na mteja, ambaye amepata dawa ya utoaji mimba kutoka kwako, tafadhali angalia kama -

 • Mwanamke anaelewa ni lini na ni vipi atatumia vidonge vya Mifepristone na/au Misoprostol kabla ya kutoka kwenye duka la dawa.
 • Hakikisha kuwa mwanamke anaelewa ni wakati gani na ni vipi kujipea mwenyewe dawa za ziada zikiwemo dawa za kuzuia maumivu.
 • Hakikisha kwamba mwanamke anaelewa ni wakati gani wa kuwasiliana na mhudumu wa afya kunapotukia ishara za hatari.

6.3 Wateja wanaorudi – visa vya mara kwa mara na jinsi ya kuvikabili

Katika mazingira fulani, wanawake wanaweza kurudi dukani mwako na maswali, majibu au wasiwasi zaidi. Hapa chini ni visa vya mara kwa mara wanavyoshuhudia wafamasia na wafanyakazi wa maduka ya dawa ambao wanapeana utoaji mimba kitabibu.

 • Kutotoka au kutoka damu kidogo baada ya kutumia dawa za kutoa mimba -
  Hali hii inaweza kuashiria moja au zaidi ya mambo yafuatayo -
  • Uwezekano wa mimba iliyo nje ya mfuko wa uzazi. Kutotoka damu na kutotoa mabaki ya mimba kufuatia utoaji mimba wa kitabibu kunafaa kudokeze mara moja uwepo wa mimba nje ya mfuko wa uzazi na mwanamke anapaswa kushauriwa kupata matibabu ya haraka katika kituo cha afya kuitibu mimba iliyo nje ya mfuko wa uzazi.
  • Utoaji mimba wa kitabibu ambao haukufaulu. Katika visa vichache, kwa sababu mbalimbali, Utoaji mimba wa kitabibu hukosa kufaulu licha ya mwanamke kufuata maagizo yote. Katika visa kama hivyo wanawake wanapaswa kushauriwa kuwa hizi dawa zinaweza kuwa hatari baadaye kwa mimba inayoendelea na hivyo basi wanapaswa kupata matibabu mara moja na kutathmini upya uchaguzi wao.
  • Kasoro katika maumbile ya mfuko wa uzazi. Katika visa vichache, kasoro za kimaumbile katika mfuko wa uzazi zinaweza kuzuia kiasi cha damu inayotoka kufuatia utoaji mimba wa kitabibu. Hili liweza kubaishwa tu na kukabiliwa na picha za ultrasonogramu au kupitia njia nyingine za upigaji picha. Kwa hivyo wanawake wanapaswa kushauriwa kupata matibabu kutoka mhudumu wa afya anayefaa.
 • Kuendelea kutoka damu nyingi hata baada ya siku 7 -
  Ikiwa wanawake hawashuhudii kupunguka kwa kiasi cha damu inayotoka au mtindo wa kutoka damu baada ya siku 7 kufuatia utoaji mimba wa kitabibu wanapaswa kuchunguzwa na mhudumu wa afya kuhakikisha kwamba utoaji mimba umekamilika. Katika visa vingi, wanawake hukumbwa na utoaji usio kamili kwa baadhi ya mabaki ya mimba kusalia ambayo husababisha huku kutoka damu. Aidha wanawake walio na uvimbe ndani ya mfuko wa uzazi wanaweza kuendelea kutoka damu nyingi na wanapaswa kupata matibabu katika kituo cha afya.
 • Kuendelea kwa ishara na dalili za mimba -
  Wanawake wanapotoa taarifa kuhusu hali hii kufuatia matumizi ya Misoprostol pekee kwa utoaji mimba wa kitabibu—mashaka makubwa yatakuwa kwa utoaji ambao hakufaulu. Kwa hali kama hizo, wanawake wanapaswa kushauriwa kwamba dawa hizi zinaweza kuwa hatari kwa mimba inayoendelea na kwa hivyo wanapaswa kupata matibabu mara moja na kutathmini upya uchaguzi wao. Kutegemea hali ya atokako na upatikanaji wa wahudumu wengine wa utoaji, ama unaweza kumtuma kwa mhudumu wa utoaji salama kutoa mimba kwa njia ya upasuaji au ajaribu dozi nyingine ya utoaji mimba wa kitabibu kutegemea uchaguzi wa mteja.
 • Vipimo vya mkojo vinaonyesha mimba bado ipo—nifanye nini?
  Wanawake wengi kawaida hupima mimba kwa vipimo vya mkojo siku chache baada ya utoaji mimba wa kitabibu kuhakikisha kwamba mimba ilitoka. Kipimo cha kawaida cha mimba (huuzwa kwenye maduka mengi ya dawa) kimeundwa kuweza kuonyesha matokeo chanya hata wakati ambapo kuna kiasi kidogo cha homoni za mimba (Beta Human Chorionic Gonadotrophin- HCG). Kwa sababu huchukua hadi muda wa wiki 3 homoni za mimba kutoweka baada ya mimba ya chini ya wiki 10 kutolewa, kupima mimba kwa mkojo huweza kuonyesha kwamba mimba bado ipo. Mwelezee mteja hii mantiki na kumtuliza. Mwambie apime baada ya wiki 3 ndipo ajue bayana. Mshauri kwamba kutoweka kwa dalili za mimba ni kiashiria sahihi cha kufanikiwa kwa utoaji mimba wa kitabibu.

Tovuti hii inaweza kuhitaji kuki zisizojulikana na huduma anuwai za mtu mwingine ili iweze kufanya kazi kunavyotakikana. Unaweza kusoma Sheria na Masharti yetu na Sera za Faragha . Ukitaka kuendelea kutumia tovuti hii, ni sharti utupe idhini ili uweze kufanya hivyo.