Kozi ya utoaji mimba na vidonge kwa wanafunzi wa matibabu.

 • 1.1 Uavyaji mimba – mtazamo wa kimataifa
 • 1.2 Usalama wakati wa uavyaji mimba
 • 1.3 Uavyaji Salama wa Mimba – Ufafanuzi na mbinu
 • 2.1 Haki za wagonjwa
 • 2.2 Maadili ya kiafya yanayohusishwa na uavyaji mimba
 • 2.3 Kuhakikisha utunzaji wa wagonjwa wa uavyaji mimba kwa njia ya heshima
 • 3.1 Anatomia Muhimu ya Uzazi
 • 3.2 Utumiaji wa dawa katika uavyaji mimba
 • 4.1 Lengo la kufanya utunzaji wa kabla ya uavyaji mimba
 • 4.2 Malengo ya utunzaji wa kabla ya uavyaji
 • 5.1 Jinsi ya Kutumia Tembe za Uavyaji Mimba: mifepristone + misoprostol
 • 5.2 Jinsi ya Kutumia Tembe za Uavyaji Mimba: Misoprostol Tu
 • 6.1 Madhara yanayotarajiwa na ushughulikiaji wayo
 • 6.2 Madhara na jinsi ya kuyashughulikia
 • 6.3 Dalili za maonyo ya madhara na jinsi ya kuziangazia
 • 7.1 Fuatilia hali ya wagonjwa wanaopitia uavyaji mimba kutumia dawa
 • 7.2 Matibabu ya uavyaji mimba ambao haukukamilika
 • 7.3 Uwezo wa kupata mimba baada ya uavyaji mimba
 • 7.4 Huduma zingine za kiafya ambazo zinahusiana na uavyaji mimba
Somo la 1- Muhtasari wa Uavyaji Mimba

Uavyaji mimba unafafanuliwa kama utoaji wa mimba ambayo imetungwa kwenye nyumba ya uzazi. Uavyaji mimba unaweza kufanyika bila kutarajia kutokana na matatizo ya mama mjamzito yanayopelekea mimba kutoka au kuaviwa kutumia dawa. Neno "kupoteza mimba" mara nyingi huchukuliwa kama uavyaji mimba huku neno "uavyaji mimba" likitumika kurejelea uavyaji mimba unaofanyika kitaalam.

1.1) Uavyaji mimba – mtazamo wa kimataifa

Uavyaji mimba ni tokeo la kiuzazi kote ulimwenguni ambapo mimba hutolewa kabla ya mtoto kukua na kuzaliwa. Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Taasisi ya Guttmacher inaonyesha kuwa moja kati ya mimba nne kote duniani iliaviwa kati ya mwaka 2010-2014. Taasisi ya Guttmacher inakadiria kuwa kati ya mwaka 2010-2014, visa milioni 56 vya uavyaji mimba viliripotiwa duniani kote. Hii inawakilisha asilimia 25 ya mimba zote kati ya mwaka 2010 hadi 2014. Katika mataifa yaliyoendelea, idadi hii ilipunguka kutoka asilimia 39 hadi 28 kati ya mwaka 1990-1994 na 2010-2014, huku idadi hii ikiongezeka kutoka asilimia 21 hadi 24 katika nchi zinazoendelea.

Wanawake wengi huenda kutafuta huduma za kuavya mimba kwa sababu walipata mimba wakati hawakutarajia. Huku idadi kubwa ya wanawake hawa hawahitaji kupanga uzazi, ni muhimu kukumbuka kuwa mbinu zote za upangaji uzazi zinaweza kufeli kwa wakati fulani na wanawake watatafuta kuavya mimba hata wakati wamepanga uzazi. Ni muhimu pia kueleza kuwa, kwa mujibu wa WHO na Taasisi ya Guttmacher, tatu kati ya mimba nne zilizoaviwa zilifanywa na watu walio kwenye ndoa.

Wakati uavyaji mimba hufanywa na wataalam kwa kutumia vifaa na dawa mwafaka, mbinu bora na kiwango kizuri cha dawa, na kwenye mazingira safi katika siku za mwanzo za mimba, utaratibu huu huwa salama zaidi bila hatari ikilinganishwa na mimba iliyokomaa.ii.

Hata hivyo, uavyaji mimba ambao haufuati viwango vilivyotajwa unaweza kupelekea matatizo zaidi ambayo yanaweza kusababisha kifo. Katika nchi zinazoendelea, uavyaji mimba usiozingatia taratibu salama huchangia idadi kubwa ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua. Utafiti wa hivi majuzi kuhusu vifo vya akina mama wakati wa kujifungua unaonyesha kuwa kati ya asilimia 8-18 ya vifo vya akina mama huhusishwa na uavyaji mimba ambao si salama, na idadi ya vifo hivyo ni kati ya watu 22,500 hadi 44,000.iiiiv v.

1.2) Usalama wakati wa uavyaji mimba

Ongezeko la ufikiaji wa dawa za uavyaji mimba limechangia jinsi ambavyo suala la uavyaji mimba kwa njia salama linavyotazamwa na jamii ya wataalam. Kwa kuegeme utafiti uliofanywa na taasisi ya WHO na Guttmacher, WHO ilitoa mfumo mpya wa kutathmini katika kuelewa suala la usalama katika uavyaji mimba1.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la afya la The Lancet , mnamo Septemba 2017, WHO inatambua kuwa uavyaji mimba huwa salama iwapo - 1) Unatumia mbinu ya muda mwafaka wa kuavya unaopendekezwa na WHO 2) Anayetekeleza uavyaji huu ana ujuzi mwafaka.

Kwa kuwa uavyaji mimba unaweza kufanywa kwa kutumia dawa (unaojulikana kama uavyaji wa kiafya) au kwa upasuaji (kama vile usafishaji wa njia ya uzazi, upanuzi au utoaji), uelezaji huu mpya wa usalama hutambua kuwa watu, maarifa, na viwango vya kiafya kwa uavyaji unaopangiwa ni tofauti kwa uavyaji wa kutumia dawa au upasuaji. Ni muhimu kukumbuka kuwa mbinu zinazohitajika katika kutekeleza uavyaji mimba wa kutumia dawa zinaweza kuptikana haraka kwa mafunzo yaliyopangika. Pia kuna kupunguka kwa haja ya uthibiti wa miundombinu na uambukizaji maradhi wakati wa kutekeleza uavyaji kwa kutumia dawa ikilinganishwa na upasuaji.

Kinyume na uavyaji salama, ule ambao si salama kama unavyoelezwa na WHO kama utaratibu wa utoaji wa mimba ambayo haihitajiki, ni ule unaofanywa na watu ambao labda hawana ujuzi unaostahili au katika mazingira ambayo hayazingatii viwango vya chini vya kiafya au yote mawili. Madhara ya kiafya ya uavyaji usio salama hutegemea mahali uavyaji unafanyika; ujuzi wa anayefanyisha utaratibu huu; mbinu inayotumika; hali ya afya ya mwanamke; na umri wa mimba inayoaviwa. Katika kulinganisha, taratibu ambazo si salama za uavyaji mimba zinaweza kujumuisha a) uingizaji wa kifaa kwenye nyumba ya uzazi, kama vile mizizi, vifaa vya chuma, au dawa za kienyeji; b) upanuzi na ukwarizaji kwenye sehemu ya ndani ya nyumba ya uzazi unaofanywa na watu ambao si wataalam; c) umezaji wa vitu au dawa ambazo ni hatari; au d) utumiaji wa nguvu za kuumiza kuharibu mimba. Haya yote yanaweza kupelekea matatizo zaidi ya kiafya au hata kuhatarisha maisha.

Uendelezaji wa Taratibu Salama za Uavyaji mimba Kutumia dawa

Zamani, WHO ilieleza uavyaji mimba kwa njia salama kuwa uliangazia uhalali wa huduma, ujuzi wa mtoaji huduma, na usalama wa mazingira ambapo uavyaji huu unafanyikia. Hata hivyo, kufuatia ongezeko la ushahidi wa mabadiliko katika uavyaji mimba, viwangowezi vya kiusalama katika uavyaji mimba vimepewa dhana mpya.

Uainishaji wa taratibu salama za uavyaji mimba

Uavyaji mimba kwa njia salama - Utumiaji wa mbinu inayopendekezwa pamoja na mtaalam aliyehitimu

Uavyaji mimba ambao si salama sana - Utumiaji wa mbinu ambayo imepitwa na wakati inayofanywa na mtaalam aliyehitimu au matumizi wa dawa ambazo hazipendekezwi.

Njia ambayo si salama ya uavyaji mimba - umezaji wa dawa au vitu visivyokubalika kiafya ili kuavya mimba au utumiaji wa mbinu mbovu na mtu ambaye hana ujuzi.

Mbali na uainishaji huu wa awali wa njia za uavyaji mbimba kiuslama, WHO hivi majuzi imetoa uainishaji wa aina tatu wa uavyaji salama wa mimba. Makundi hayo matatu ni - salama, si salama sana na si salama kabisa. Mbinu ya "si salama sana" na "si salama kabisa" zinachukuliwa njia ambazo si salama katika kutekeleza uavyaji mimba. Uainishaji huu unatilia maanani vigezo kadha ambavyo ni wahusika, ujuzi wao, mbinu zilizotumika, upataji wa habari na utunzaji unaotolewa katika utaratibu mzima. Haya yote hupelekea uangaziaji wa uavyaji mimba kama utaratibu mfululizo. Uainishaji huu pia huwasaidia wanawake na watoaji huduma za kiafya kuelewa ni sehemu gani katika uavyaji mimba kwa njia salama zinahitaji kuimarishwa.

Ni muhimu kukumbuka kuwa japo dawa za mifepristone na misoprostol ni salama zinapotumika ipasavyo, si kwamba hazina madhara yoyote. Matumizi ya kiwango kisichostahili katika uavyaji mimba yanaweza kupelekea hali hatari, hasa matumizi ya misoprostol. Nyumba ya uzazi huadhirika zaidi na misoprostol kadri mimba inavyozidi kukua. Hivyo, ni muhimu kubaini kuwa siku za kwanza za mimba (muhula wa kwanza) unahitaji kiwango kikubwa cha misoprostol ili kufanikisha uavyaji mimba. Kadri mimba inavyozidi kukua ndivyo kiwango cha misoprostol kinastahili kupunguzwa kuwiana na umri wa mimba.

Utoaji wa misoprostol kwa kiwango chini ya inavyohitajika siku za mapema za ukuaji wa mimba unaweza kupelekea kutotoka kwa mimba inavyostahili, hali ambayo inaweza kupelekea utokaji wa damu na maambukuzi mengine. Utoaji wa kiwango zaidi ya inavyohitajika wa dawa ya misoprostol, kwa upande mwingine, unaweza kusababisha urarukaji wa nyumba ya uzazi ambao ni hatari kwa maisha.

Hatimaye, wazo hili la usalama linaangazia usalama wa taratibu za hospitalini za huduma za kiafya zinazotolewa. Ni muhimu kwa mtoaji huduma wa kiafya kufahamu kuwa, katika mazingira mengi, haja na utaratibu wa kutekeleza uavyaji mimba unaweza kuathiri hali ya kiafya na kiusalama ya mwanamke. Visa vya ufungiwaji, mauaji ya kiheshima, na dhuluma kwa wanawake wanaotaka na kupokea huduma za uavyaji mimba kote duniani. Kama watoaji huduma za kiafya wanaolenga kufanikisha afya ya kijumla, ni muhimu kuwa wanafunzi wa taaluma udaktari kuyafahamu haya kwa muktadha halisi.

1.3) Uavyaji Salama wa Mimba – Ufafanuzi na mbinu

Kwa kuangazia upitiaji wa kitaratibu wa ushahidi, WHO inapendekeza mbinu salama zifuatazo. Tafadhali kumbuka kuwa, sawia na nyanja zingine za sayansi ya udaktari, maendeleo ya kiteknolojia, ushahidi wa kimatibabu na utafiti utapelekea kuimarishwa na uboreshaji wa miongozo ya kitaalam.

 • Upulizaji pumu (kwa njia ya kawaida au kielektroniki) - Hii ni mbinu ya kiupasuaji ambapo mimba hutolewa kutumia upulizaji wa kutumia tubu ya plastiki inayoingizwa kwenye nyumba ya uzazi. Upulizaji huu unafanywa kwa njia ya kawaida au kutumia pampu ya kutumia umeme. Kwa kuwa mbinu inayotumika si ya chuma, na dawa unayopulizwa ni ya kiwango cha chini, utaratibu huu ni salama na hupunguza hatari ya kuharibiwa kwa viungo ikitumiwa ipasavyo. Mbinu hii inatumika kuavya mimba ya kati ya wiki 12-14.
 • Uavyaji wa kutumia dawa (MA) - Katika mbinu hii matumizi ya dawa aina mbili au dawa inayorudiwa vya aina moja ya dawa hupewa mama kuavya mimba. Hii ni njia isiyotumia upasuaji, isiyohitilafiana na njia ya uzazi, na huitoa mimba. Dawa ambazo hutumika kwa kawaida ni Misoprostol peke yake au kutumiwa kwa pamoja na Mifepristone. Kwa mujibu wa tafiti nyingi za kiafya, WHO na mashirika mengine ya kimataifa yametambua maelekezo mazuri zaidi na taratibu za matumizi ya dawa hizi katika kutekeleza uavyaji mimba salama. Kiwango cha dawa kinachotumika hutegemea na umri wa mimba ili kupata matokeo bora yenye madhara machache mno kwa mwanamke. Mbinu hii inaweza kutumika wakati wowote wa ujauzito, kwa kubadilisha kiwango cha dawa kinachotumika ili kufanya uavyaji.
 • Upanuzi na Uondoaji - Baada ya majuma 14 ya ujauzito, WHO inapendekeza utaratibu unaoitwa Upanuzi na Uondoaji, ambapo dawa au vifaa maalum vya upanuzi hutumika kufungua mlango wa uzazi na mimba hutolewa kutumia kifaa cha kushika kuwili. Huu ni utaratibu wa hali ya juu na changamano wa kiafya unaofanywa na wataalam wenye ujuzi wa hali ya juu na kwenye mazingira mwafaka.

Ni muhimu kukumbuka kuwa Upanuzi na Uondoaji unaojulikana kama "D&C" au "Uondoaji" HAUCHUKULIWI kuwa salama kufuatia ushahidi uliopo, hivyo basi WHO haiupendekezi kama njia salama ya kuavya mimba.

Somo la 2: Uavyaji Mimba na utunzaji wake

Uavyaji mimba umetambuliwa kama suala la haki za kibinadamu na wadau wengi wakiwemo serikali, mashirika ya kiraia, na makundi ya kutetea haki. Ingawa inatambuliwa kama suala la haki za kibinadamu na sehemu ya utunzaji muhimu wa kiafya, ni suala changamano linalohusisha maadili, dini na utamaduni. Hili hupelekea suala hili kuwa la mzozo na gumu kulijadili waziwazi na mbele ya watu au hata kwenye taasisi.

Changamoto kubwa katika mjadala huu wa uavyaji mimba ni matumizi ya majina yanayoharibu mahusiano kama vile "anayependelea" na "asiyependelea" -ambayo yamepelekea utofauti unaozunguka suala la uavyaji mimba. Hili pia hupunguza nafasi za utafakari wa suala hili changamano na kuhusiana na wengine kujenga makubaliano. Ni muhimu kwa wataalam wa kiafya kujiepusha na maono hayo ambayo hutenganisha ambayo yanaweza kuathiri kazi yao. Badala yake, ni muhimu sana kwa watoaji huduma za kiafya kujenga mahusiano ya kiheshima na wanaowahudumia kwa kuangazia hali yao ya kiafya bila kuwakosoa kimaadili.

Kuna malengo mawili makuu katika lesoni hii. Kwanza, tutaeleza kuhusu haki za wagonjwa. Pili, tutavifafanua viwango vya kimaadili na kitaalam vinavyowalenga watoaji huduma pale ambapo wanawake wanalenga kupata uavyaji mimba wa njia salama.

2.1) Haki za wagonjwa

Suala la heshima kwa binadamu lilijumuishwa mwanzo katika sheria ya kimataifa chini ya Tangazo la Utambuaji wa Ulimwengu Mzima wa Haki za Kibinadamu mnamo mwaka 1948 Tangazo hili lilikuwa muhimu sana kwa kuwa lilitambua haki za mtu binafsi na kutoa mazingira ya kisheria ya kuboresha utunzaji wa kiafya. Kwa kuegemea msingi huu, maadili kama vile uhuru wa kibinafsi, utu, na usawa wa watu wote ulijumuishwa kwa kiwango kikubwa kwenye taaluma ya huduma za kiafya na suala la haki za wagonjwa hatimaye limeundwa. Baadhi ya haki za wagonjwa zinajumuisha haki ya usiri, habari zao kuwekewa usiri, kukubali au kukataa matibabu, na kufahamishwa kuhusu hatari yoyote inayohusishwa na utaratibu wa kimatibabu wanaopitia.

Pamoja na haki za wagonjwa, ni vyema kuzitambua haki za kingono na za uzazi za kila mmoja. Haki za masuala ya kingono huwalinda watu wote wanapotimiza masuala yao ya kingono na kufurahia afya yao, bila kuhujumiwa, na kuziheshimu haki za wengine.

Kwa mujibu wa ufafanuzi huu, haki kuu zinazohusiana na afya ya uzazi hujumuisha -

 • haki ya kutobaguliwa na usawa
 • haki ya kutoteswa, au kutotendewa unyama au kudunishwa
 • haki ya kuwekewa usiri
 • haki ya kupokea matibabu ya kiwango cha juu (yakijumuisha afya ya uzazi) na usalama wa kijamii.
 • haki ya kuoa/kuolewa na kuanzisha familia kwa makubaliano ya mwenziwe na usawa wakati wa kuivunja ndoa.
 • haki ya kuamua idadi ya watoto mtu anataka na nafasi kati yao.
 • haki ya kupata habari, pamoja na elimu.
 • haki ya kutoa maoni na kujieleza.
 • haki ya kufidiwa na kusaidiwa pale haki zako zimekiukwa.

Ni muhimu kuchukua muda kufikiria kuhusu matumizi ya haki hizi kwa muktadha wa utunzaji wa wagonjwa wa uavyaji mimba, hasa haki zinazohusiana na usawa, usiri, viwango vya juu vya afya, habari na elimu, na idadi ya watoto na nafasi kati yao anaotaka kupata pamoja na haki ya kutodhulumiwa au kutendewa unyama.

2.2) Maadili ya kiafya yanayohusishwa na uavyaji mimba

Katika kuunga mkono haki za wagonjwa, watoaji huduma sharti waongozwe na maadili ya kikazi na kanuni za utendakazi kitaaluma. Hasa udaktari. Wataalam sharti waepuke kusababisha madhara, kuimarisha njia za kutoa usaidizi wa kiafya, kutumia mbinu bora kwa wagonjwa, na kulinda hadhi ya wagonjwa wakati wa matibabu yao. Utafiti wa Biothetics na Taaluma ya Huduma za Kiafya ni muhimu katika kuelewa suala hili kiundani.

Bayothetiki katika taaluma ya udaktari inaegemea kanuni tatu - kanuni ya
1) uhuru wa kujiamulia; 2) faida na kutonyanyaswa na; 3) haki.

Kanuni ya uhuru wa kujiamulia inaweka jukumu la mtoaji huduma kuheshimu haki ya ni matibabu au taratibu gani za kimatibabu wanazopendelea. Uhuru wa kujiamulia pia unampa mgonjwa kuamua ujumuishwaji wa watu wengine kama vile familia au wanajamii katika maamuzi yake ya kimatibabu. Chini ya kanuni ya uhuru wa kujiamulia, watoaji huduma za kiafya wana jukumu la kutoa habari zote muhimu kumsaidia mgonjwa kufanya maamuzi , na sio wao kufanya maamuzi kuhusu ni utunzaji wa aina gani anaopewa mgonjwa.

Faida na kutonyanyaswa huwataka watoaji huduma watathmini pamoja na wagonjwa wao ubora wa aina ya matibabu sawia na hatari zake au hali hatari inayoweza kuleta madhara. Ni muhimu kuwa habari hizi zipewe kwa njia wazi na rahisi kwa mgonjwa kuelewa njia mbalimbali zilizopo na aweze kuchagua njia anayoipendelea zaidi.

Kanuni ya haki katika muktadha wa afya unawataka wahusika wote kuwa na ufikiaji wa huduma za kiafya. Pia, inaelezea kuhusu haki ya mtu binafsi ya kupata kwa usawa manufaa ya kiafya na hatari zinazohusiana na huduma fulani ya kiafya.

Kanuni hizi zinaangaziwa katika uelewa na utekelezaji wa uavyaji mimba. Pamoja, zinahakikisha kuwa viwango vya kitaaluma vya udaktari vinazingatiwa nyakati zote.

Pamoja na hayo, ni muhimu pia kuzingatia utaalam wa utoaji huduma ya kiafya kama mwongozo mkuu katika kueleza na kuongoza jukumu la daktari katika utekelezaji wa uavyaji mimba. Taaluma ya udaktari inaegemea kwenye maadili ya nidhamu, kujitolea na ustadi wa kitaaluma. Katika muktadha wa utunzaji wa wagonjwa wa uavyaji mimba, taaluma ya kiafya inaeleza umuhimu ambao wataalam hawa sharti waelewe, wakubali na kuchukua jukumu la kulinda na kukuza haki za wagonjwa. Taaluma ya udaktari inahitaji kuwa madaktari sharti waepuke kuwashawishi au kutumia kanuni zao za kimaadili, kibinafsi au kidini katika maamuzi yanayomhitaji mgonjwa.

Ufikiaji wa huduma salama za kuavya mimba ni jambo linalobaki kutopewa kipaumbele katika maeneo mengi. Uavyaji mimba usio salama ni tatizo la afya ya umma ambalo hujumuisha ukiukaji wa haki, haki za kibinadamu na usawa wa kijinsia. Kanuni za Kimaadili zinahitaji kuwa, wataalam wa huduma za kiafya wana jukumu la kuitikia dharura la kiafya, hivyo basi, wahudumu sharti waliangazie suala la uavyaji mimba kama la kiafya kabla ya kuwa suala la kisheria. Kupata mimba isiyotarajiwa na kulenga kupata habari na huduma za uavyaji mimba kwa njia salama lazima uchukuliwe kama sehemu ya huduma ya kiafya ambayo madaktari wakubali kuwa kuondoa maradhi na vifo vinavyotokana na uavyaji mimba ambao si salama si uhalifu lakini sehemu ya majukumu yao kama wataalam wa kiafya.

2.3) Kuhakikisha utunzaji wa wagonjwa wa uavyaji mimba kwa njia ya heshima

Njia ambazo wanawake hutafuta na kupokea usaidizi wa uavyaji mimba umeanza kubadilika kwa miaka michache iliyopita. Upatikanaji wa maelezo na habari kuhusu uavyaji kutumia dawa, kuna nyenzo nyingi ambazo wanawake hutafuta habari na kupata utunzaji wa kiafya. Nyenzo hizi mpya, nyingi ambazo ziko nje ya taratibu za kitamaduni ambazo ni -

 • Kufikia vituo vya kiafya (za umma, kibinafsi, ambazo si za serikali)
 • Kupata usaidizi kupitia maduka ya dawa, wauzaji dawa, au maajenti wa kijamii
 • Kupata utunzaji kupitia mitandao na chaneli zingine za mawasiliano (tovuti, nambari za simu, n.k.)
 • Kupata utunzaji kwa njia za kibinafsi kutumia dawa au mbinu zingine.
 • Kufikia utunzaji kupitia njia ambazo hazijaidhinishwa.

Hivyo basi, katika utendaji wako, inawezekana kuwa umehusiana na wanawake katika vitengo mbalimbali katika kutafuta utunzaji, ikijumuisha kulenga kutafuta habari, au kutafuta matibabu wakati wa na baada ya uavyaji mimba.

Ni muhimu kwa madaktari kuangazia haki za wagonjwa wao, za kingono na kibinadamu, na maadili yao ya kibinafsi na taaluma ya udaktari wakati wanahusiana na wanawake wakati wa utaratibu huu. Hakuna mwanamke ambaye anastahili kunyimwa haki yake wakati wowote wa mchakato wa utekelezaji wa uavyaji mimba, kabla, wakati wa, au hata baadaye.

Somo la 3- Anatomia Muhimu, Fiziolojia na Sayansi ya Dawa kwa Uavyaji Mimba

Somo hili litatoa muhtasari wa anatomia fiziolojia na usomi wa dawa muhimu kwenye uavyaji mimba wa kutumia dawa. Maelezo na habari kwenye somo hili yataongezewa habari na maelezo kutoka kwa mafunzo rasmi ya udaktari.

3.1) Anatomia Muhimu ya Uzazi

Sehemu za uzazi za mwanamke zinaweza kugawika kuwili- sehemu za ndani na sehemu za nje. Sehemu za uzazi za nje zinapatikana nje ya mfupa wa nyonga na hujumuisha- sehemu kati ya njia ya uzazi na mkundu, kinembe, midomo ya njia ya uzazi, tezi za vestibula, na sehemu za kupitishia mkojo. Kwa upande mwingine, sehemu za uzazi za ndani ni sehemu ambazo ziko ndani ya fupanyonga. Hizi zinajumuisha kuma, nyumba ya uzazi, mlango wa kizazi, tubu za kupitisha mayai ya uzazi, na ovari. Wacha tuziangalie sehemu za ndani za uzazi kwa undani.

 • Nyumba ya uzazi - Nyumba ya uzazi ni sehemu ya uzazi yenye umbo la pea lililogeuzwa chini yenye misuli na inayopatikana kati ya kibofu na rektamu. Ukuta wa nyumba ya uzazi una safu tatu. Safu ya juu zaidi inaitwa utando wa majimaji au perimetriamu ambao una tishu ya epithelia ambayo hufunika sehemu ya nje ya nyumba ya uzazi. Safu ya kati, inayoitwa miometriamu, ni safu nzito yenye misuli inayowezesha nyumba ya uzazi kujivuta. Nyumba ya uzazi kwa kiwango kikubwa ni tishu ya miyometriamu. Misuli kwenye tishu hii imepangika kutoka juu kwenda chini, kushoto kwenda kulia na kutoka pembe hadi pembe, ili kuruhusu misuli kujibana kwa nguvu wakati wa mama kujifungua na kuhakikisha haijibani sana wakati wa hedhi na kuondoa mimba wakati wa uavyaji sawia na kusimamisha ufujaji wa damu baada ya uavyaji au kujifungua. Zaidi, ujivutaji/ujibanaji wa miyometriamu ni chanzo kikuu cha maumivu yanayohisiwa wakati wa kuavya mimba. Hatimaye, safu ya ndani zaidi ya nyumba ya uzazi inaitwa endometriamu. Endometriamu inajumuisha tishu inayounganisha na ambayo imefunikwa na tishu ya epithelia ambayo iko juu ya lumeni. Nyumba ya uzazi ina sehemu mbili- sehemu zisizo na uwezo za mlango wa uzazi, na sehemu kuu ya sehemu hii inaitwa mwili wa nyumba ya uzazi, au corpus uteri. Mwili wa nyumba ya uzazi una umbo la mviringo na unapatikana juu ya kuma kwa 90º. Sehemu ya juu ya nyumba ya uzazi imejipinda na huitwa fundus; ni sehemu yenye misuli zaidi kwenye nyumba ya uzazi. Fundus inaweza kutambuliwa kwa kuweka mkono kwenye sehemu ya chini ya tumbo wakati wa utathmini wa ukubwa wa nyumba ya uzazi. Mwili wa nyumba ya uzazi hata hivyo una jukumu la kubeba mimba.
 • Mlango wa nyumba ya uzazi - Mlango huu una misuli na una umbo la kimviringo ambapo kuna njia katikati. Njia hii huunganisha sehemu ya ndani ya nyumba ya uzazi na njia ya uzazi. Sehemu wazi ya nje kuingia kwenye njia ya uzazi inaitwa os ya nje, na njia ya ndani ya kuingia kwenye nyumba ya uzazi huitwa os ya ndani. Os ya nje ni sehemu ya mlango wa uzazi wa kike ambayo hupanuka kuruhusu mtoto kutoka wakati wa kujifungua. Ukubwa wa wastani wa mlango wa uzazi ni sentimita 3-5. Mlango wa uzazi una neva za parasympathetic kutoka kwa sehemu za karibu na fupanyonga ambazo jubeba nyuzi za maumivu. Hivyo, ni muhimu kubaini kuwa mlango wa uzazi huwa na uwezo mkubwa wa kutambua maumivu, na hubadilisha mlango wa uzazi, na mabadiliko yoyote kwake, hasa wakati wa kuavya mimba yanaweza kuwa chanzo cha maumivu.
 • Tubu za kusafirisha mayai ya uzazi (tubu za falopia) - Tubu hizi hupatikana kwenye sehemu ya juu na zimeenea kuwili. Jukumu lake kuu ni kusafirisha manii kuelekea kwa yai la uzazi la kike, ambalo huachiliwa na ovari, na pia kuruhusu upitaji wa yai lililotungishwa mimba kurundi kwenye nyumba ya uzazi kulelewa. Kila tubu ina urefu wa sentimita 10 na upana wa sentimita 1 na hupatikana kwenye sehemu inayoitwa mesosalipinks. Kila tubu ya falopia ina sehemu tatu - Ya kwanza, iliyo karibu sana na nyumba ya uzazi inaitwa istimasi (shingo). Sehemu ya pili inaitwa ampula, ambayo hupanuka zaidi kwa upana na ni sehemu ambapo yai hukutana na manii ya kiume ili mimba kutungika. Sehemu ya mwisho na ambayo iko mbali na nyumba ya uzazi inaitwa infundibalam. Infundibalam ina maungo yafananayo vidole ambayo yana jukumu la kulikamata yao wakati linapoachiliwa kutoka kwa ovaro. Sehemu hii ni muhimu kwa kuwa inaunganisha utupu wa nyumba ya uzazi na utupu wa peritonia ambapo mimba ya ektopia hufanyika.

Fiziolojia Muhimu ya Uzazi -

Sehemu hii inaweka wazi mambo muhimu kuhusu mfumo wa mzunguko wa hedhi, fiziolojia ya mimba ya mapema na homoni muhimu katika ukuaji wa mimba.

Mfumo wa hedhi unamaanisha mabadiliko yanayofanyika kwenye mwili, hasa kwenye ovari na nyumba ya uzazi kutokana na mabadiliko ya kiwango na usawazishaji wa homoni mbalimbali za kike. Mfumo wa hedhi unathibitiwa na homoni zanazotoka kwa haipothalamasi, tezi za pituitari na ovari. Mwanzo wa mzunguko huu au mfumo huu huanza wakati wa kubalehe na huendelea hadi pale mwanamke anakoma hedhi. Kila mwanamke amezaliwa na idadi fulani ya mayai ya uzazi ambapo kila moja huachiliwa kwa kila mzunguko wa hedhi kutoka anapobalehe hadi kukoma hedhi. Muda wa kupata hedhi hubadili kutoka mwanamke hadi mwingine au hata kwa mwanamke mmoja, huja wakati tofauti kutokana na vigezo vya ndani kama viwango vya homoni, au hata vigezo vya nje kama vile mawazo.

Mfumo wa hedhi huanza na siku ya kwanza ya hedhi. Urefu wa mzunguko wa hedhi hubainishwa kwa kuhesabu siku ya kwanza ya kuona damu kwa mizunguko miwili inayofuatana. Kwa kuwa muda wa mzunguko wa hedhi ni siku 28, huu ndio muda unaotumiwa kubaini matukio kwenye mzunguko. Hata hivyo, urefu wa mzunguko wa hedhi hubadilika kutok akwa mwanamke mmoja hadi mwingine, na hata kwa mwanamke mmoja kutoka mzunguko mmoja hadi mwingine, sanasana kutoka siku 21-32. Mzunguko wa hedhi una awamu tatu zifuatazo -

1) Awamu ya kuona damu - Awamu hii ya mzunguko wa hedhi ni wakati ambapo sehemu ya juu ya ndani ya nyumba ya uzazi hung’oka; hivyo basi ni wakati mwanamke huona damu. Kwa wastani, huchukua siku tano, lakini huweza kuchukua kati ya siku 2-7, au zaidi. Awamu hii hufanyika kutokana na kupunguka kwa homoni za projesteroni kwenye mwili. Kupunguka kwa projesteroni husababisha kung’oka kwa sehemu ya juu ya ndani ya nyumba ya uzazi na hufikisha mwisho awamu ya lutiamu.

2) Awamu ya ukuaji wa mayai - Awamu hii ni pale ambapo mayai yauzazi ya kike hukua na kukomaa kabla ya kuachililiwa. Pituitari ya ndani hutoa FSH na LH, ambazo hufanya kazi moja kwa moja kwa seli za kinyweleo. FSH husisimua seli za kinyweleo kukua na kutoa estrojeni. Homoni hizi pia ukuaji wa tishu za endometria (ambazo hukua kwa matayarisho ya kupokea yai lililotungishwa mimba), hubadilisha makamasi ya mlango wa uzazi, na kusisimua vipokezi vya LH kwenye seli za kinyweleo. Chini ya athari ya homoni nyingi, zote isipokuwa moja ya nyeleo hizi zitaacha kukua. Nyweleo ambazo hukua kabisa huitwa Graffian na huwa na yai ambalo litaachiliwa kuelekea tubu ya fallopia.

Karibu siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, viwango vya esterojeni hufika kiwango ambacho hupelekea kutolewa kwa idadi kubwa ya LH, inayojulikana kama LH surge. Uachiliwaji wa LH hulifanya yai kukua haraka na kulifanya kuachiliwa kwenda oocyte ya pili. Hili huitwa uachiliwaji yai la kike.

3) Awamu ya unyaji (Awamu ya utoaji) - Homoni za pituitari ya ndani za FSH na LH husababisha sehemu zilizosalia za kinyweleo cha Graffian kubadilika na kuwa corpus luteum. Corpus luteum hutoa projesteroni, na kwa kiwango kidogo, esterojeni, kwa muda wa hadi siku 12 baada ya yai kuachuliwa. Madhara ya projesteroni ni kuwa inapelekea kunenepa kwa sehemu ya juu ya endometria, mabadiliko kwenye utoaji, na kujiachilia kwa miyometriamu kuzuia ujivutaji ambao unaweza kuathiri upandikizaji wa yai lililotungishwa mimba kwenye nyumba ya uzazi.

Kama utungishaji mimba umefanyika, yai lililotungishwa mimba (zaigoti) hupandikizwa kwenye nyumba ya uzazi na mimba huanza kukua. Trofoblasti huanza kutoa korioniki za kibinadamu (hCG) ambazo huzuia corpus lutem na kuruhusu kutolewa zaidi kwa projesteroni kudumusha mimba. Kazi hii baadaye huchukuliwa na kondo la uzazi. Kama yai halijatungishwa mimba, viwango vya chini vya projesteroni husababisha kung’oka kwa endometriamu, na huitwa hedhi au kuona damu ya hedhi. Hivyo basi, ni muhimu kuwa na viwango vya juu vya projesteroni kutoka kwa corpus luteum na kondo la uzazi (linaloundwa mwanzoni mwa ukuaji wa mimba) kuhakikisha kuendelezwa kwa mimba.

3.2) Utumiaji wa dawa katika uavyaji mimba -

Uavyaji mimba unaokubalika kiafya kwa kutumia dawa kutoka maduka ya dawa umekua ni hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake katika kubadilisha jinsi uavyaji mimba hufanyika. Hata kama idadi ya dawa kama vile gemeprost na methotrexate, yametumika na kutafitiwa katika uavyaji mimba, dawa ambazo zinapendekezwa katika uavyaji mimba ni mifepristone na misoprostol.

Mifepristone - Mifepristone, ambayo pia huitwa RU-486, ni dawa inayopigana na projestin na glucocorticoid na hufanya kazi katika kiwango cha upokezi. Wakati dawa hii inamezwa, inashindana na homoni za projesteroni ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa mimba. Mifepristone hufunga utendakazi wa projesteroni. Hili hupelekea -

 • Kuachana kwa mfuko wa mtoto na ukuta wa nyumba ya uzazi.
 • Kulainika na kupanuka kwa mlango wa nyumba ya uzazi; na
 • Ongezeko la uwezo wa ukuta wa nyumba ya uzazi kujivuta na kufanya kazi kama mwandalizi wa Misoprostol

Uenezwaji muhimu wa dawa mwilini2 -
Kulingana na kazi ambayo dawa imeundiwa kutekeleza, inaweza kukaa dukani wa muda wa miezi 24-48. Mifepristone sharti imezwe huku athari yake ikianza kuonekana baada ya masaa 12-24. Uenezwaji wa Mifepristone kwa mwili huwa kwamba inaingia kwenye damu haraka, na huwa na muda mrefu ndani pale wa saa 25-30 kama kuna mazingira bora kwa matumizi yake na kwa kufuata kiwango kinachofaa cha matumizi.

Baada ya kumezwa na kuvutwa kwenye damu, mifepristone hubalidishwa mwilini na kutengeneza bidhaa za kibayolojia tatu- mono-demethylated, di-demethylated na hydroxylated. Hizi tatu hubaki na uwezo fulani dhidi ya projesteroni ya binadamu na vipokezi vya glucocorticoid vina jukumu la utendakazi kibayolojia wa mifepristone.

Misoprostol - Misoprostol ni dawa ya uwiano wa prostagilandin (Aina ya E1) ambayo mwanzo ilisajiliwa kwa uzuiaji wa vidonda vya tumbo vinavyohusiana na dawa za kupigana na mwasho. Hata hivyo, tangu kuvumbuliwa kwa dawa hii, watumizi wa Misoprostol wametambuliwa katika nyanja ya Ujifunguaji na Afya ya Kizazi cha Kike. Misoprostol inatumika katika nchi nyingi kwa sasa kuanzisha maumivu ya kujifungua, uzuiaji na kutibu uvujaji wa damu, na kutibu mimba ambayo haikutoka kabisa au iliyolazimishwa kutoka. Kufuatia matumizi yake mengi, Misoprostol imejumuishwa kwenye Orodha ya WHO ya Dawa Muhimu kwa Watu Wazima. Inatambuliwa na Tume ya UN kwenye bidhaa za kuokoa maisha kwa wanawake na watoto, hasa katika matumizi yake ya uavyaji mimba ulio salama.

Misoprostol huweza kustahimili viwango vya juu kiasi vya joto (ikilinganisha na Oxytocin) lakini hupoteza uwezo wake kwenye mazingira yenye majimaji mengi kwenye hewa na viwango vya juu sana vya joto. Ni muhimu tembe za misoprostol kuwekwa kwa pakiti zenye karatasi za aluminium mara mbili na kuhifadhiwa kwenye mazingira kavu na yenye viwango vya chini vya joto.

Baada ya kuvutwa kwenye damu, misoprostol hubadilishwa na kuwa asidi ya misoprostol ambayo hupelekea mambo yafuatayo -

 • Husababisha kujivuta sana kwenye nyumba ya uzazi
 • Hulainisha na kupanua mlango wa nyumba ya uzazi, hivyo kurahisisha kutoka kwa mimba.

Uenezwaji muhimu wa dawa mwilini3 -

2Heikinheimo O, Clinical pharmacokinetics of mifepristone , Clinical Pharmacokinetics - 1997 Jul;33(1)-7-17. DOI 10.2165/00003088-199733010-00002
3O.S. Tang et al. misoprostol- Pharmacokinetic profiles, effects on the uterus and side-effects. International Journal of Gynaecology and Obstetrics, 2007 99, S160-167

Misoprostol inaweza kutumiwa kwa njia nyingi kama vile kumezwa, kutiwa chini ya ulimi, kutiwa kati ya shavu na ufizi wa meno au kuingizwa kwenye njia ya uzazi. Ufuatao ni uenezaji na uvutwaji kwenye damu kimuhtasari wa dawa hii kwa njia zilozotajwa -

1) Kumezwa - Baada ya kumezwa, misoprostol huvutwa kwa haraka na karibu yote kwenye damu lakini kwanza hupitishwa na kubadilishwa kuwa asidi ya misoprostol. Kufuatia dozi moja ya 400mcg ya misoprostol, kiwango cha misoprostol kwenye damu huongezeka kwa haraka na hufika juu zaidi kwa dakika 30 na hupunguka kwa haraka kwa dakika 12 na hubakia kiwango cha chini baadaye. Matokeo ni kuwa, kumeza misoprostol hupelekea kujivuta kwa nyumba ya uzazi na si kwa mfuatano wa kawaida ambao ni muhimu kwa uavyaji mimba. Kufuatia mtindo huu wa ujivutaji wa nyumba ya uzazi, njia ya kumeza dawa hii ndiyo inayopendekezwa kama njia ya kutibu uavyaji wa mapema, usio changamano na usiokamilika.

2) Njia ya kuweka kwenye njia ya uzazi - Kufuatia utumiaji dawa kwa njia hii, viwango vya plasma huongezeka na kufika kiwango cha juu kabisa baada ya dakika 70-80, na baadaye kupungua polepole hadi kiwango kinachoweza kutambulika baada ya saa 6. Upatikanaji mrefu wa dawa hii mwilini baada ya kutumiwa unaweza kutumiwa kueleza ni kwa nini matokeo yake ni bora kutumia njia hii.

3) Kutia chini ya ulimi - Ingawa tembe za misoprostol zilitengenezwa ili kumezwa, zinaweza kuchanganyika kwenye maji kwa haraka sana na huweza kuisha kwa dakika 20 baada ya kuwekwa chii ya ulimi. Hii inapelekea kuvutwa kwake kwa haraka kwenye damu na huepuka kupitishwa kwenye ini hivyo basi hufikia upeo wake kwa karibu dakika 30. Njia hii ya kutia chini ya ulimi inachukua muda mchache kwa mwanamke kuanza kuhisi kujivuta kwa nyumba ya uzazi, viwango vya juu zaidi, upatikanaji wa kiwango cha juu, na kuanza kwa haraka kwa matumizi yake. Hata hivyo, uharaka huu unaweza kupelekea madhara mengine ambatano kama vile kibaridi, joto mwilini na kuendesha.

4) Kutia kati ya shavu na ufizi wa chini wa meno - Njia nyingine ya kutumia misoprostol ni kwa kuweka tembe hii kwenye sehemu ya chini kati ya meno na shavu. Ingawa hakuna utafiti wa kuonyesha ubora wa njia hii, bado ni njia inayopendekezwa. Kufutia kutumia dawa hii kwa njia hii, muda unaotumiwa kufikia upeo wake ni sawa na njia ya matumizi kwa kutia kwenye njia ya uzazi.

Hivyo basi, kutegemea njia ya matumizi, wanawake wengi watapokea maumivu sawia na ya hedhi na kutokwa damu baada ya saa 1-2 baada ya dozi ya kwanza ya misoprostol na mimba itatoka baada ya masaa 24 ya kutumia tembe ya mwisho ya misoprostol.

Somo la 4: Utunzaji wa kabla ya uavyaji mimba

Katika somo hili, tutajadili umuhimu wa kuwapima wagonjwa kabla ya kuavya mimba. Pia, tutabainisha malengo makuu ya kupima hali ya afya, na jinsi ya kutimiza haja ya malengo haya kwa njia rahisi na inayoeleweka. Baada ya kumaliza lesoni hii, utakuwa na uwezo wa kueleza umuhimu na malengo ya kupima afya ya wagonjwa wa uavyaji mimba katika utendakazi wako.

4.1) Lengo la kufanya utunzaji wa kabla ya uavyaji mimba

Utunzaji wa kabla ya kuavya mimba ni kumaanisha ushauriano unaostahili kuwepo kati ya daktari na mteja ili kuhakikisha mteja amehitimu kupata huduma ya uavyaji mimba yenye ufuatiliaji wa kiwango cha chini au hata kutokuwepo.

Lengo kuu la utunzaji huu wa kabla ya uavyaji mimba ni kuhakikisha mteja anapata habari mwafaka na dawa sahihi na kuhakikisha kuwa utaratibu wote ni salama, unapunguza hatari ya kuwepo matatizo yoyote na kuimarisha uwezekano wa uavyaji wenye kufanikiwa.

4.2) Malengo ya utunzaji wa kabla ya uavyaji

Malengo makuu ya utunzaji huu yanajumuisha -

 • Kubainisha kuwa mimba ipo na ina umri gani. Hili ni muhimu kwa kuhakikisha utoaji wa kiwango kinachostahili cha dawa ili kupunguza uwezekano wa kutokamilika kwa uavyaji mimba au kuhitilafiana na nyumba ya uzazi.
 • Kutathmini iwapo mgonjwa anastahili kuavya mimba kutumia dawa kama utaratibu wa wagonjwa wanaotembelea hospitali na kubaini matatizo mengine ya kiafya ambayo mwanamke huyo huenda ako nayo kabla ya uavyaji mimba.
 • Kutathmini mahitaji ya uthibiti wa maumivu kwa kila mteja.

Lengo la 1 - Lengo la kwanza la utunzaji wa kabla ya uavyaji mimba ni kubaini kama mimba ipo, iko wapi na ina umri gani.

Kwa nini hili ni muhimu? Ili kubainisha kuhitimu kwa mwanamke kufanya uavyaji kutumia dawa, ni muhimu kwanza kubaini kuwa mwanamke kweli ana mimba, mahali mimba iko na muda ambao mimba imekuwa hapo kuhakikisha kuwa utaratibu lengwa unafanikiwa na ni salama. Uavyaji mimba kutumia misoprostol peke yake au pamoja na mifepristone utafanikiwa kama mimba iko kwenye nyumba ya uzazi. Utumiaji wa kiwango kinachohitajika cha misoprostol kitapunguza uwezekano wa utaratibu utakaofeli kutokana na kiwango cha chini au kusisimuliwa kupita kiasi kwa nyumba ya uzazi unaotokana na kutumia kiwango kinachozidi kwa kulinganisha umri wa mimba yenyewe.

Jinsi ya kuthibitisha kama kunayo mimba - Uthibitishaji huu unaweza kufanywa kutumia moja au kuchanganya njia zifuatazo -

 • Historia na utathmini wa hali ya nje ya mwili - Kuna mambo mengi makuu ya kujifunza kwa kutathmini historia na hali ya kuonekana ya mwili katika kuthibitisha uwepo wa mimba. Ili kutathmini kuwepo kwa mimba vema kabisa na kubaini umri wa mimba, rekodi siku ya mwisho ya mwanamke ya kuona hedhi (LMP), kupata kwake hedhi na mzunguko wa hedhi yake. Ni muhimu kupata habari zaidi kutoka kwa mgonjwa ambazo huenda zikakuchanganya katika kubaini mimba ya mapema kama vile kuchelewa kwa hedhi, matumizi ya dawa za kupanga uzazi au historia ya hedhi ambazo hazina wakati maalum.
  Dalili zingine kama vile kuhisi kutapika, kulainika na kuvimba kwa matiti, na uchovu kunaweza kusaidia katika kubainisha kama mimba ipo.
  Dalili zaidi zinaweza kusaidia katika kupata umri wa mimba iwapo utathmini wa njia ya uzazi utafanywa. Dalili ya Hegar inathibitika kwa kulainika kwa kunenepa kwa mlango wa uzazi na unaweza kutambulika baada ya wiki sita. Dalili ya Chadwick inatambulika kwa kuwepo kwa unyevu wa rangi ya samawati na unaweza kutambuliwa kati ya wiki 8-10.
 • Kupima mimba - Kupima mimba ni mbinu ya kubaini kama mwanamke ana mimba au la. Njia nyingi zilizopo za kupima mimba ni zile za kupima kiwango cha hCG na vipengee vinavyohusiana, kwa mkojo au kwenye damu. Upimaji mwingi uliopo unalenga kubaini kitengo kidogo cha beta cha hCG ambacho huimarisha usahihi wa matokeo na hupunguza uwezekano wa matokeo chanya ambayo si ya kweli. Upimaji wa kutambua kitengo kidogo cha beta cha hCG kinaweza kufanywa kwa kutumia sampuli ya damu au mkojo.
  Sampuli za mkojo zinapatikana kwa urahisi katika maduka mengi ya dawa na hurejelewa kama upimaji mimba. Ni rahisi kubaini viwango vya chini vya hCG kutoka 20 hadi 100 mIU/mL. Kwa kawaida huwa ni siku 7-10 baada ya kukosa hedhi. Inapendekezwa kuwa wanawake watumie sampuli ya mkojo ya asubuhi na waepuke mkojo wenye maji kuepuka uwezekano wa kupata matokeo hasi katika mimba changa.
  Sampuli za damu zinaweza kutumika kama njia mbadala ya mkojo. Sampuli za damu hugharibu pesa nyingi kiasi na vifaa vya maabara kupima mimba. Upimaji huu hukadiria kiwango cha hCG kwenye damu na zinaweza kutambua viwango vya chini kama 5 mIU/mL. Ubora wa upimaji huu ni kuwa unakadiria kiwango cha hCG kwenye damu, ambacho kinaweza kubaini umri wa mimba pia (kwenye mimba ya mtoto mmoja). Upimaji zaidi unaweza kutumika kubaini hali zingine kama vile mimba ya zaidi ya mapacha, mimba iliyo kwenye tubu la falopia, na ugonjwa wa trophoblastic.

Jinsi ya kubaini eneo ilipo mimba -
Ukaguzi kuwili kutumia mikono kupitia kwenye njia ya uzazi na unaoonyesha dalili ya mimba sawia na ukubwa wa nyumba ya uzazi unatosha kubaini mimba iliyo kwenye nyumba ya uzazi. Ni muhimu kuhakikisha hakuna dalili za kuonyesha kuwa mimba ipo kwenye tubu ya falopia. Dalili za mimba kwenye tubu ni pamoja na tofauti kati ya LMP na ukubwa wa nyumba ya uzazi, kuwepo kwa sehemu laini kwenye kuta za njia ya uzazi na ulaini kwenye pochi ya Douglas.

Njia sahihi kabisa ya moja kwa moja ya kubaini aina hii ya mimba ni kupitia upigaji picha (ultra sonogra). Ultra sonogram sharti uwe kupitia njia ya uzazi kama kuna amenorrhea ya chiniya wiki 6 au kupitia sehemu ya chini ya tumbo kama amenorrhea inazidi wiki 6.

Kutokana na matukio machache ya mimba kwenye tubu ya fallopia, hakuna matumizi ya mara kwa mara ya sonogramu katika uavyaji mimba changa. Upigaji picha utatumika tu kama kuna kisio la kitaalam la kuwepo kwa mimba kwenye tubu ya falopia, ama iwapo kuna shaka kuhusu umri wa mimba.

Kumbuka - Matumizi ya pamoja ya viwango vya chorionic gonadotropin ya binadamu (hCG) nyumba ya uzazi tupu kupitia picha, maumivu ya tumbo, na utoaji damu kupitia njia ya uzazi ni ishara ya mimba iliyoko kwenye tubu ya fallopia. Dawa za kuavya mimba hazitoshi katika kutoa mimba iliyo kwenye tubu ya fallopia. Haya ndiyo masuala yanayochangia vifo vya wanawake katika miezi mitatu ya kupata mimba na sharti yabainishwe mapema.

Jinsi ya kubaini umri wa mimba -
Umri wa mimba au muda imekuwepo ni kupitia mbinu moja au zaidi ya moja ya zifuatazo-

 • Muulize mwanamke kukufahamisha siku ya kwanza yake ya kupata hedhi ya mwisho (LMP) na kupiga hesabu ya idadi ya majuma kutoka kwa LPM hadi siku ambapo dawa hizi zitatumika kutumia kalenda. Utafiti unaonyesha kuwa kutumia LMP kubaini muda wa mimba huwa sahihi na unaokubalika. Pia, kwa mara nyingi, wanawake wanaweza kukumbuka LMP kwa usahihi.
 • Tathmini sehemu ya fupanyonga (sehemu ya uzazi) kutumia mikono miwili kubaini ukubwa wa nyumba ya uzazi. Kama ukubwa wa nyumba ya uzazi unawiana na tarehe inayotokana na LMP, hiyo inatosha kubaini umri wa mimba kabla ya uavyaji mimba.
 • Kutumia upigaji picha pia kunaweza kubainisha umri wa mimba.

Hakikisha kuwa mimba haijazidi majuma 10 kwa mujibu wa hesabu yako. Kama mimba ina chini ya majuma 10, unaweza kutumia dawa kuiavya kama ilivyoelekezwa kwenye lesoni ya 5.

Iwapo mimba ina uwezekano wa kuwa zaidi ya majuma 10, basi usimpe dawa za kuavya mimba kama inavyoelezwa chini ya lesoni ya 5. Utahitajika kubadilisha kiwango cha dwa ya misoprostol kwa kukadiria umri wa mimba na mwanamke anaweza kuhitaji msaada zaidi na/au usimamizi wa jinsi anavyotumia dawa.

Lengo la 2 - Tathmini kuhitimu kwa mwanamke kwa uavyaji wa kutumia dawa na pima viashiria ambavyo huenda vikahitilafiana na dawa za uavyaji mimba.

Kama dawa zote zile, mifepristone na misoprostol zina vitu vya kutathmini kabla ya kumpa mgonjwa kama vile, mizio kwa mifepristone, misoprostol au viungo vingine, au kama mwanamke ana hali zingine za kiafya ambazo haziruhusu matumizi ya aina hii ya dawa.

Viashiria vya kutowiana na dawa ya Mifepristone hujumuisha -

 • Matibabu ya muda mrefu na yanayoendelea ya kimfumo ya corticosteroid
 • Matatizo yanayohusiana na kufeli kwa adrenali
 • Ugonjwa wa Porphyrias uliorithiwa.
 • Matatizo yanayohusiana na damu
 • Matibabu yanayoendelea ya ugandaji wa damu, na
 • Mizio kwa mifepristone au mwili kuikataa.

Viashiria vya kutowiana na dawa ya Misoprostol hujumuisha -

 • Mizio kwa misoprostol au viungo vingine vya dawa hii.

Pale ambapo mwanamke ana viashiria vya kutoendana vema na dawa ya Miferipristone, matumizi ya Misoprostol yanaweza kutumiwa iwapo tu hamna kutoelewana kwa mwili na matumizi ya Misoprostol.

Huku kuwepo kwa tatizo lolote la utokwaji damu ni ishara ya kutotumia dawa ya kuavya mimba, matumizi ya viwango vya chini vya asprini au klopidrojeli si ishara ya kutotumika kwa dawa ya uavyaji mimba. Huku pia hakuna utafiti wa karibuni unaoonyesha hatari ya kutokwa na damu katika matibabu yoyote kwa wanawake wanaofanya uavyaji mimba, kijumla, matumizi ya kiwango cha chini cha asprin hayaongezi utokaji damu au kupelekea kifo cha mwanamke. Hata hivyo, iwapo mteja anatumia kiwango cha chini cha asprin na clopidrogel, sharti hali yao ya kiafya ipimwe kabla ya kumpa dawa ya kuavya mimba.4.

Ueneaji wa porphyrias unatofautiana miongoni mwa makundi tofauti ya watu na ni vigumu kupima watu mahali hakijakuwa na historia yake. Hata katika vituo vya afya, hali hii inaweza kupimwa kinyumenyume kwa kufuata utoaji wa dawa. Basi, fahamu hili na umweleze mgonjwa kuwa kuna uwezekano wa madhara mengine yanayotokana na matumizi ya dawa za uavyaji mimba.

Pia, ni muhimu kufahamu kuwa kuna hali zingine nyingi za kiafya ambazo zitalazimisha mteja kuwa chini ya uangalizi kutumia dawa au usaidizi wakai wa uavyaji mimba.

Hali za kiafya ambazo zimedhibitiwa kama vile shinikizo la damu, kisukari au pumu ni kawaida, na uavyaji mimba wa mapema unaweza kusimamiwa vema bila mgonjwa kulazwa hospitalini. Mara chache, hali za afya zilizokuwepo zinalazimu mgonjwa kutumwa hospitalini kwa utunzaji wa uavyaji mimba. Hali hizi zinajumuisha magonjwa hatari ambayo hayajadhibitiwa kama vile shinikizo la damu, kisukari, pumu au hali ya afya ambayo ni changamano inayohisisha mfumo wa neva, endokrine, palmona na matatizo ya moyo.

Pia ni muhimu kukumbuka kuwa dawa za kutibu kifafa, kifua kikuu na dawa za kupunguza makali ya Ukimwi zinaweza kupunguza ufanikifu wa mifepristone kama zinatumiwa kila wakati. Haya yanastahili kutiliwa maanani wakati wa kutekeleza uavyaji mimba kutumia dawa.

Lengo la 3 - Kutathmini mahitaji ya kuthibiti maumivu kwa wagonjwa-
Kama ilivyoelezwa katika lesoni ya 3, vyanzo vya maumivu wakati wa uavyaji mimba kutumia dawa huwa ni maumivu yanayohusiana na hedhi na kujivuta kwa nyumba ya uzazi na wakati wa kutoa mimba kupitia mlango wa uzazi. Viwango vya maumivu ambavyo wanawake hupitia huwa tofauti kutegemea vigezo mbalimbali kama vile umri wa mimba, ustahimili wa maumivu, viwango vya wasiwasi, na viwango vya utulivu wakati wa kupitia utaratibu huu. Dawa za maumivu sharti zipewe kwa wanawake wote wanaopitia uavyaji mimba wa kutumia dawa au upasuaji bila kuchelewa. Kila mwanamke atathminiwe kibinafsi kwa kuangazia hitaji lake la udhibiti wa maumivu yake. Ni muhimu kutumia njia zingine zisizokuwa za kutumia dawa katika kupunguza maumivu na wasiwasi. Hizi ni pamoja na maandalizi ya kutosha kabla ya kufanya uavyaji kutumia dawa, kuwa katika eneo salama, kuvaa ngua nzuri, ukaribu na usaidizi kwa kisaikolojia, matumizi ya chupa zenye maji moto kwenye sehemu ya chini ya tumbo wakati wa uavyaji mimba. Maelezo zaidi kuhusu udhibiti na usimamizi wa maumivu wakati wa uavyaji mimba kutumia dawa yametolewa kwenye lesoni ya 6.

Somo la 5: Dawa za Uavyaji Mimba na matumizi yake

Katika somo hili, tutajadili vigezo muhimu vya kutathmini wakati wa kutoa na kutumia dawa za kuavya mimba. Mwisho wa sehemu hii, utakuwa na uwezo wa kutambua kwa usahihi dawa za uavyaji mimba, viwango vyao, muda wa matumizi na njia ya kuzitumia kwa uavyaji mimba iliyo chini ya majuma 10.

Baada ya hatua ya kumpima na kutathmini mgonjwa, utakuwa umetambua umri wa mimba, na kubaini kuwa mteja amehitimu kufanya uavyaji kutumia dawa. Kwa kuangazia hali ilivyo na upatikanaji wa dawa, kuna chaguzi mbili kuhusiana na uavyaji mimba kutumia dawa -

Chaguo la 1- kutumia pamoja dawa ya mifepristone kufuatiwa na misoprostol

Chaguo la 2- kutumia misoprostol tu kwa kurudia

Pale ambapo chaguo zote mbili zipo, habari kuhusiana na utendakazi wake sharti yapewe mteja pamoja na gharama yake ili wao wachague njia gani wanayoipendelea. Jedwali lifuatalo linatoa ulinganifu baina ya mbinu hizi mbili.

Mifepriston na misoprostol Matumizi ya Misoprostol tu
Huwa na matokeo yanayotarajiwa ya asilimia 95-99 ikitumika chini ya majuma 10 ya ujauzito, huku ufanikifu wake ukiegemea pia njia ilivyotumika. Ina matokeo mazuri kwa asilimia 75-90
Hatari kwamba mimba itaendelea kukua na kuwa na madhara makubwa ni ya chini mno (<1%) Hatari ya mimba kuendelea kukua baada ya kuitumia dawa hii ni karibu asilimia 5-10.
Ni ghali zaidi kwa kuwa aina mbili ya dawa inatumika. Haina gharama kubwa sana.

5.1) Jinsi ya Kutumia Tembe za Uavyaji Mimba - mifepristone + misoprostol

Wakati wa kutoa dawa ya mifepristone na misoprostol, hakikisha kuwa dawa kwa ukamilifu wake inapatikana kwa mteja. Ni vema sana mteja kuwa na dawa zote kabla ya kutumia dosi ya kwanza ili kuhakikisha utaratibu wote unafanikiwa.

Mgonjwa anastahili kupata tembe moja ya 200mg ya mifepristone na tembe nne za 200mcg za misoprostol pamoja na maelezo yafuatayo -

Hatua ya 1 - Meza tembe moja ya Mifepristone (200mg) kutumia maji. Wanawake wengine (hadi asilimia 40) wanaweza kuhisi kichefuchefu baada ya kumeza tembe ya mifepristone. Iwapo atatapika kabla ya saa moja kuisha baada ya kumeza tembe ya mifepristone, kuna uwezekano wa kutofanya kazi na anatakiwa kumeza tembe nyingine. Iwapo mteja atatapika baada ya saa moja ya kuimeza tembe ya Mifepristone, dawa ya kutosha itakuwa imevutwa kenye damu kufanikisha uavyaji na hastahili kumeza nyingine.

Hatua ya 2 - Subiri kwa masaa 24-48. Ni lazima umweleze mteja kusubiri masaa 24 kabla ya kumeza Misoprostol, lakini asisubiri zaidi ya masaa 48. Huku mteja akisubiri, anaweza kuendelea na kazi yake nyingine kama vile kuwatunza watoto au kuenda kazi au shule. Chini ya silimia 10 ya wanawake hutokwa na damu au kupata maumivu sawia na ya hedhi baada ya kutumia Mifepristone.

Hatua ya 3 - Baada ya saa 24 na kabla ya saa 48 kwisha, kunywa maji kiasi na kuhakikisha kinywa chako kina majimaji. Tia tembe 4 za Misoprostol (kila moja ina 200mcg) kati ya shavu na ufizi wa meno (tembe 2 kwa kila upande), au zote chini ya ulimi.

Hatua ya 4 - Hakikisha tembe hizo zinasalia pale kwa muda wa dakika 30. Tembe hizi zinaweza kukifanya kinywa kukauka kidogo au kuwa na ladha ya kichaki wakati zinayeyushwa. Usinywe au kula kitu wakati huu wa dakika 30. Meza mate au majimaji yoyote kinywani mwako na usiteme kitu wakati wa dakika hizi 30.

Hatua ya 5 - Baada ya dakika 30, safisha kinywa chako kwa maji safi na umeze kila kitu kilichosalia mdomoni.

5.2) Jinsi ya Kutumia Tembe za Uavyaji Mimba - Misoprostol Tu

Wakati unampa mteja dawa ya misoprostol tu, hakikisha dawa ipo kwa kiwango kinachohitajika. Kwa kuwa ni vigumu kubaini ni mwanamke yupi atahitaji dozi zaidi ya dawa na kwa wakati gani, kutoa kiwango chini ya dozi kamili huenda ikapunguza uwezekano wa kupata matokeo bora na kuzua madhara mengine.

Hakikisha kuwa kuna tembe 12 za 200mcg anazopewa mteja na kuwa kuna maelezo yanayohitajika. Wakati wa kumwelekeza mteja jinsi ya kutumia tembe hizi, mweleze kuwa anahitaji kutoa tembe nje ya karatasi yake wakati tu anataka kuitumia na si mapema. Tembe zingine zibakie kwenye karatasi zilivyopakiwa hadi wakati wa matumizi.

Maelezo ya matumizi ya misoprostol tu ni kama yafuatayo -

Hatua ya 1 - Kunywa maji kidogo kukifanya kinywa chako kuwa majimaji. Weka tembe 4 chini ya ulimi na kuziacha kuyeyuka. Zishikilie chini ya ulimi kwa dakika 30. Zinaweza kukifanya kinywa kukauka au kuwa na ladha ya kichaki. Usile au kunywa kitu kwa dakika hizi 30. Meza mate au majimaji yoyote kinywani mwako na usiteme kitu wakati wa dakika hizi 30.

Baada ya dakika hizi 30, safisha kinywa chako kwa maji safi na umeze mabaki yote ya tembe yaliyosalia kinywani

Subiri masaa 3-4 kabla ya kuendelea.

Hatua ya 2 - Baada ya masaa 3-4, hata kama umeanza kuhisi uchungu kama wa hedhi na kuanza kutokwa na damu, rudia Hatua ya 1 kwa tembe zingine 4.

Wait 3-4 hours after completing Step 2.

Hatua ya 3 - Baada ya masaa mengine 3-4 (hivyo ni kusema masaa 6-8 ya kumeza tembe za kwanza za Misoprostol), rudia Hatua ya 1 Kwa tembe 4 za mwisho. Hakikisha kuwa umekamilisha Hatua ya 3 hata kama una maumivu makali na kutokwa na damu na kuona uavyaji ukifanyika.

Somo la 6: Kozi ya Kikliniki - Uavyaji Mimba kutumia dawa

Katika somo hili, tutajadili huduma zaidi inayoweza kutolewa kwa wanawake wanaopitia utaratibu wa uavyaji mimba kutumia dawa. Maelezo ya sehemu hii yatakusaidia kuwasaidia wagonjwa katika kuangazia madhara yanayotarajiwa na yasiyopendeza ya uavyaji mimba, na kuimarisha utoshekaji wa wateja wanaohitaji huduma hii.

Zaidi ya kutoa tu dawa za kuavya mimba, kuna juhudi zingine ambazo unaweza kufanya kama daktari kuhakikisha kuwa kuna matokeo mazuri na kutosheka kwa wagonjwa wanaopitia utaratibu huu. Juhudi hizi ni muhimu kuhakikisha kuwa unatoa huduma ya hali ya juu na hupelekea kutosheka kwa wateja.

6.1) Madhara yanayotarajiwa na ushughulikiaji wayo

Dalili moja ya kawaida ambayo huonekana wakati wa uavyaji mimba ni maumivu na kutokwa na damu. Dalili hizi zinatarajiwa katika utaratibu huu. Ni bora iwapo wanawake wote watafahamishwa kuhusu dalili hii na kupewa usaidizi wa kutosha na utunzaji wa kabla ili kuelewa jinsi ya kushughulikia hali hii.

Wanawake wengine wanaweza kupata madhara mengine ambayo si mazuri sana ambayo yanaweza kuathiri mtazamo wao kuhusu uavyaji mimba. Ni vema iwapo wanawake wote watazielewa dalili zinazotarajiwa na ambazo ni muhimu ili uavyaji ukamilike, na madhara mengine ambayo yanaweza kushuhudiwa baada ya kutumia dawa za uavyaji mimba.

Huku madhara marefu au mabaya hayaripotiwi sana, madhara madogomadogo machache yanaweza kushuhudiwa. Kwa wanawake wengi madhara haya hupotea baada ya masaa 4 hadi 6 ya kutumia misoprostol. Hakuna madhara ya muda mrefu ya matumizi ya dawa za uavyaji mimba.

Utunzaji huu unalenga kuangazia dalili na madhara ya matumizi ya dawa hizi na kuwasaidia wagonjwa kuhisi salama na bila wasiwasi.

Kushughulikia dalili zinazotarajiwa

Kabla ya kuanza utaratibu wa kuavya mimba, hakikisha kuwa mwanamkw anajua -

 • Asiwe na wasiwasi iwapo atapata maumivu na utokwaji wa damu zaidi ya kawaida.
 • Anaweza kunywa na kula anavyotaka baada ya kumaliza kutumia dawa.
 • Ajaribu kukaa mahali ambapo anahisi ni salama na bila wasiwasi hadi ahisi vema.
 • Ayafahamu madhara yanayoambatana na matumizi ya dawa hizi na maonyo yake.
 • Unaweza kumpa dawa na kumweleza jinsi ya kushughulikia madhara, lakini pia awe kwamba ameutafakari uamuzi wake na jinsi atakavyopata usaidizi wa kiafya wa dharura iwapo utahitajika.
 • Wanawake wengi hurejea kwa hali ya kawaida chini ya masaa 24.

Ni muhimu kumfahamisha mwanamke kuwa mengi ya madhara yanahusiana na misoprostol na sharti afanye mpango wa kuwa katika mahali salama, bila wasiwasi na binafsi kabla ya kutumia misoprostol.

Dalili zinazotarajiwa-

Maumivu sawia na ya hedhi
Wanawake wengi hupata maumivu baada ya dakika 30 za matumizi ya misoprostol. Maumivu sawia na ya hedhi ni ishara kuwa nyumba ya uzazi imeanza kujivuta na iko kwenye harakati za kutoa mimba iliyomo. Hii ni dalili kwamba dawa inafanya kazi. Kiwango cha maumivu huwa tofauti kwa watu tofauti. Ni sawa na wakati wa kujifungua ambapo wanawake huwa na maumivu wa muda usiotoshana.

Utokwaji wa damu
Wanawake wengi watatokwa na damu inayofanana kwa karibu na ile ya hedhi. Huku chini ya silimia 10 ya wanawake watatokwa na damu baada ya kutumia mifepristone, wanawake wengi wataanza kutokwa na damu baada ya kutumia dozi ya kwanza ya misoprostol Baada ya kuanza, utokwaji damu unaweza kuendelea kwa saa kadhaa. Wanawake wanaweza kuona damu iliyoganda na nzito wakati huu na wanashauriwa kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa ni kawaida na mimba inatoka.

Kiwango cha damu pia hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine na huhusishwa na umri wa mimba pia. Kwa wanawake wengi, utokwaji damu utapungua baada ya saa 1-2 baada ya utokaji wa bidhaa zote za ujauzito na utaendelea kwa juma 1-2 huku ukiendelea kupungua. Wanawake wengine hutokwa na damu hadi majuma manne baada ya kutumia dawa za uavyaji mimba.

Dalili hizi zote ni muhimu kwa sababu huonyesha kuwa dawa inafanya kazi. Ili kupunguza maumivu wakati wa utaratibu huu, wanawake wanastahili kupewa dawa za maumivu.

Ili kupunguza maumivu wakati wa uavyaji mimba-

 • Toa ushauri wa kijumla wa njia ambazo si za kutumia dawa ili kupunguza maumivu na wasiwasi, kama vile kuwa katika eneo salama, kusikiliza muziki, kujiepusha na kazi nzito, na kutumia chupa zenye maji moto kwenye sehemu ya chini ya tumbo (sawia na wakati wa hedhi)
 • Wape dawa za maumivu wanawake wanaopitia uavyaji mimba. Kwa kawaida, hizi hutolewa pamoja na mefipristone na misoprostol.
 • Kutumia dawa ambazo hazihitilafiani na homoni za uzazi na zinazopunguza mwasho (NSAIDS) kama vile Ibuprofen or Diclofenac ambazo husaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa maumivu wakati wa uavyaji mimba. Dozi inayopendekezwa ya dawa za NSAIDS ni -
  • Ibuprofen - 400-800 mg kwa kila masaa 6-8 na si zaidi ya dozi ya 3200mg kwa saa 24.
  • Diclofenac Sodium - 50 mg kwa kila masaa 12 na si zaidi ya dozi ya 150mg kwa saa 24.
 • Hakikisha kuwa dawa za kumezwa za maumivu ndizo zitakazokuwa na matokeo mema na kupendekeza watumie baada ya dakika 30-45 za kutumia dozi ya misoprostol. Wanawake washauriwe kutumia dawa za maumivu mapema kabla ya kuenda kwa kazi zao. Wasisubiri hadi pale maumivu ni makali sana ndipo wameze dawa za maumivu.
 • Fahamu kwamba acetaminophen (au paracetamol), wakati inamezwa haisaidii katika kupunguza maumivu wakati wa uavyaji mimba na isitumike.

6.2) Madhara na jinsi ya kuyashughulikia

Kwa kuongezea kwa madhara yanayotarajiwa ya dawa za uavyaji mimba, misoprostol inaweza kuwa na madhara ambayo si mazuri sana. Ukali wa madhara yenyewe hutegemea njia ya matumizi ya misoprostol. Matumizi kwa njia ya kutiwa chini ya ulimi huhusishwa na madhara mengi yanayoripotiwa. Hivyo basi, ni muhimu kuwasaidia wanawake kuangazia madhara haya ili kupunguza wasiwasi.

Kichefuchefu na kutapika

Kichefuchefu, ulegevu na kutapika huenda vikawapata wananwake wengine na vitaisha baada ya masaa 2 hadi 6 baada ya kutumia misoprostol. Wakati mwingine, kichefuchefu kinachohusiana na ujauzito kinaweza kuwa kibaya sana au kuchanganyisha na kile kinachosababishwa na utumizi wa misoprostol. Hili linaweza kuwatia wasiwasi wanawake na huenda kikasababisha kutapika na kupoteza maji mwilini. Hali hii huisha baada ya uavyaji kukamilika na dawa ya misoprostol kutoweka kwenye mwili.

Mpe mteja ushauri wa kumsaidia kama vile kula vyakula visivyo vya majimaji ili kupunguza kichefuchefu. Dawa zaidi kama vile Domperidone, Onadansetron na Metaclopromide zinaweza kupewa mwanamke kushughulikia madhara haya kama hamna pingmizi za kiafya za matumizi yao.

Unyonge/Ulegevu -

Karibu asilimia 20 ya wanawake wanaotumia misoprostol wanapata ulegevu ambao mara nyingi hauelezeki vizuri. Kuhakikisha kuwa wanawake wamekula na wamepumzika husaidia kushughulikia madhara haya. Kama yalivyo madhara mengine, mteja anaweza kudhibiti hali hii na hakuna dawa zinazopendekezwa.

Maumivu ya tumbo na kuendesha -

Hadi asilimia 40 ya wanawake hupata kuendesha kidogo. Kutumia misoprostol pamoja na chakula kunaweza kusaidia kiasi kupunguza kuendesha. Hali hii pia ikiwa mteja anaweza kuishughulikia, kwa siku moja baada ya dozi ya mwisho ya misoprostol, dawa kama Loperamide zinaweza kutolewa kwa mwanamke kama zinahitajika.

Joto mwilini na Kibaridi

Kupata joto jingi mwilini kunahusishwa na kiwango cha misoprostol na mbinu ya matumizi. Kiwango kikubwa cha joto hutokana na kutumia kwa kuweka chini ya ulimi. Hata hivyo, kuna tofauti za kiurithi na kimakundi katika jamii kuhusiana na hili. Wanawake wengi wanaotuma dawa kwa kutia chini ya ulimi hupata joto jingi pamoja na kijibaridi. Joto jingi hushuhudiwa saa 1-2 baada ya kutumia misoprostol na huisha baada ya masaa 8 ya dozi ya mwisho. Ibuprofen husaidia kusuluhisha tatizo hili. Kama hiyo haitoshi, paracetamol inaweza kutumiwa pamoja na Ibuprofen. Hata hivyo, kuwa makini kwa kiwango cha matumizi ya dawa za NSAIDS katika masaa 24.

6.3) Dalili za maonyo ya madhara na jinsi ya kuziangazia

Uavyaji mimba kwa njia ya kutumia dawa ni njia salama na kuna matatozo machache ya kiafya yanayoambatana. Hata hivyo, ni muhimu kwamba wanawake wanapata habari kamili za dalili za maonyo wakati wa matatizo na jinsi ya kuyashughulikia kwa mapema ili kuepuka madhara. Dalili za matatizo ya kiafya yanayohusiana na matumizi ya dawa za kuavya mimba ni -

 • Kutokwa damu kwa wingi Hii inweza kukadiriwa kwa kujaza tauli mbili za hedhi kwa saa moja na kwa masaa mawili mfululizo, hasa unapoambatana na unyonge, kuishiwa nguvu na uchovu.
 • Kutotokwa na damu au damu chache sawa na ya hedhi baada ya matumizi ya misoprostol. Hii ni ishara ya mimba iliyo kwenye tubu ya fallopia au uavyaji uliofeli.
 • Joto la nyusi 38°C (100.4°F) au zaidi, au ongezeko la joto siku moja baada ya dozi ya mwisho ya misoprostol kutumika.
 • Harufu mbaya inayotoka kwenye sehemu nyeti na/au majimaji yasiyo ya kawaida.
 • Maumivu makali ya tumbo baada ya kutumia misoprostol.
 • Kuhisi mgonjwa sana pamoja na au bila joto mwilini, kichefuchesu kisichoisha, kutapika au kuendesha kwa zaidi ya masaa 24.

Mwanamke ambaye anaona yoyote kati ya dalili hizi huenda anapitia hali mbaya na sharti atafute usaidizi katika kituo cha afya haraka iwezekanavyo. Katika kesi nyingi, madaktari wenye ufahamu huwashughulikia wagonjwa wa aina hii kwa urahisi. Katika kesi chache, wanawake wanaweza kulazwa hospitalini, kufanyiwa upasuaje, kuongezewa dmu au kupewa utunzaji wa hali ya juu.

Mwishoni mwa ushauriano na mgonjwa, ni vema kuhakikisha kuwa -

 • Mwanamke anaelewa wakati na jinsi ya kutumia tembe za mifepristone na/au misoprostol vikijumuisha dozi, mbinu ya matumizi na muda wa kuzitumia.
 • Hakikisha kuwa mwanamke anaelewa ni wakati gani na ni kwa njia gani anahitaji dawa zingine zikiwemo za maumivu na madhara mengine.
 • Hakikisha mwanamke anaelewa dalili za maonyo ambazo zitampelekea kupata usaidizi zaidi wa kiafya.
Somo la 7: huduma ya baada ya uavyaji mimba

Katika somo hili la mwisho, tutajadili habari muhimu ili kuwasaidia wanawake ambao wanatafuta huduma ya baada ya uavyaji mimba, kufuatia jaribio la kuavya mimba kwingine au uliofanywa nawe kuiondoa mimba ambayo haikuhitajika. Mwisho wa somo hili, utakuwa na uwezo wa kutoa huduma na usaidizi wa baada ya uavyaji mimba kwa wanawake kama vile katika uavyaji ambao haukukamilika, kujadili kurejea kwa uwezo wa kupata mimba na uangalizi unaohitajika na kutoa au kumwelekeza mwanamke kwa usaidizi zaidi wa huduma za afya ya uzazi.

7.1) Fuatilia hali ya wagonjwa wanaopitia uavyaji mimba kutumia dawa

Muda wa uavyaji mimba

Uavyaji huwa unafanyika kwa chini ya saa 24 baada ya kutumia tembe za mwisho za misoprostol. Hata hivyo, utaratibu mzima unaweza kuendelea kwa siku chache zinazofuatia. Wanawake wengi humaliza machakato wa uavyaji baada ya siku 7 huku wengine wakichukua muda zaidi. Kwa kuwa muda wa kupata maumivu na kutokwa damu hutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi kwa mwingine, ni vigumu kukisia vile hali itakuwa. Kadri mwanamke anapokea utokaji wa mimba na vyote vilivyomo kwenye nyumba ya uzazi, bila dalili za kutia shaka, hakuna kingine cha kufanya.

Kijumla, utokaji wa damu mwingi hufanyika wakati wa uavyaji mimba wenyewe. Hapa mwanamke hupata damu nyingi zaidi ya anavyopata wakati wa hedhi yenye maumivu. Kutokwa damu na maumivu hupungua baada ya mimba kutoka kikamilifu. Utokwaji wa damu sawia na ule wa wakati wa hedhi ya kawaida utaendelea kwa wiki mbili baada ya kuavya mimba. Hata hivyo, uzito na wingi wa utokwaji wa damu sharti upungue polepole.

Fuatilia baada ya uavyaji mimba -

Wanawake ambao wanatumia mifepristone na misoprostol kwa uavyaji wa mimba changa hawana haja ya kufuatiliwa na mhudumu wa kiafya, kama baada ya uavyaji mimba mgonjwa hahisi kuwa na mimba, hakuna dalili za madhara mabaya na utokaji damu unapungua.

Hata hivyo, wakati unatumia misoprostol tu, hadi asilimia 10 ya wanawake huripoti kuendelea kwa mimba. Hili linaonyesha kuwa misoprostol haijaweza kuiondoa mimba. Hivyo basi, watoaji huduma wanastahili kuwashauri wanawake kuhusiana na dalili za uendeleaji wa mimba na kutoa suluhisho mwafaka katika kuavya mimba kwa muda unaofaa. Kwa kawaida wanawake wanaopata damu chache inayotoka au hata kutotokwa na damu ni wale wanaotumia misoprostol na hupata dalili za mimba inayoendelea kukua na sharti wajulishwe kuhusu uavyaji uliofeli. Katika hali kama hii, wanawake wapewe maelekezo jinsi ya kutafuta usaidizi zaidi kutoka kwa daktari siku saba baada ya dozi ya mwisho ya misoprostol ili kubaini ukamilifu wa uavyaji mimba.

Pamoja na hayo, ibainike kuwa misoprostol inaweza kuhitilifiana na mtoto anayekua tumboni. Hivyo basi, iwapo uavyaji mimba unafeli na mimba inaendelea kukua, mtoto anayekua ana hatari ya kuzaliwa na matatizo ya kiafya ya mifupa, kichwa au hata ya neva pamoja na mengine. Wagonjwa sharti wafahamishwe kikamilifu kuhusu hatari hizi kuu iwapo wataamua kuiacha mimba kuendelea baada ya jaribio lililofeli.

7.2) Matibabu ya uavyaji mimba ambao haukukamilika

Ufafanuzi wa uavyaji mimba ambao haukukamilika unaweza kubadilika kutoka mazingira mamoja ya kiafya hadi mengine. Hata hivyo, ufafanuzi huu unakubalika; uavyaji mimba ambao haukukamilika ni hali ambayo baadhi ya sehemu za mimba inayoaviwa inabaki kwenye yumba ya uzazi.

Ni muhiu kutambua kuwa uavyaji ambao haukukamilika, licha ya kuwa unazua usumbufu kwa mgonjwa, unaweza kupelekea kupotezwa kwa damu mwilini na kuongeza hatari ya kupata maradhi. Hivyo, ni lazima kusimamiwa vema kuhakikisha kufanikiwa kwake. Kwa kuwa uavyaji mimba ni utaratibu, ni vyema madaktari kuuelewa utaratibu huu na wasihitilafiane nao katika kutaka kufahamu kama umekamilika au la. Mara nyingi, wanawake ambao wanatumia dawa za hali ya juu na wanaofuata maagizo na viwango vinavyostahili humaliza uavyaji wao kwa siku 7.

Uavyaji ambao haujakamilika unaweza kutibiwa kwa usimamizi unaotarajiwa, ambao unaruhusu uondolewaji wa vyote vilivyomo kwenye yumba ya uzazi, au kufanyiwa upasuaji au mbinu ya kutumia dawa. Usimamizi unaotarajiwa haupendelewi na wagonjwa wengi na madaktari kwa kuwa una mafanikio ya kiwango cha chini na muda unaochukuliwa kuondoa mabaki ya mimba haukadiriki. Mbinu ya upasuaji pia haipatikani kwa urahisi au pia haiwezekani. Matumizi ya misoprostol kwa uavyaji ambao haukukamilika na uliofanywa mapema ni njia salama na inayowezekana katika mazingira mengi.

Katika mazingira mengine, wanawake wenye mimba ambayo haikukamilika kuaviwa wnaweza kuwa na matatizo yanayoweza kuhusishwa na mbinu ya matumizi ya dawa za uavyaji mimba. Wanawake wanaweza kuwa na majeraha ya ndani au ya nje, kupata maradhi, kupoteza damu au/na tatizo la usambazaji wa damu mwilini. Pale ambapo wanawake wana dalili za maradhi ya uzazi, ya kimwili na shida za usambazaji wa damu, wanahitaji utunzaji wa hali ya juu. Hii inajumuisha uondoaji wa mara moja wa vyote vilivyomo kwenye nyumba ya uzazi kutumia mbinu ya upasuaji na utunzaji unaojumuisha matumizi ya antibiotics na IV fluids.

Mara tu baada ya kutambua kwamba mwanamke aliye na mimba ambayo haikukamilika kuaviwa anahitimu kwa vigezo vifuatavyo, anaweza kupata usaidizi wa kimatibabu wa kutumia misoprostol.

Vigezo vya kuhitimu kupewa usaidizi wa uavyaji ambao haukukamilika ni kama vifuatavyo -

 • Historia ya ujauzito wa hivi majuzi
 • Afya ya kizazi hasa saratani
 • Utokwaji wa damu kupitia njia ya uzazi au historia ya utokaji wa damu wakati wa mimba.
 • Ukubwa wa nyumba ya uzazi sawa na ule wa wiki 13 za ubebaji mimba, Fahamu kuwa hapa tunarejelea ukubwa nyumba ya uzazi wakati mwanamke anakuja na tatizo la uavyaji ambao haukukamilika na si umri ambapo mwanamke alienda kutafuata huduma za uavyaji mimba.
 • Kutokuwa na dalili za maradhi mengine.
 • Kutokuwa na tatizo la usambazaji damu mwilini au mshtuko.

Kuna chaguo mbili wakati wa kutoa dawa kwa ushughulikiaji wa uavyaji mimba ambao haukukamilika ambao haukuwa na tatizo.

Watoaji huduma wanaweza kupendekeza dozi moja ya 600mcg ya misoprostol ambayo inamezwa au dozi moja ya 400mcg ya misoprostol itakayotiwa chini mwa ulimi.

7.3) Uwezo wa kupata mimba baada ya uavyaji mimba

Uavyaji mimba ambao hauna tatizo hauna athari mbaya kwa uwezo wa mwanamke wa kupata mimba kwa siku za usoni. Kurudi kwa uwezo wa kushika mimba baada ya uavyaji mimba katika miezi mitatu ya kwanza hakubadiliki kwa sababu ya mbinu iliyotumika. Yai la uzazi linaweza kuachiliwa kwa siku 8 baada ya uavyaji. Takriban asilimia 83 ya wanawake hupata yai la uzazi kuachiliwa wakati wa mzunguko wa kwanza baada ya uavyaji.

Kama ilivyotajwa awali, ni muhimu kukubali kuwa vigezo vingi tofauti kwa kila mwanamke vinaweza kuathiri uamuzi wake wa kutafuta huduma ya uavyaji mimba. Ili kuheshimu haki za wa wagonjwa kikamilifu, wanawake wote wapewe habari zote muhimu kuhusiana na uwezo wa kupata mimba baada ya uavyaji.

Pale ambapo wanawake wanahitaji kupanga uzazi, wapewe papo na wakatu huo wa kuja kumwona daktari. Vigezo vya Shirika la Afya duniani vya upangaji uzazi vinapendekeza kuwa mbinu zote za upangaji uzazi za kisasa isipokuwa kifaa cha kuingizwa kwenye nyumba ya uzazi na upasuaji wa kufunga tubu za uzazi zinaweza kupeanwa kwa mwanamke wakati wa kutembelea kituo cha afya kutafuta dawa za uavyaji mimba. Kifaa cha kuingizwa kwenye njia ya uzazi na ufungaji wa tubu za uzazi kupitia upasuaji zinaweza kutumiwa tu kama uavyaji wa mimba utakuwa umekamilika.

7.4) Huduma zingine za kiafya ambazo zinahusiana na uavyaji mimba

Jambo jingine ambalo madaktari wanastahili kukumbuka ni kuwa, wakati wanawake wanaenda kutafuta huduma za uavyaji mimba ni nafasi nzuri ya kujifahamisha kuhusu huduma zingine za kiafya. Kwa maombi yake na pale inawezekana, mgonjwa anaweza kupata huduma zingine za kiafya zinazopatikana kwa wanawake.

Mtagusano kati ya daktari na mgonjwa unaweza kuwa nafasi nzuri ambayo itapelekea ongezeko la , upataji na matumizi ya huduma zingine za afya ya uzazi na afya kijumla. Njia moja ya kufanikisha haya ni kuhakikisha kuwa pale inawezekana, inakubalika na kufikiwa, daktari huhakikisha kuwa mwanamke anapata huduma zingine za kiafya hitajika wakati anakuja kutafuta matibabu ya matatizo yanayohusiana na uavyaji mimba, na ikiwezekana kwa kituo sawa cha afya.

Iwapo haiwezekani kwa kituo cha afya kumpa huduma zingine za kiafya, au pale mwanamke anaomba muda kulitafakari hili, mikakati ya kumtuma kwa kituo kingine au kufuatilia inaweza kuwekwa kuhakikisha mahitaji ya mwanamke yanatimizwa kwa njia ya heshima na isiyo ya kumshawishi. Kuwa makini wakati wa kumwelekeza mwanamke kwa hospitali nyingine au kupendekeza huduma zingine za kiafya kwake.

Huduma zingine za afya ya uzazi au afya kwa kijumla ambazo zinaweza kuangaziwa ni pamoja na -

 • utathmini wa unyanyasaji wa kingono, kinyumbani au unyanyasaji mwingine wa kijinsia.
 • elimu ya uzuiaji wa magonjwa ya zinaa/HIV, upimaji na utoaji wa matibabu.
 • kupima damu mwilini na elimu kuhusu lishe bora.
 • upimaji wa saratani ya kizazi na mapendekezo ya mahali pa matibabu.

Tovuti hii inaweza kuhitaji kuki zisizojulikana na huduma anuwai za mtu mwingine ili iweze kufanya kazi kunavyotakikana. Unaweza kusoma Sheria na Masharti yetu na Sera za Faragha . Ukitaka kuendelea kutumia tovuti hii, ni sharti utupe idhini ili uweze kufanya hivyo.